Kilichofutikwa ni uvundo

Kilichofutikwa ni uvundo

View attachment 393968sikutaka tuwe na post leo..ilikuwa tupumzike..mishemishe za kilingeni jana zilikuwa si haba
Lakini hebu tujadili kidogo hili la maiti(sio marehemu)
Maiti ni mzoga pumzi ikishatoka imetoka kinachofuata ni mchakato wa kuanza kuoza/kuvunda, kuharibika na baadae kuwa mabaki ya mwili na vile utakavyozikwa navyo kama ukibahatika kuzikwa (si kila mmoja anajaaliwa mazishi)
Pamoja na mazishi ya gharama sana pamoja na majeneza ya thamani kubwa pamoja na kuzikwa na Vito na vitu vingine vya thamani..kilichofutikwa humo ni uvundo mtupu......
Ukishafukiwa kifuatacho ni uvundo tuu hadi nyama zote zitakapoliwa na funza na bakteria chini ya ardhiView attachment 393975
Upuuzi wa wengi ni pale marehemu kabla ya kifo chake Kuteseka na kuugua sana bila misaada ya ndugu na marafiki...ama la kwa wale wanaojiweza kufanya mazishi ya kufuru kwenye mwili unaooza
Dhima ya kufanya yote haya ninini?
Sifa?
Upendo?
Kujali?
Kumbukumbu?
Kuiga?
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na jibu lake lakini vyovyote iwavyo tukubali tukatae kufuru kwenye mzoga wakati kuna watu bado wana uhitaji ni laana
Mimi huwa mgumu sana kutoa rambirambi. Kwann mgonjwa taarifa hazitoki kwa sauti kuliko umauti??

Unafiki wa mwanadamu ni laana ya ulimwengu.
 
Mimi huwa mgumu sana kutoa rambirambi. Kwann mgonjwa taarifa hazitoki kwa sauti kuliko umauti??

Unafiki wa mwanadamu ni laana ya ulimwengu.
Unafiki wa mwanadamu ni laana ya ulimwengu.[emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Burian Wicknell Chivayo na Lucy Muteke (Lulu)
1791394621845.jpg
 
THAMANI HALISI YA GENEZA LA CHIVAYO.

Inaelezwa kuwa geneza la Wicknell Chivayo limetengezwa kwa dhahabu yenye uzito wa karati 14 za dhahabu ambayo thamani yake inakadiriwa kuwa dola za Marekani 217,000 (US$217,000). Hii ni sawa Shilingi za Kenya 28 milioni au Shilingi za Tanzania 520 milioni.

Chivayo na mke wake Lucy Mukete (Lulu) waliuawa katika ajali ya Helikopta katika eneo la Marondera karibu na mji mkuu wa Zimbabwe ambao ni Harare. Chivayo alijenga ukaribu au urafiki mkubwa na Marais hawa: Mnangagwa (Zimbabwe), Ruto (Kenya) na Samia (Tanzania)

Marais wote walitoa salamu za pole huku Rais Samia akielezwa kwenda kwa siri kutoa mkono wa heri nyumbani kwa Chivayo na kuwa media na vyombo vya habari pamoja na waombolezaji hakuna aliyeruhusiwa kupiga picha wakati Rais Samia alipowasili nyumbani kwa Chivayo siku ya tarehe 6 Oktoba 2026.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Tanzania, 8 Oktoba 2026; Saa 4:15 jioni
1791470042121.jpg
 
MAKABURI YA FAHARI YA CHIVAYO NA LULU

Makaburi ya kifahari ya Wicknell Chivayo na mkewe Lucy Mukete (Lulu) yakiandaliwa katika Uwanja wa Sahwira Glenforest Memorial Park mjini Harare. Chivayo na Lulu watazikwa humu siku ya leo.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
8 Oktoba 2026
1791473445960.jpg
 
Back
Top Bottom