Kilewo: Wabunge wa Dar acheni kulalamikia kauli ya Magufuli, chukueni hatua


Tupoleni sana wakazi wadar es salaam kwa dharau hii kubwa tuliyoonyeshwa na waziri huyu, tusife moyo tunaweza kujiongoza wenyewe kupigania haki zetu za msingi bila hata kusubiri wa wakilishi wetu kutuongoza katika hili. twendeni mbele tusirudi nyuma na harakati hizo lazima zianze sasa, si kwa maana ya uovu, ni kulinda dhamani ya utu wetu na kuwafundisha wenyedharau kuwa na adabu kwani huenda wengine hawajawahi kufundshwa adabu na wazazi wao licha ya kuwa viongozi watawala. Asanteni sana na mungu atubariki by HENRY J KILEWO; KATIBU CHADEMA MKOA KINONDONI NA KANDA YA DAR ES SALAAM.KIL
Mkuu wewe Katibu wa CDM Mkoa wa Kinondoni Kanda ya Dar es Salaam, sasa hiyo KIL ya nini hapo au ulikuwa unataka kuandika Kilimanjaro?
 
Ongelea pia nauli za magari naona wengi mnafikiri ni 200/=ndo inalalamikiwa tu. hata hivyo si watu wote wanaishi just few meters from ferry. Tumieni akili kufikiri. Unapanda gari to ferry Tzs.350/= + kivuko 200/=+ ferry to kazini 300/- ni sawa na Tzs.800/=. Tuwe tunafanya japo analysis ndo tutoe mawazo yanayojenga.

Hivi umeambiwa kwamba wanaolipa shs 300 kwa ferry mwanza wote wanaishi jirani na vivuko ? au wengi wao kama ilivyo kigamboni ni watu wanaofika kivukoni baada ya kuwa wamelipa nauli nyingine kwenye mabasi, daladala etc. Nasisitiza kaa chini fanya Cost benefit analysis ya kazi yako na maisha yako huko kigamboni, ongeza kwa kufanya comparative advantage ya wewe kuendelea kuishi huko au kuhamia mahali pengine ambako utakuwa na net benefit, kwa ufupi free yourself from mawazo mgando kwamba ukishapata hiyo kazi yako Dar ni lazima ubaki nayo mpaka mwisho, nani ajuaye labda kupanda kwa gharama za kivuko kutakusaidia kutafuta namna mbadala ya maisha yaliyo bora penginepo na uwaachie wenye uwezo wa kulipa 200tshs waendelee kuishi kigamboni na kuchangia maboresho ya miundombinu ya huko?????????????!!!!!!!!!, Nachelea kusema tukipata watu wengi wenye kukubaliana na mawazo kama ya kwako, itapelekea nchi yetu kuendelea kuwa na huduma mbovu za kijamii, lakini mbaya zaidi inawatia moyo viongozi wenye tabia nyemelezi (opportunistic leaders) wenye vijitabia vya kuact kama CROWD PLEASERS, kama walivyofanya wabunge wa dar ambao wameamua kujifanya wanawahurumia sana wananchi bila kujua kwamba mwisho wa siku serikali itakosa mapata ambayo yangetumika kuboresho huduma za kivuko AMBAYO IN THE LONG RUN YAWEZA PELEKEA AJALI MBAYA KUTOKANA NA MATUMIZI YA MELI VIVUKO VISIVYOKUWA NA VIWANGO STAHILI KIUSALAMA, NA niseme iwapo watafanikiwa itakuwa furaha ya kitambo to myopic citizens of your calibre lakini longterm impact ya tabia hizo ndiyo inatupelekea kuendelea kuwa nchi tegemezi hata baada ya miaka hamsini ya uhuru.
 
Tunapoongelea utawala wa haki na sheria tunazungumzia ufuataji wa sheria na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa nchi yetu kila siku kwa maana tunajua nchi bila sheria na taratibu ni kama uwendawazimu! sasa kama serikali yenyewe kupitia wizara ya Ujenzi haifuati utaratibu katika kupandisha nauli yaani inajipandishia bila idhini ya SUMATRA, je pale wauza mafuta wanapokataa kushusha bei za mafuta wanapoamriwa na EWURA tumlaumu nani?

JK aliwalaumu wauza mafuta kwa kukataa kupunguza baei ya mafuta katika salamu zake za kufunga mwaka, je si muda muafaka pia kuanza kuwalaumu TEMESA pia kujipandishia bei bila ya kufuata taratibu yaani idhini ya EWURA? Au hizi sheria ziko kwa ajili ya wananchi wa kawaida tu? yaani wamiliki binafsi (hapa tunaongelea wa Kitanzania maana hata wale wa kigeni sheria huwapitia kando pitia suala la Songas na upandishaji wa bei ya gesi)!

Natoa ushauri tuangalie hii tabia ya kutofuata taratibu isije ikafika kiwango cha kutoweza kushikika/kuratibiwa maana tunaona hili ni janga la kitaifa maana mbali ya hii mada hata mavyuoni wakuu wa vyuo hawafuati taratibu na sheria, tunaona wanafuta serikali za wanafunzi kinyume na miongozo ya vyuo inavyosema!

Vilevile tunaona mikopo wanapewa wasiostahili, mikataba pia inasainishwa kwa watu wasio na uwezo bila kufuata taratibu za utangazaji wa tenda! Hata bungeni napo chombo cha kutunga sheria wanajipandishia mishahara na kujilipa bila ya utaratibu! Mawizarani pia huko mishahara inalipwa kama wanavyojitakia wao (wakubwa) na hata malipo ya kampuni zinazojenga barabara zetu yanafanywa kwa matakwa ya wakuu wanavyojiskia na kusababisha gharama kuongezeka mara dufu maana kuna matozo ya muda wa nyongeza kwa kutozingatia muda wa mkataba uliowekwa!

Tusisahau TANESCO nao naskia wako mbioni kuongeza umeme kwa 254.6% kwa kila unit ya umeme inayotumika! Sijawahi ona dunia hii gharama zikiongezeka zaidi ya 50% ya gharama halisi iliyopo ilhali mishahara ikibaki kama ilivyo na ongezeko la ukali wa maisha ukiwa juu ya 20%!

Kwa kifupi hii nchi inaelekea katika ile hali ya "failed state" na tunasubiri tu pale wananchi watakapochoka na hali halisi iliyopo na kuingia mitaani labda tuliyempa dhamana ya kuongoza nchi ataamka na kujua majukumu yake ni nini japokuwa atakuwa amechelewa! Jamani naombeni mtafakari hili...ninawasiwasi huu mwaka machafuko yatatokea maana hii serikali imeshindwa kuja na majawabu ya mambo muhimu kwa wananchi wake! Mungu ibariki Tanzania
 
Na Mwandishi Wetu

SAKATA la nauli mpya ya kivuko cha mv Magogoni limechukua sura mpya baada ya mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji kuwajia juu wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, akiwataka kuacha kumshambuliaji Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na badala yake wahangaike kutatua matatizo ya msingi ya wananchi katika majimbo yao.

Wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, juzi walizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, kitendo cha Magufuli kutangaza ongezeko nauli ya kivuko hicho kwa asilimia 100 bila kushirikisha wananchi, hakina tofauti na udikteta.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dewji alisema wabunge hawapaswi kupinga kila jambo kwa lengo la kujijenga kisiasa na kusisitiza kuwa Magufuli ana hoja za msingi, hivyo aungwe mkono kwa lengo la kuboresha usafiri wa majini katika eneo hilo na jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

"Jamani, ongezeko la sh 100 linaleta chokochoko za nini? Leo hii hata ombaomba ukimpa sh 100 anaweza kukurushia usoni. Wanalalamikia shilingi 100 wakati wao walijiongezea posho za laki mbili hawakuona ubaya wowote…nadhani wabunge wa Dar es Salaam walipaswa kumuunga mkono Magufuli ili kivuko kijiendeshe na kutoa huduma bora na za kudumu, badala ya kila kitu kutegemea kitoke serikali kuu.

"Hivi kila kitu kikitoka serikalini, fedha nyingine za maendeleo zitatoka wapi, kama si kuishia kuziba mapungufu kama yanayojitokeza kwenye vivuko vyetu vinapoharibika?" alihoji na kusema kama fedha zisipokusanywa, na vivuko vikapata hitilafu na kushindwa kutoa huduma, watakuwa wa kwanza kudai serikali imewasahau wana-Kigamboni.

Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, pesa zitakazokusanywa kutokana na nauli mpya zitachangia pia kulipa ongezeko la posho za wabunge, kwa kuwa ni fedha za wananchi na wabunge wanalipwa kutokana na fedha za walipakodi.

"Daladala zinapanda kila kukicha, hatusikii kelele, sasa angalia, Waziri Magufuli amesema kwa mara ya mwisho bei ya kuvuka kwenda na kutoka Kigamboni ilipandishwa miaka 14 iliyopita, hawaoni kuwa bei hiyo imepitwa sana na wakati?

"Na mbaya zaidi nasikia wanataka wakabidhiwe kazi ya kuendesha kivuko, mbona baadhi yao majimbaoni mwao tayari mambo yameanza kuwa ya shingo, hayaendi kabisa. Nadhani wangejikita katika kustawisha majimbo kwanza, wakishamaliza ndipo waombe kusaidia kazi za wengine, huu kwao si wakati sahihi wa kutoa msaada," alisema na kuhoji kwanini wasizungumze kumaliza kero nyingine za jijini, ikiwemo foleni.

Kauli ya Dewji, aliyekuwa anazungumza kwa hisia kauli, huku akisisitiza wabunge kuacha kudandia mambo kwa lengo la kupata umaarufu aliouita wenye kuwajenga zaidi kisiasa badala ya kuwanufaisha wananchi wa kawaida, imeibuka huku kukiwa na mjadala mkali tangu kupandishwa kwa nauli za kivuko cha Magogoni.

Jumapili iliyopita, Dk. Magufuli alitangaza kuwa, serikali imeamua kupandisha nauli hiyo kutoka kati ya sh 50 na Sh 100 hadi sh 200 kwa safari moja ya kivuko hicho, kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu. Alisema nauli iliyokuwapo ni ya tangu mwaka 1997, huku nauli ya vivuko vingine zaidi ya 30 nchini imekuwa ikipanda mara kwa mara.

Magufuli alisema kivuko cha Magogoni kimekuwa kikitoza nauli za chini ikilinganishwa na Chato, kinachotoza sh 300, Pangani Sh 200, Kisorya Sh 300, Lugolora Sh 500, Nyakarilo Sh 300, Chato-Bukombo Sh 2,000, Kirambo sh 500 na Utete Sh 300, huku wanafunzi wakisafiri bure.

Sambamba na upandishaji nauli kwa watu, pia nauli ya magari imepanda ambapo madogo yatatozwa Sh 800 na Sh 1,500, pick up sh 1,000 na Sh 2,000 na yale ya kuanzia tani tatu na nusu Sh 5,000 hadi Sh 7,500.


TUESDAY, JANUARY 03, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG
 
Hivi nauli za vivuko vingine kama Busisis zinapangwa na SUMATRA? Nauliza tu?
 
Hivi nauli za vivuko vingine kama Busisis zinapangwa na SUMATRA? Nauliza tu?
Kisheria SUMATRA huidhinisha matozo ya nauli! SUMATRA ni chombo cha kumlinda mwananchi wa kawaida kutoka uwezekano wa kunyonywa na waendeshaji wa vyombo vya usafirishaji!
 
Haya ni majibu ambayo viongozi wa serikali wamezoea kuyatoa kwa wananchi wakidhani watz hawana akili!!!!!
 
Hakukosea.....Cabinet lazima iliridhia.....na serikali haina hela ya kuendesha hivyo vivuko

nani anasimamia maamuzi ya kabineti pale ambapo yanalenga kumnyonga mlalahoi? huoni hapo kuna muingiliano wa majukumu? SUMATRA (chombo huru) ndio wanapaswa kuidhinisha ongezeko la nauli na si serikali! serikali (kama mmiliki wa chombo cha usafirishaji kupitia wizara ya Ujenzi) inapaswa kupeleka mapendekezo tu! tufuate sheria jamani kabla nchi haijashindwa kukalika! Inshangaza mijitu ni madokta (PHD holders) lakini hawafuati sheria na taratibu unaweza kuona ni matatizo na ukandamizaji gani wanavyuo wetu wanayakabili huko vyuoni chini ya uongozi wa wasomi wetu hawa!
 
Uamuzi wa waziri ni wa msingi, nauli lazima ipande sasa wakazi wa dar wakidhani mapato hayo ni kwa ajiri ya maendeleo yao2 watakuwa wamepotoka.. Na hao wabunge kama hawana la kuongea wakae kimya wasijitafutie sifa kwa wananchi.
 
Wakuu,

Nina mwanangu anasoma darasa la pili ukimpatia tsh 100 anakuuliza sasa hii itanunua nini ?.Ni jambo la kushangaza kama si kusikitisha wabunge wanalipwa tsh 70,000 kwa siku wanadai hazitoshi wamejiongezea kinyamela hadi tsh 200,000/= kwa siku wanadhani hilo ongezeko nani atafidia kama si serekali kutafuta vyanzo vingine.

Nauli mpya ya tsh 200 lazima ilipwe asiyetaka apige mbizi.
 
Serikali imekuwa inabeba mizigo mingine pasi na sababu yoyote, kama hili la Kigamboni.

Halafu, wananchi tunataka hata wajibu wetu wa msingi, ubebeshwe serikali. Enzi zimebadilika na wananchi tubadilike kifikra.
 
Sasa ugomvi utakuwa baina ya Wabunge wa Dar na Azim Dewji! Viongozi wetu hawapendi kuambiwa ukweli na hawataki kujihangaisha kutatua kero za msingi za Wananchi.
 
Haraka haraka unaweza kumuona Magufuli kama Kichaa ama mtu alielewa madaraka, lakini mimi namtizama kama mtu shujaa , anaetaka kusimamia yale ambayo ndio msimamo wa ccm na ndio vile ambavyo cabinet imekubaliana ndani ya vikao vyao vya siri .

Wanaccm wengi wamekua wakiunga mkono swala la kuongezewa posho kwa wabunge wao, ingawa kunakurushiana maneno juu ya hili, lakini ukweli unabaki swala hilo la posho linabaraka la wajumbe wengi wa NEC ya ccm , na huenda hata Bwana Mkubwa pale kitalu namba moja anahusika.

Hatujasikia kauli madhubuti za Viongozi waandamizi kukataa posho hii, japo Nape aliwahi kutoa msimamo wake binafsi juu ya swala hilo.

kwanini Magufuli kaongeza gharama za Nauli pale Kivukoni ?
Ameongeza kwakua anatafuta pesa za kufidia pesa watakazaongezewa wabunge wetu KAMA AMBAVYO MMESIKIA, ameamua kuongeza vyanzo vipya vya mapato ili kuweza kuifanya serikali kumudu gharama za kuendesha Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hili ukute linabaraka za wakubwa , na tusubiri kupanda kwa rate za ushuru maeneo kadhaa. kelele za wabunge wa ccm kule Kigamboni na Ilala ni ukosefu wa kumbukumbu kwamba ni wao wanaolimbikiza madeni kwa serikali na waache kutafuta sifa kwa matatizo ya wananchi.
Viva Magufuli, unatekeleza Ilani ya CCM ipasavyo, na Bado cha moto tutakiona.
 
Hivi zile Boat za Azm Dewji ziliishia wapi?...maana nakumbuka Mh POMBE alizikomalia kweli kweli
 
Tatizo ni kuweka siasa kwenye kila kitu, katika WABUNGE hawahawa kuna mmoja alimuwakia Prof Tibaijuka juu ya wakazi wa Jangwani eti hatakubali wapiga kura wake wanyanyaswe, hao hao wamechukuliwa na mafuriko juzi wengi wakapoteza Mali na maisha Yao. Mbunge yule Yukon wapi sasa? Jiji hili kutwa lina kero kibao; foleni, usalama, ujenzi holela, sewage system mbovu...kwa nini wabunge hawaungani kukabili shida hizo kwa kuiwekea pressure serikali kutatua matatizo hayo kwa mji huu mkuu wa nchi kibiashara? kwani like it or hate it, Dar is the heartbeat of this country! Dar deserves better than this...
 
Serikali imekuwa inabeba mizigo mingine pasi na sababu yoyote, kama hili la Kigamboni.

Halafu, wananchi tunataka hata wajibu wetu wa msingi, ubebeshwe serikali. Enzi zimebadilika na wananchi tubadilike kifikra.
tena apewe mtu binafsi akiendeshe kibiashara na huduma ziboreke
 
Back
Top Bottom