Kilichofanywa na Serikali ya Kenya siyo Tusi la Kidiplomasia kwa Serikali ya Tanzania?

Huku nyuma kuna Mtu mmoja aliwahi kuniambia kwamba ni kheri Mtu akakupiga tu Ngumi ya moja kwa moja au Kukutukana tu Tusi la moja kwa moja ujue moja kuliko kuyafanya yote mawili katika mwamvuli wa lugha ya Kidiplomasia kwani yanauma, yanaumiza na maumivu yake huwa ni ya muda mrefu pia.

Akaenda mbele na kuniambia kwamba hakuna kitu kibaya duniani kama pale Wewe unayejiona ni Mbabe au Mkorofi halafu ukamchokoza Mtu ambaye pengine unadhani ni dhaifu Kwako ukiwa na mategemeo makubwa kwamba na Yeye atakurudishia vile vile ili upate chanzo cha Kumdhuru halafu Yeye ( uliyemchokoza ) badala ya kukujibu kwa Shari / Ugomvi badala yake anakujibu kwa Hekima na Busara kwani hilo huwa ni tusi kubwa na baya mno la Kidiplomasia.

Yawezekana Serikali ya Kenya imebobea sana katika matusi ya Kidiplomasia kwani ama hakika kwa Vitendo vya siku za karibuni ambavyo vimefanywa na Serikali ya Tanzania dhidi ya Mifugo na Bidhaa za Kenya usingetegemea kama Wakenya wange hundle hii situation in a diplomatic manner like this badala yake sasa inaonekana kabisa kwamba Serikali ya Tanzania ndiyo imepata aibu na imetukanwa vibaya mno Kidiplomasia.

Vitendo vya Kuwafidia Wafugaji waliopoteza Mifugo yao huku mpaka sasa wakifanya mazungumzo ya kurudisha zile Ng'ombe kadhaa kutoka Tanzania zilizokamatwa katika ardhi yao tofauti na ambavyo Sisi tumefanya kama kutaifisha Mifugo yao na hata Kuchoma moto hadharani ni Tusi la Kutukuka si tu kwa Serikali ya Tanzania bali na kwa Watanzania wote.

Mwisho nimalizie kwa kusema tu kwamba kama Wabobezi wa Diplomasia nchini Tanzania hawatashtuka na kuamka ili kuliingilia hili kati kuna hatari kila siku tukaendelea Kutukanwa Kidiplomasia na si tu Wakenya bali hata Mataifa mengine ambayo yanajielewa. Serikali ya sasa ya Tanzania ipitie upya aina ya Diplomasia yake na isione pia shida / tabu kuomba ushauri kwa Baba wa Diplomasia nchini Tanzania Rais mstaafu wa awamu ya Nne Mzee Jakaya Mrisho Kikwete.

Kosa la Mtu mmoja linatusababishia Watanzania wote katika macho ya Kimataifa tunaonekana ni wa hovyo hovyo. Hapana hili halikubaliki na huyu Mhusika ikiwezekana afundishwe jinsi ya kuishi na Watu hasa Majirani na kuheshimu Uhusiano wa muda mrefu wa Kidiplomasia wa Tanzania na nchi zingine kwani Tanzania siyo Kisiwa na ipo siku hawa hawa ambao leo tunawachokoza tutawahitaji kwa namna moja au nyingine. Namwomba abadilike upesi sana na ikiwezekana hata huu uzi wangu apewe wote kama ulivyo ausome ili ayajue mapema mapungufu yake Kimataifa. Tumechoka and We need peace in East Africa please!!!!!!!

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambayo siku zote huwa haikai na uchafu halafu sijazoe Unafiki bali nanyoosha tu hata kama ni Kipenzi changu au ni Adui yangu.

Nawasilisha.
Unaijua Diplomasia wewe???? Humjui Mkenya Vizuri wewe kiumbe
 
programmer95 ,

Mkuu, ndiyo hivyo.

Tatizo watu wengi na nchi jirani zilikuwa zinatuchukulia poa sana.

Ila sasa, Hapa ni Maslahi ya Taifa, ,,,, "Tanzania Kwanza"
Maslahi ya kwanza ya Taifa ni uchumi wa Taifa lako. Utakuwa mpumbavu kama unafanya jambo lolote ambalo litaathiri uchumi wako halafu unasema unasimamia maslahi ya Taifa lako.

Bidhaa zetu nyingi zinaenda Kenya kwa sababu wana viwanda na pia wana masoko ya uhakika nje. Ni lazima uende kwa akili, taratibu ili siku moja na wewe uwe na viwanda vyako vyenye uwezo wa kushindana, na uweze kuyapata masoko ya kimataifa bila ya kupitia kwa wengine.

Watalii wanaokuja Tanzania, zaidi ya 60% wanapitia Kenya. Japo na wao wanafaidika kwa kutumia vivutio vyetu lakini na sisi tunafaidika.

Fuatilia jinsi machafuko ya kisiasa ya Kenya yalivyoathiri sekta ya utalii Tanzania. Uchumi ni werevu, ni akili na umakini wala siyo mabavu au misuli.
 
Vipi uhusiano wa Kenya na nchi zingine za EAC ukiacha Tanzania ni wakuridhisha?Au ni ule urafiki wa kawaida wa kupeana salam tu?
Uhusiano wa Kiuchumi kati ya Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda ni mzuri. Ndiyo maana mpaka sasa mataifa haya yanapitisha mizigo yake mingi Kenya kuliko Tanzania. Lakini pia Kenya na Uganda zimekuwa zikiilaumu Tanzania kuchelewesha mambo mengi yaliyokubaliwa kwenye mikutano ya EAC. Lakini pia usisahau kuwa nchi ya Kenya, kiuchumi ipo juu kushinda nchi nyingine zote za EAC zikiwekwa pamoja. Ni hulka ya watu dhaifu kumchukia anayewazidi.
 
Hamieni Kenya chuki zenu na mtu zisiwapotezee uzalendo na nchi...naweza kuuchukia utawala ila nchi yangu kwanza.!.. Sijui mnafurahi kusifua wakenya wapo smart eti wamesoma na hujawahi kufika hata namanga au horo horo unasoma habari za mtandaoni...mefikia hatua mbaya sana ya kutaka tuonekane wajinga,tushindwe kula kitu nchi ikwame just because tunamchukia mtawala...ni upuuzi na kukosa kujitambua magufuli atapita nchi itabaki hata Rais awe nani watu hatuwez kuwa sawa na hata rais awe nani hakuna atakae kuletea hela nyumban mambo yanapoharibika ni kwa wote now uchumi umekuwa mgumu ni kwa wote hakuna anaefurahishwa ila siwez kusaliti nchi na nikafurahia watu wa mataifa mengine kuitukana nchi yangu....kama kizazi cha leo ndio kingetakiwa kupigania uhuru tusingeupataga kamwe.!.. Manakera sana too negative on everthing.!
 
Na mnapotaka kuzungumzia mabingwa wa diplomasia hapa africa Heshima ya Tanzania huwez kuiweka mizan moja na Kenya tulisitisha nchi zote zenye migogoro kimbilio lao ni hapa tanga wanatafuta uhuru....ruksa kuuchukia utawala na serikali yake ila nchi yako kamwe..!..hata china ilipotaka irudi umoja wa mataifa ilikuja hapa tulisitisha uhusiano na Uingereza na ujeruman mgogoro wa Bi afra..nambie Kenya ina uzito gani kwenye diplomasia za kiafrica na kidunia kulinganisha na Tz.!
 
Uhusiano wa Kiuchumi kati ya Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda ni mzuri. Ndiyo maana mpaka sasa mataifa haya yanapitisha mizigo yake mingi Kenya kuliko Tanzania. Lakini pia Kenya na Uganda zimekuwa zikiilaumu Tanzania kuchelewesha mambo mengi yaliyokubaliwa kwenye mikutano ya EAC. Lakini pia usisahau kuwa nchi ya Kenya, kiuchumi ipo juu kushinda nchi nyingine zote za EAC zikiwekwa pamoja. Ni hulka ya watu dhaifu kumchukia anayewazidi.
Hiyo ya Uganda kuilaumu Tanzania nakusikia ww labda unipe maelezo kidogo.Lakini pia siamini kama kuwa mbele Kenya kiuchumi ndo sababu kubwa za hii migogoro ila naweza kubaliana nawe kwamba mfumo wa uendeshaji siasa au nchi wa Kenya na Tanzania au nchi zingine unaathiri pakubwa sana diplomacy ya hizi nchi.Kenya wanatumia sana democratic leadership style wakati hizi nchi nyingine ni autocratic leadership style. Na kwa siasa za Tanzania kuingilia siasa za Kenya naona nalo ni Ttz sana kwa diplomacy.Viongoz wakuu wa UPINZANI tena wanaoshindana na jpm kila siku kushirikiana na kenyata nafikir ni kitu kinachochochea mvurugano huu diplomacy. Mgogoro naona uko kisiasa sana licha kuna mambo ya bomba la mafuta.
 
Bams,

Kama ungeelewa kwa nini Kenya inailaumu Tanzania huko kwenye EAC usingeandika sana kiasi hicho.

Any way, wanaoona kuwa Kenya imeonewa juu ya mifugo na vifaranga basi wahamie Kenya kama baadhi walivyofanya kwenda kuishi Kenya na mgonjwa na wengine wakapeleka "Actually" nyiingii kwenye media za Kenya.
 
df4ac3f42d59710c745ce6d6dab8c6c3.jpg
40fcbcebfdab027cae67e30c3b107272.jpg
magari ya jeshi toka kenya yakileta msaada Tanzania wakati wa tetemeko bukoba.
 
Huku nyuma kuna Mtu mmoja aliwahi kuniambia kwamba ni kheri Mtu akakupiga tu Ngumi ya moja kwa moja au Kukutukana tu Tusi la moja kwa moja ujue moja kuliko kuyafanya yote mawili katika mwamvuli wa lugha ya Kidiplomasia kwani yanauma, yanaumiza na maumivu yake huwa ni ya muda mrefu pia.

Akaenda mbele na kuniambia kwamba hakuna kitu kibaya duniani kama pale Wewe unayejiona ni Mbabe au Mkorofi halafu ukamchokoza Mtu ambaye pengine unadhani ni dhaifu Kwako ukiwa na mategemeo makubwa kwamba na Yeye atakurudishia vile vile ili upate chanzo cha Kumdhuru halafu Yeye ( uliyemchokoza ) badala ya kukujibu kwa Shari / Ugomvi badala yake anakujibu kwa Hekima na Busara kwani hilo huwa ni tusi kubwa na baya mno la Kidiplomasia.

Yawezekana Serikali ya Kenya imebobea sana katika matusi ya Kidiplomasia kwani ama hakika kwa Vitendo vya siku za karibuni ambavyo vimefanywa na Serikali ya Tanzania dhidi ya Mifugo na Bidhaa za Kenya usingetegemea kama Wakenya wange hundle hii situation in a diplomatic manner like this badala yake sasa inaonekana kabisa kwamba Serikali ya Tanzania ndiyo imepata aibu na imetukanwa vibaya mno Kidiplomasia.

Vitendo vya Kuwafidia Wafugaji waliopoteza Mifugo yao huku mpaka sasa wakifanya mazungumzo ya kurudisha zile Ng'ombe kadhaa kutoka Tanzania zilizokamatwa katika ardhi yao tofauti na ambavyo Sisi tumefanya kama kutaifisha Mifugo yao na hata Kuchoma moto hadharani ni Tusi la Kutukuka si tu kwa Serikali ya Tanzania bali na kwa Watanzania wote.

Mwisho nimalizie kwa kusema tu kwamba kama Wabobezi wa Diplomasia nchini Tanzania hawatashtuka na kuamka ili kuliingilia hili kati kuna hatari kila siku tukaendelea Kutukanwa Kidiplomasia na si tu Wakenya bali hata Mataifa mengine ambayo yanajielewa. Serikali ya sasa ya Tanzania ipitie upya aina ya Diplomasia yake na isione pia shida / tabu kuomba ushauri kwa Baba wa Diplomasia nchini Tanzania Rais mstaafu wa awamu ya Nne Mzee Jakaya Mrisho Kikwete.

Kosa la Mtu mmoja linatusababishia Watanzania wote katika macho ya Kimataifa tunaonekana ni wa hovyo hovyo. Hapana hili halikubaliki na huyu Mhusika ikiwezekana afundishwe jinsi ya kuishi na Watu hasa Majirani na kuheshimu Uhusiano wa muda mrefu wa Kidiplomasia wa Tanzania na nchi zingine kwani Tanzania siyo Kisiwa na ipo siku hawa hawa ambao leo tunawachokoza tutawahitaji kwa namna moja au nyingine. Namwomba abadilike upesi sana na ikiwezekana hata huu uzi wangu apewe wote kama ulivyo ausome ili ayajue mapema mapungufu yake Kimataifa. Tumechoka and We need peace in East Africa please!!!!!!!

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambayo siku zote huwa haikai na uchafu halafu sijazoe Unafiki bali nanyoosha tu hata kama ni Kipenzi changu au ni Adui yangu.

Nawasilisha.
Watanzania wengi wako namna hii, too emotional.
Mkuu, samahani kama nimekukwaza ila ukweli ni kuwa uwezo wako wa kuelewa mambo kwa upana upo too low.
Or may be niamini unafanya makusudi.
 
Hakuna Binadamu ambaye amekubaliana na Mwenyezi Mungu kuwa ataishi Milele hapa duniani halafu moja ya Utamaduni wa Kabila langu la Kizanaki ni kuwa mkweli, siyo mwoga, siyo mnafiki, simamia katika haki, rekebisha kwa minajili ya kujenga na kutomuonea Mtu haya hata kama anakulisha au anakunywesha brandi ( pombe )

Kama leo wataniona Mimi nimekuwa adui yao kwa kuwaambia huu ukweli bali na wao pia si vibaya wakajiuliza kwamba ni kwanini mara nyingi pia nimekuwa nikiwasifia / nikiwapongeza humu kwa mengi tu na hata muda mwingine nikipambana na maadui zao wakubwa Kisiasa Watu wa CHADEMA na wala hawajanifuata na hizo Nissan Patrol zao kunipa ama Tuzo au hata Zawadi tu ya Pesa?

Kwahiyo GENTAMYCINE anaonekana tu mzuri Kwao pale akiwanganga maadui zao ila akiwagusa wao anakuwa mwiba mchungu / adui yao? Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba hata katika maisha yangu nilipata pia malezi kidogo kutoka kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere pale Msasani hivyo kukaa nae kule alinifunza mengi na nilijifunza mengi pia hivyo nitayaiga yale yote aliyokuwa akiyafanya. Nina uhakika hata Yeye ( Nyerere ) kama angekuwepo hai hivi leo basi huu upuuzi / upupu wa Kidiplomasia unaoendelea angeukemea tena kwa ukali zaidi.

Poise siogopi Kufa Mkuu wangu tena hata kama Wewe unanijua vyema tu nakukaribisha muda na wakati wowote ule uje uniue ili nikamfuate na nikaungane na Babu yangu Mwalimu Nyerere huko Kaburini aliko kusudi niweze kumweleza haya mambo ya hovyo hovyo yanayoendelea sasa na yanayoshika Kasi pia.

Tena kama wamekutuma kawaambie kwamba sitobadilika katika kufanya analysis zangu humu JF na siku zote nitakuwa 50/50. Nimemaliza
huna lolote wewe.
 
Wachezeeni hao hao Wakenya ila siyo Wanyarwanda. Wenzako walio katika Vitengo wanajua uwezo na nguvu ya Kivita iliyo nayo Rwanda. Narudia tena kusema na kusisitiza Kwako tena kwa jeuri kubwa kabisa kamba wachezeeni hao hao Wakenya ila msije mkakosea mkajichanganya wa Rwanda na Wanyarwanda kwani ndani tu ya muda mfupi Tanzania yeu itakuwa mali ya Rwanda. Naomba niishie hapa tafadhali. Halafu mada iliyopo mezani ni suala la Kenya na Tanzania hili la Rwanda hapa limeingiaje? Mbona unakuwa kama vile Mwanamke Malaya ambaye anataka kupigwa Paipu?
Ng'ombe zaidi ya 10,000 kutoka Uganda na Rwanda watapigwa mnada karibuni.
 
Kwa Watanzania wale tu waliozunguka nchi za watu na wale wanaoishi mipakani ndio watakaokuelewa vizuri kuhusu uzito wa hoja yako.

Kifupi hii serikali inatuharibia sawa wakazi wa mipakani.
Mkuu hao watu wanaotetea kuingiza mifugo kienyeji nchi mwao kwa kigezo cha diplomasia wakati unahatarisha maisha na uchumi wa mamilioni ya raia wako waambie wakazungukie na UK, USA na Australia wakaingize kifaranga kimoja cha kuku na ngombe hai angalau mmoja tu bila vibali wala chanjo ya magonjwa kisha waje watufunze diplomasia waliyokutana nayo huko.
 
Sheria ya nchi IPO wazi ikivunjwa lazima itekelezwe ipasavyo.kama Sheria imezuia Mifugo ya nje kuingia nchini kiholela bila kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria hiyo ikafafanua adhabu itakayotolewa kwa atakayekiuka Sheria / utaratibu huo mfno.Kupiga mnada , kuchoma,jela au vyote kwa Pamoja.

Kama imetekelezwa sheria tukae kimya na tuwapongeze walio simamia hiyo Sheria kwani tumezitunga kwa maslahi mapana ya Taifa. Tusiishi kwa Mazoea kwamba zamani mbona ukikamatwa unatoa kitukidogo wanakuachia hawa wa Leo wapo kazini kwa Maslahi ya Taifa siyo kwa maslai yao binafsi.

DIPLOMASIA INGEFAA KAMA HAO WATU HAWAJA VUNJA SHERIA YA NCHI NA WAMECHOMEWA AU KUPIGWA MNADA MIFUGO YAO. WEWE NENDA KWAO KAVUNJE SHERIA YA NCHI YAO ALAFU WAO KAMA WATATAKA DIPROMASIA LAZIMA WATAFUTA SHERIA INASEMAJE NA WAITEKELEZE.
Ni nini Maana ya Diplomasia?!
 
Mkuu hao watu wanaotetea kuingiza mifugo kienyeji nchi mwao kwa kigezo cha diplomasia wakati unahatarisha maisha na uchumi wa mamilioni ya raia wako waambie wakazungukie na UK, USA na Australia wakaingize kifaranga kimoja cha kuku na ngombe hai angalau mmoja tu bila vibali wala chanjo ya magonjwa kisha waje watufunze diplomasia waliyokutana nayo huko.
Mtafute Bwana mmoja anaitwa Richard Osburn niliwahi kukuta amekaririwa katika issue kama hii... USA- Canada border kuna msuguano mkubwa mpaka serikali ikabidi ishauriwe kuangalia namna ya kuaccomodate maisha ya hawa watu mpakani.. Walikuwa wanafungwa kuvuka upande mwingine ilhali wao ni ndugu na hii mipaka(Artificial lines) imewakuta wakiishi hivyo...
Japo Russia na Marekani ni mahasimu ila kuna jamii za watu wa Alaska wanashare tamaduni na udugu na wa warusi..kuna mambo kama haya lazima utaheshimu tu hakuna namna...

Diplomasia ndio kama Marekani na Canada wanavyochukua muda kuliangalia na kulifanyia utaratibu wa kuwaruhusu kuishi bila mvutano kwa upendo kama ndugu japo wanabeva vitambulisho tofauti..

Mfamo.mzuri hapa kwetu ni ile migration ya wanyama pori.. Kwann tusi wajengee ukuta wasiende Kenya?!.. Watakufa waishe.. Ndio hivyo hivyo kwa wafugaji wataenda Kenya kipindi malisho yamedorora Tanzania... Na watarudi Tanzania wakati malisho yamedorora Kenya...

Nadhani kama wataalam wangetena maeneo machache yatumike kwa ajili hiyo kwa pande zote mbili.. Upande Wa Kenya wawe na Maeneo yatakayo lisha mifugo ya watanzania wakati Wa ukame na Tanzania watenge maeneo yatakayolisha ng'ombe Wa Kenya..

Japo wote kila MTU kwa nchi yake awe na enforcement mechanism yake kuhakikisha hakuna anayekwenda pasipotakiwa.. Hii itasaidia kudhibiti magonjwa na uharibifu wa Mazingira.. Na overcrowding... Maana ngombe watafugwa kulingana na maeneo kila nchi ipo tayari kutenga kuwalisha ng'ombe wa jirani...

tusipofanya hivyo mapori ya ndani yatavamiwa... Migogoro ya wakulima na wafugaji..na uharibifu wa mazingira kwa ujumla..au ng'ombe watakufa.. Na kuathiri jamii za kifugaji.
 
Utamaduni wa Kabila langu la Kizanaki ni kuwa mkweli, siyo mwoga, siyo mnafiki, simamia katika haki, rekebisha kwa minajili ya kujenga na kutomuonea Mtu haya hata kama anakulisha au anakunywesha brandi
Hayo uliyo yasema kama ni kweli mbona unasifia wakenya walilo fanya? Mbona unataka Tanzania isiwaaambie ukweli WaKenya kwamba kulisha mifugo nchi ya jirani bila ruhusa ni makosa na hatua kali zitachukuliwa?
 
Mtafute Bwana mmoja anaitwa Richard Osburn niliwahi kukuta amekaririwa katika issue kama hii... USA- Canada border kuna msuguano mkubwa mpaka serikali ikabidi ishauriwe kuangalia namna ya kuaccomodate maisha ya hawa watu mpakani.. Walikuwa wanafungwa kuvuka upande mwingine ilhali wao ni ndugu na hii mipaka(Artificial lines) imewakuta wakiishi hivyo...
Japo Russia na Marekani ni mahasimu ila kuna jamii za watu wa Alaska wanashare tamaduni na udugu na wa warusi..kuna mambo kama haya lazima utaheshimu tu hakuna namna...

Diplomasia ndio kama Marekani na Canada wanavyochukua muda kuliangalia na kulifanyia utaratibu wa kuwaruhusu kuishi bila mvutano kwa upendo kama ndugu japo wanabeva vitambulisho tofauti..

Mfamo.mzuri hapa kwetu ni ile migration ya wanyama pori.. Kwann tusi wajengee ukuta wasiende Kenya?!.. Watakufa waishe.. Ndio hivyo hivyo kwa wafugaji wataenda Kenya kipindi malisho yamedorora Tanzania... Na watarudi Tanzania wakati malisho yamedorora Kenya...

Nadhani kama wataalam wangetena maeneo machache yatumike kwa ajili hiyo kwa pande zote mbili.. Upande Wa Kenya wawe na Maeneo yatakayo lisha mifugo ya watanzania wakati Wa ukame na Tanzania watenge maeneo yatakayolisha ng'ombe Wa Kenya..

Japo wote kila MTU kwa nchi yake awe na enforcement mechanism yake kuhakikisha hakuna anayekwenda pasipotakiwa.. Hii itasaidia kudhibiti magonjwa na uharibifu wa Mazingira.. Na overcrowding... Maana ngombe watafugwa kulingana na maeneo kila nchi ipo tayari kutenga kuwalisha ng'ombe wa jirani...

tusipofanya hivyo mapori ya ndani yatavamiwa... Migogoro ya wakulima na wafugaji..na uharibifu wa mazingira kwa ujumla..au ng'ombe watakufa.. Na kuathiri jamii za kifugaji.
Umeongea mengi mazuri yenye kujenga lakini hii diplomasia ifanywe kwa mambo mengine sio kuvusha mifugo kienyeji bila taratibu za kudhibiti magonjwa na pia janga la uharibifu wa mazingira kutokana na ufugaji holela ni kubwa sana hapa kwetu.

Tayari hapa nyumbani tuna migogoro mikubwa na nchi inakuwa jangwa kwa kasi maeneo ya wafugaji, athari zake ni kubwa mno sio za kuzichukulia kirahisi na kutaka kuwafurahisha jirani. Ile njaa na ukame wa Kenya utakuja kwa kasi zaidi.

Diplomasia ifanyike kwenye mambo ya ukanda huru wa kibiashara na ajira n.k. sio mambo ya afya na mazingira.

Huo ujirani mwema wa Marekani na Mexico sio kuingiza bidhaa za chakula au mifugo hasa hai bila vibali na animal disease control. Au kurusu kuchunga wanyama ovyo hata kwa wafugaji wa ndani ni kosa na hatua za kisheria zinachukuliwa.
 
Back
Top Bottom