Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,260
- 2,864
Sijajua mwaka 2020 Maalim Sharrif atakuwa na miaka mingap. Lakini ni waz kuwa umri wake utakuwa umeenda na waswas wangu ni zaid hata afya yake sijajua itakuaje. Mimi si Mungu wala Mtabiri lakini ni wazi atakuwa na athari kwa sababu kadhaa wa kadhaa.Nmeuliza so suala la Zanzibar linaendeleaje au limekuaje sasa? Ni wazi cuf wamepoteza na sasa wamejipoteza kwenye siasa za visiwani humo kabisa. Mwaka 2020 utakuwa ni mwaka rahisi sana kwa CCM upande wa Bara na Visiwani. Watashinda kwa urahisi sana maana watu weng wameshakata tamaa. Vyama vya upinzani vimeonekana kukosa nguvu kabisa. Vimenyong'onyea, vimeanza kukonda, sauti zao hazitoki tena au hazisikiki. Napata waswas na demokrasia ya vyama ving ambayo sasa imeshazikwa. Ni ngumu kwa miaka ya hapa karibun kupata vuguvugu na ari ya mwaka 2015 .itachukua miaka mingi sana. Je la Zanzibar ndo limeisha? Kama hivyo tu?