Kilichobaki Zanzibar ni nini? ndo tumemaliza?

Mtu yeyote ambae amewahi kuwa Mwana CCM abadan hatoweza kuwatoa CCM kwenye Uchaguzi. Tusubiri kizazi ambacho hakijawahi kuwa na Kadi ya CCM. "...sikiliza Tido, kwa kifupi sana fahamu kuwa CCM haitotolewa Madarakani na Makapi yaliyotokana na CCM"-Comrade Abdulrahman bin Omar bin Kinaanah Al Habshy.
Nimeipenda sana hii nukuu umenikumbusha mbali kaka.
 
Mkuu nina u hakika hujafanya uchunguzi kuhusu hayo unayoyasema, nakubaliana tu na wewe kuhusu issue ya umri wa maalim Seif lakini kuhusu kupotea kwa CUF sidhani, go and do your homework properly. CUF walitangaza kususia uchaguzi na wakaeaomba hata wafuasi wao wasiende kupiga kura, taarifa zilizopo humu (kuna Uzi humo humu ndani) zinaonesha out 500,000 voters only 58,000 voters ndio walio turn up na kati yao 47,000 waliipigia KURA ccm, tafsiri ya haraka haraka inanambia bado Wazanzibari wengi waliitikia wito wa Maalimu Seif na CUF yao, kundi hili la waluogoma ni kubwa sana, binafsi ningependa sana hekima na busara itumike sana huko Zanzibar kwasababu hata watawala wana jua ushindi wa kule ulifanyikia maabara.
Inaumiza na kusikitisha sana. Sijui haya madhila ya ukandamizaji yataisha lini. Nadhani mpaka siku CCM ije kutoka madarakani Mola wangu atakua ashachukua roho yangu nipo kaburini. Na hii si hapa kwetu tu the rest of Africa ambapo kuna serikali dhulmat kama hii ya hapa kwetu. Inaniumiza sana!
 
Ngoja tusubiri tuone kama picha ndio limeisha au ndiyo linaanza.
 
Tusilaumu cuf na wa zanzibar, wanajeshi walio letwa zanzibar hawana ndugu zao huku na walikuwa wako tayari kutuuwa sote Wazanzibari, tatizo kubwa lipo kwa ukawa nzima imeshindwa kusimamia democracy ya Tanzania kwa vile chadema wamrporwa ushindi wakaamuwa kutowaunga mkono Wazanzibari.
Wakati wanajeshi wanapelekwa zanzibar ukawa Tanzania tanganyika ilikuwa ifanye maandamano nchi nzima kupinga utawala wa Kidekteta unao fanywa zanzibar
 
Maalimu Seif ndiyo CUF na CUF ni Maalimu Seif, hivyo basi kama Hali haitamruhusu kugombea 2020, hali itakuwa tete. Maalimu aliwekeza kwa wapemba alipokuwa kiongozi kwa mambo mema kadhaa aliyowatendea na sasa wanalipa fadhila viongozi wengi mnapaswa kujifunza kutokana na hili. Kwa hiyo basi wapemba hawachagui chama bali wanamchagua mtu. Hili ndilo linakuwa tatizo mzee atakaposema basi kugombea. Anapaswa kuweka mazingira bora ya atakaemuona anafaa kuchukuwa nafasi yake atakapostaafu siasa ili wafuasi wake wabadilike mapena kisaikologia vinginevyo itakuwa mtihani kwa CUF na nderemo kwa CCM.
 
Mtu yeyote ambae amewahi kuwa Mwana CCM abadan hatoweza kuwatoa CCM kwenye Uchaguzi. Tusubiri kizazi ambacho hakijawahi kuwa na Kadi ya CCM. "...sikiliza Tido, kwa kifupi sana fahamu kuwa CCM haitotolewa Madarakani na Makapi yaliyotokana na CCM"-Comrade Abdulrahman bin Omar bin Kinaanah Al Habshy.
Hakika Andiko Lako Ni lenye kufikirisha!
 
Walishasema hata uchaguzi utumie Nini hawang'oki...!! Issue hapa Ni kwamba Hakuna UCHAGUZI WA KWELI wenye uwazi Na ukweli.

Kama siku tutafanikiwa kupata uchaguzi wenye uhuru, uwazi Na haki basi hapo tutakua tumefanikiwa, Ila kinyume chake tutaendelea Kua Na UPINZANI WA KUSADIKIKA!

NB; waambieni watawala Kua Kututawala haina maana Kua wao Ni magenious Au wana IQ KUBWA zaidi yetu watawaliwa! Tunaona, Tunasikia, Tunaelewa kila hatua wanayopiga kwenda mbali Na sisi baada ya uchaguzi.
 
Acha watanzania tumeamua kuendelea na umasikini chini ya Ccm maana ccm kuwa madarakani ni muhimu kwetu kuliko maendeleo yetu
Sijajua mwaka 2020 Maalim Sharrif atakuwa na miaka mingap. Lakini ni waz kuwa umri wake utakuwa umeenda na waswas wangu ni zaid hata afya yake sijajua itakuaje. Mimi si Mungu wala Mtabiri lakini ni wazi atakuwa na athari kwa sababu kadhaa wa kadhaa.Nmeuliza so suala la Zanzibar linaendeleaje au limekuaje sasa? Ni wazi cuf wamepoteza na sasa wamejipoteza kwenye siasa za visiwani humo kabisa. Mwaka 2020 utakuwa ni mwaka rahisi sana kwa CCM upande wa Bara na Visiwani. Watashinda kwa urahisi sana maana watu weng wameshakata tamaa. Vyama vya upinzani vimeonekana kukosa nguvu kabisa. Vimenyong'onyea, vimeanza kukonda, sauti zao hazitoki tena au hazisikiki. Napata waswas na demokrasia ya vyama ving ambayo sasa imeshazikwa. Ni ngumu kwa miaka ya hapa karibun kupata vuguvugu na ari ya mwaka 2015 .itachukua miaka mingi sana. Je la Zanzibar ndo limeisha? Kama hivyo tu?
 
CCM itatawala kwa miaka mingi sana. Mhe. Kafulila alisema bungeni kuwa kama upinzani utashindwa kuchukua dola ktk uchaguzi wa 2015 basi itachukuwa zaidi ya miaka 100 ccm kuondoka madarakani.
 
Zanzibar ni zaidi ya CCM na CUF .Zanzibar kuna magroup hata kusiwe na chama hata kimoja hayaondoki.
Group la kwanza :Wahafidhina hawa liwalo na liwe ila serikali ya mapinduzi na baraza la mapinduzi lisiondoke.
Hawa wengi ni CCM na wanapigia chapuo muungano kwa sababu ya madaraka na maslahi binafsi.

Group la pili:Group la pili ni wanaharakati ,wapenda mabadiliko,Wanaotaka haki zao ndani ya Muungano.Wana chukia unyanyasaji .Wenye kujitambua.Group hili wengi ni wapinzani hasa kutoka CUF .Group hili linaongezeka idadi kwa sababu kila anaejielewa hujieka group hili.

Group la Tatu:Ni la upemba na Unguja hili tunajitahidi kuliua.

Group la nne: Watanganyika: Group hili ndilo group linalofanya maisha ya wapinzani zanzibar kua magumu sana.Wakitoka Tanganyika hawa hupewa sumu na wahafidhina kua wapinzani na wanaharakati wataleta waarabu,wabaguzi,Wanataka kuvunja muungano,Hawakupendeni.Group hili kidogo lowasa ali neutrilse asilimia kubwa ikawa mguu nje mguu ndani.
Lakini hili ndio group linalotumiwa zaidi na CCM.Group hili lina maslhi
MAkubwa ndani ya kisiwa cha zanzibar katika ngazi ya utalii,80% ya ajira za utalii wananufaika .

CUF inaweza kufa lakini kumbuka kwamba sisi ni kama tunadai uhuru kwa mara nyengine kwa hivyo harakati zinaweza kuja kivyengine ambazo hua ni hatari zaidi mfano za uamsho.

Utakiwa usali uombe CUF isife ndio pekee inazalisha amani kwa njia ya demkrasia .Wazanzibar wakirafta haki yao kwa njia nyengine basi amani ya baadhi ya magroup itapotea kabisaa
 
Sijajua mwaka 2020 Maalim Sharrif atakuwa na miaka mingap. Lakini ni waz kuwa umri wake utakuwa umeenda na waswas wangu ni zaid hata afya yake sijajua itakuaje. Mimi si Mungu wala Mtabiri lakini ni wazi atakuwa na athari kwa sababu kadhaa wa kadhaa.Nmeuliza so suala la Zanzibar linaendeleaje au limekuaje sasa? Ni wazi cuf wamepoteza na sasa wamejipoteza kwenye siasa za visiwani humo kabisa. Mwaka 2020 utakuwa ni mwaka rahisi sana kwa CCM upande wa Bara na Visiwani. Watashinda kwa urahisi sana maana watu weng wameshakata tamaa. Vyama vya upinzani vimeonekana kukosa nguvu kabisa. Vimenyong'onyea, vimeanza kukonda, sauti zao hazitoki tena au hazisikiki. Napata waswas na demokrasia ya vyama ving ambayo sasa imeshazikwa. Ni ngumu kwa miaka ya hapa karibun kupata vuguvugu na ari ya mwaka 2015 .itachukua miaka mingi sana. Je la Zanzibar ndo limeisha? Kama hivyo tu?
naona bora ukatafute bangi halafu unywe gongo ndio utakuwa ok. hivi nimpuuzi gani wa maisha asiyejuwa kuwa CCM inatawala kwa mabavu ivi unaona hii tume ya huyu mganga njaa lubuvu sio ya CCM hivi wewe hujuwi hili linaloitwa POLISI kama ni tawi la CCM hivi ww hujuwi kama hili linaloitwa usalama wa taifa ni tawi la CCM
 
Suala la zanzibar ni la kihistori. Hayo makundi unayoyataja na athari zake ni hali iliyokua kabla na baada ya mapinduzi.
Kabla ya mapinduzi Kuna kundi lilinyanyasika sana.
Na Kuna kundi Lili enjoy sana maisha Yale kabla ya mapinduzi.
Sasa basically hekima kubwa sana inahitajika kutanzua mfarakano huu, kuzika yale yaliyopita na wao wajione kwa dunia ya leo kila kundi ni muhimu kwa lenziwe kwa mustkabari wa maendeleo yao.
Hivyo ni jukumu la wadau wote kulisemea hili bila woga.
Kwa sababu hawaaminiani nashauri likae jopo la wanasheria itungwe sheria ambayo itakua check nd balance kwa hao watawala.
Iswepo mamlaka yenye guvu kuliko mwingine juu ya masuala nyeti ya kitaifa.
Kwa mfano muungano ni muhimu, istokee mtu kalala kaamka anauvunja kama alivyosema mstaafu kwamba wanmhofia yule jamaa atauvunja.
Ni mtizamo tu
 
You must be out of your mind. Hebu nenda kapimwe akili. Kama unataka kumwaga damu, unasubiri nini? Anza mwenyewe ukamwage damu yako halafu wafuate familia yako hapo tutakuelewa.
You must be out of your mind. Hebu nenda kapimwe akili. Kama unataka kumwaga damu, unasubiri nini? Anza mwenyewe ukamwage damu yako halafu wafuate familia yako hapo tutakuelewa.
 
Back
Top Bottom