Kilewo: Wabunge wa Dar acheni kulalamikia kauli ya Magufuli, chukueni hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilewo: Wabunge wa Dar acheni kulalamikia kauli ya Magufuli, chukueni hatua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Jan 3, 2012.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema bwana HENRY KILEWO amesema anawashangaa sana wabunge wa Dar es salaam kumlalamikia magufuli ile hali wao wenyewe wamelala bila hata ya kutambua mamlaka walizopewa, Wameshindwa kulifanya jiji kuwa Active *kwa reaction pale linapotokea jambo la msingi kama hili la wananchi kupandishiwa gharama za usafiri bila kushirikishwa.Wabunge hawa wanapaswa kujilaumu wao wenyewe *kulikuwa hamna haja ya kutoa kauli ya kuwa magufuli awatake Radhi wakazi wa dar es salaam, kilichokuwa kinatakiwa kifanyike ni wao kuwaongoza wananchi wao mpaka kwenye ofisi za waziri huyo bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa na kupigania haki za wanyonge.


  Kiukweli jiji limepooza sana na limekosa mvuto wa kisiasa ukilinganisha na majiji mengine kama Arusha, Mwanza na Mbeya ambayo yapo juu kisiasa kutokana na wabunge wao kujitoa muhanga kusimamia ukweli kivitendo na siyokupiga kelele kwenye vyombo vya habari. Wabunge hawa wanapaswa kujitambua ya kuwa wanaongoza jiji lenye changamoto mbalimbali na katika kukabiliana na changamoto hizo wanapaswa kuwa wajasiri kusimamia ukweli. Dunia ya sasa imebadilika si kila kitu chakupeleka bungeni kufuata eti taratibu za sheria za kuombana radhi ama kutakana radhi, Kama mtu amekiuka maadili ya utu hamna haja ya kumfanyia utu maana magufuli alipotamka maneno hayo alikuwa na akili timamu ya nini kusubiri bunge? ile hali yupo ndani ya jiji mnaloliangoza? mimi ninaamini njia sahihi ya kupinga dhuluma hii ya wasiyonacho kuonewa na wenye mamlaka ya juu ni maandamano ya siyo na kikomo ili iwefundisho kwa wengine. Thamani ya utu wa mwanadamu haiwezi kupiganiwa kwa kelele zisizo kuwa na vitendo.


  Wabunge hawa waache uoga wawaongoze wananchi kulinda thamani ya utu wao, kwani alichofanya magufuli ni kebehi na dharau kubwa sana kwa wawakilishi wa wananchi wa dar es salaam.
  Tupoleni sana wakazi wadar es salaam kwa dharau hii kubwa tuliyoonyeshwa na waziri huyu, tusife moyo tunaweza kujiongoza wenyewe kupigania haki zetu za msingi bila hata kusubiri wa wakilishi wetu kutuongoza katika hili. twendeni mbele tusirudi nyuma na harakati hizo lazima zianze sasa, si kwa maana ya uovu, ni kulinda dhamani ya utu wetu na kuwafundisha wenyedharau kuwa na adabu kwani huenda wengine hawajawahi kufundshwa adabu na wazazi wao licha ya kuwa viongozi watawala. Asanteni sana na mungu atubariki by HENRY J KILEWO; KATIBU CHADEMA MKOA KINONDONI NA KANDA YA DAR ES SALAAM.KIL
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  kama wewe ni kiongozi wa chama ndani ya dar, ulishindwa nini na wewe kuwaongoza wananchi kuzidai haki zao kama hawo wabunge wameshindwa?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  wapige mbizi
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakuunga mkono na jambo hili kwa Tanzania imekuwa ni fasion tu,watu wanawahi kwenye media halafu jambo linaishia hapo lakini ki ukweli kinachotakiwa katika dunia ya sasa inayoenda kwa kasi ya ajabu ni kufanya vitendo,hakuna muda wa kupiga porojo za kwenye media,we need action,to me i trust that action speaks louder than words.
  Na fo sure Jiji la DAR linahitaji wawakilishi wa wananchi wanaongea kwa vitendo na ndio maana limepooza sana utadhani ni halmashauri ya mji wa Nkasi.
  Najiuliza hata dada yetu Mdee nae amepatwa na nini she is too quite,tulitegemea akishirikiana na Mnyika japo wangelikuwa wanali-beep jiji hili.sasa hapa nasi wananchi tufungue akili tuachane na wawakilishi wa kwenye media tuchague watekelezaji,sio wananchi wenu waliowachagua wanatukanwa matusi na kashfa juu wabunge wanaishia kenye media then inakuwa end of story.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mhurumieni huyu waziri kwani vituko vyake ni kama vya Augustine Mrema
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mimi niseme tu kwamba wa kulaumu si tu wabunge bali hata viongozi wa kisiasa.Dar ni makao makuu ya vyama vyote vya upinzani,kwanini hawachukui hatua? Tukija hata kwenye chama pekee tegemeo cha chadema mbona harakati zao wanafanyia tu mikoani? Mbona vyama vikubwa duniani harakati zake ziko miji mikuu? Chadema hawajawahi hata kuitisha mkutano wa hadhara hapa Dar tokea uchaguzi mkuu.Sasa badala ya kufanya haya mtegemee wabunge wa CCM waongoze harakati Dar? Think twice!
   
 7. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  eeh, kauli yako emeendana na yangu hapo juu, maana aliyesema haya na yeye ni kiongozi wa chadema hapa jijini, sijaona sababu za msingi za kuwashutumu wabunge ile hali hata hawo viongozi wa chama hawaamshi wanachama wao, kwa hili Kileo sikuungi mkono.
   
 8. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ila jamani, mbona shilingi mia mbili ni reasonable? Kumbukeni, dai la msingi la wananchi waliokuwa wakizomea lilikuwa ni kulalamikia kupandishwa nauli, hilo la kukejeliwa limekuja baadaye! Bila kujali hela zinafujwa au hazifujwi, mia mbili kwa kivuko ni hela ya kawaida tu. Wengine wamedai lina impact kwenye bei za bidhaa, lakini hata nauli ya sh. 300/= kwenye daladala kituo hadi kituo (minimum) nayo ina impact kwenye bei ya bidhaa, lakini haikuwahi kulalamikiwa, na hili ni jambo la kushangaza. Nionacho hapa mimi ni kwamba Magufuli ameponzwa na kitendo cha kutangaza nauli mpya directly mbele ya wahanga, na sijui kilichompeleka kule kwenye site ni nini. Nauli ya daladala huwa haitangazwi directly face to face mbele ya wahanga, bali utasikia tu kwenye runinga au redio kwamba SUMATRA wametoa nauli mpya, na hakuna mtanzania aliyewahi kuthubutu kukataa nauli mpya! Magufuli apunguze misisfa, ila nauli ya sh. 200/ si mbaya ukilinganisha na kuzungukia Kongowe (au kupiga mbizi!)
   
 9. K

  Konya JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nafikiri kuna tatizo la msimamo wa pamoja kama umoja wa mp's wa Dar kutokana na tofauti zao za kiitakadi so suala la kusema tuandamane mpaka ofisi y waziri mkuu sizani kama linawezekana kirahisi
   
 10. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwacheni magufuli awaambie ukweli kama huwezi kulipa shs mia mbili kwenye kivuko hama jiji , kuna mashamba mengi tanganyika ukalime. Mbona wenzenu kwenye vivuko vya mwanza wanalipa mia tatu muda mrefu tuu!!!! Na kama huna kipato na hutaki kutoka jijini basi jifunze kupiga mbizi kama alivyo waambia mpiganaji magufuli, uchumi wa nchi yetu unadidimia kutokana na watu msioweza kuzingatia kwamba serikali haiwezi kuboresha huduma zake bila kutoza kodi na tozo nyingine za kutosha ili kulipia gharama zinazoendana na improved standard of living that we so much desire, mnataka kigamboni lijengwe daraja hizo hela zitapatikana wapi!!??? Tabia hizo za kupenda dezo zitawapeleka pabaya ukizingatia matamshi ya hivi karibuni ya cameron na baadaye kusisitizwa na je duong obama. Na kwa comrade magufuli nina ushauri mmoja tu..............stick to your gun, usiwaombe radhi hao wacheza kiduku, bora uwarudishie uwaziri wao waendelee kucheza mdundiko na kutegemea kuishi kidezo dezo history will prove you right. Tunahitaji vimagufuli kama vitatu kwenye cabinet ili tuweze kuikwamua nchi yetu kutokana na huu ulegevulegevu. Bravo magufuli press on!!!!!!!!!!!!!
   
 11. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Umenena mkuu
   
 12. d

  dotto JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ongelea pia nauli za magari naona wengi mnafikiri ni 200/=ndo inalalamikiwa tu. hata hivyo si watu wote wanaishi just few meters from ferry. Tumieni akili kufikiri. Unapanda gari to ferry Tzs.350/= + kivuko 200/=+ ferry to kazini 300/- ni sawa na Tzs.800/=. Tuwe tunafanya japo analysis ndo tutoe mawazo yanayojenga.
   
 13. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  *ubarikiwe sanaaaaaaa kwa kuona mbali
   
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  watanzania tuache kuingiza siasa kwenye realities.gharama zimepanda na kivuko kinahitaji kujiendesha.magufuli kasema ukweli bana.hao wabunje wa dar wanatetea nini mbona wao kashfa kibao UDA,DDC,MACHINGA COMPLEX? Wasiwadanganye wapiga kura wa kigamboni kama walivyonwahadaa wale wa bonde la msimbazi.
  Mia 2 ituhamishe fikra tuanze kujadili siasa? Mbona wakazi hao wakivuka pantoni yenye engine kadhaa na generator na milango ya hydraulic wanapanda kidaladala cha engine moja na wanalipa 300? Waulize watu wa kimara mbezi,bunju,gongolamboto na mbagala wanalipa nauli bei gani.Tuache unafki.pantoni ipo asiyelipa 200 atulie nyumbani
   
 15. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,562
  Trophy Points: 280
  wapige mbizi tu....
   
 16. Exaud Mamuya

  Exaud Mamuya Verified User

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unalolisema kamanda Kilewo ni la msingi sana lakini katika umoja huu wa wabunge hawa walioungana yaani wa upinzani na wa chama kilichounda serikali unafikiri ni rahisi hivyo kwa wabunge hawa wa ccm kukubali kuandamana na kuikosoa serikali kwa kumpinga waziri mwenye dhamana! Hakika ni vigumu na ndio maana wanaweza hata kuwapumbaza wabunge makini wa upinzani kwa kutatua matatizo ya wananchi kwa kupitia vyombo vya habari pasipo kuchukua action. Nakupongeza kamanda Kilewo kwa kuliona hili.
   
 17. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkubwa umechimbua kaburi lenye rupia good memory
   
 18. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  Kilewo?
   
 19. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  mbona umeshangaa?
   
 20. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Acheni siasa zisizo na tija, ongezeko la nauli ni lazima kwa kipindi hiki
  Wamemzomea Waziri, nae ni binadam ana nyongo! He is not perfect.
  Watu wa Dar mmezubaa sana, hamtaki CHANGES, bakini hivyo na siku zote mtakuwa mnapiga kelele bila kufanya actions kama Arusha, Mbeya na Mwanza.
   
Loading...