Haraka haraka unaweza kumuona Magufuli kama Kichaa ama mtu alielewa madaraka, lakini mimi namtizama kama mtu shujaa , anaetaka kusimamia yale ambayo ndio msimamo wa ccm na ndio vile ambavyo cabinet imekubaliana ndani ya vikao vyao vya siri .
Wanaccm wengi wamekua wakiunga mkono swala la kuongezewa posho kwa wabunge wao, ingawa kunakurushiana maneno juu ya hili, lakini ukweli unabaki swala hilo la posho linabaraka la wajumbe wengi wa NEC ya ccm , na huenda hata Bwana Mkubwa pale kitalu namba moja anahusika.
Hatujasikia kauli madhubuti za Viongozi waandamizi kukataa posho hii, japo Nape aliwahi kutoa msimamo wake binafsi juu ya swala hilo.
kwanini Magufuli kaongeza gharama za Nauli pale Kivukoni ?
Ameongeza kwakua anatafuta pesa za kufidia pesa watakazaongezewa wabunge wetu KAMA AMBAVYO MMESIKIA, ameamua kuongeza vyanzo vipya vya mapato ili kuweza kuifanya serikali kumudu gharama za kuendesha Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hili ukute linabaraka za wakubwa , na tusubiri kupanda kwa rate za ushuru maeneo kadhaa. kelele za wabunge wa ccm kule Kigamboni na Ilala ni ukosefu wa kumbukumbu kwamba ni wao wanaolimbikiza madeni kwa serikali na waache kutafuta sifa kwa matatizo ya wananchi.
Viva Magufuli, unatekeleza Ilani ya CCM ipasavyo, na Bado cha moto tutakiona.
Zilipita Kenya Kama sikosei....Hivi zile Boat za Azm Dewji ziliishia wapi?...maana nakumbuka Mh POMBE alizikomalia kweli kweli
wapige mbizi
Ndio Lugha za wanaccm wote hizo baada ya kushinda chaguzi , daima kejeli na matusi ndio lugha tulizozizoea, huwezi kutenga magufuli na CCM , hiyo ndio rangi yao halisiMkuu, vipi kuwa lugha ya jeuri kwa watu? Yeye kama kiongozi alitakiwa kuelezea sababu ya ongezeko la 100%. Ukiwa kiongozi vitu hivi ni muhimu sana. Vile vile, kuhusu ubadhirifu wa makusanyo mbona hajaongelea?
tatizo jingine ni hao wanaoongozwa hawajitambui wanapelekwapelekwa tu na hao wachumia tumboni...wapiga kura wa temeke acheni hizo! amkeni mjiletee development...mbona mdundiko na sare za harusi kila siku mnashona MIA iwe tabu!!Tatizo ni kuweka siasa kwenye kila kitu, katika WABUNGE hawahawa kuna mmoja alimuwakia Prof Tibaijuka juu ya wakazi wa Jangwani eti hatakubali wapiga kura wake wanyanyaswe, hao hao wamechukuliwa na mafuriko juzi wengi wakapoteza Mali na maisha Yao. Mbunge yule Yukon wapi sasa? Jiji hili kutwa lina kero kibao; foleni, usalama, ujenzi holela, sewage system mbovu...kwa nini wabunge hawaungani kukabili shida hizo kwa kuiwekea pressure serikali kutatua matatizo hayo kwa mji huu mkuu wa nchi kibiashara? kwani like it or hate it, Dar is the heartbeat of this country! Dar deserves better than this...
Hivi zilikuwa za Azim Dewji au yule Dewji mwingine wa Hadees Restaurant(Food World)?Hivi zile Boat za Azm Dewji ziliishia wapi?...maana nakumbuka Mh POMBE alizikomalia kweli kweli
Na Mwandishi Wetu
SAKATA la nauli mpya ya kivuko cha mv Magogoni limechukua sura mpya baada ya mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji kuwajia juu wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, akiwataka kuacha kumshambuliaji Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na badala yake wahangaike kutatua matatizo ya msingi ya wananchi katika majimbo yao.
Wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, juzi walizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, kitendo cha Magufuli kutangaza ongezeko nauli ya kivuko hicho kwa asilimia 100 bila kushirikisha wananchi, hakina tofauti na udikteta.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dewji alisema wabunge hawapaswi kupinga kila jambo kwa lengo la kujijenga kisiasa na kusisitiza kuwa Magufuli ana hoja za msingi, hivyo aungwe mkono kwa lengo la kuboresha usafiri wa majini katika eneo hilo na jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.
"Jamani, ongezeko la sh 100 linaleta chokochoko za nini? Leo hii hata ombaomba ukimpa sh 100 anaweza kukurushia usoni. Wanalalamikia shilingi 100 wakati wao walijiongezea posho za laki mbili hawakuona ubaya wowote…nadhani wabunge wa Dar es Salaam walipaswa kumuunga mkono Magufuli ili kivuko kijiendeshe na kutoa huduma bora na za kudumu, badala ya kila kitu kutegemea kitoke serikali kuu.
"Hivi kila kitu kikitoka serikalini, fedha nyingine za maendeleo zitatoka wapi, kama si kuishia kuziba mapungufu kama yanayojitokeza kwenye vivuko vyetu vinapoharibika?" alihoji na kusema kama fedha zisipokusanywa, na vivuko vikapata hitilafu na kushindwa kutoa huduma, watakuwa wa kwanza kudai serikali imewasahau wana-Kigamboni.
Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, pesa zitakazokusanywa kutokana na nauli mpya zitachangia pia kulipa ongezeko la posho za wabunge, kwa kuwa ni fedha za wananchi na wabunge wanalipwa kutokana na fedha za walipakodi.
"Daladala zinapanda kila kukicha, hatusikii kelele, sasa angalia, Waziri Magufuli amesema kwa mara ya mwisho bei ya kuvuka kwenda na kutoka Kigamboni ilipandishwa miaka 14 iliyopita, hawaoni kuwa bei hiyo imepitwa sana na wakati?
"Na mbaya zaidi nasikia wanataka wakabidhiwe kazi ya kuendesha kivuko, mbona baadhi yao majimbaoni mwao tayari mambo yameanza kuwa ya shingo, hayaendi kabisa. Nadhani wangejikita katika kustawisha majimbo kwanza, wakishamaliza ndipo waombe kusaidia kazi za wengine, huu kwao si wakati sahihi wa kutoa msaada," alisema na kuhoji kwanini wasizungumze kumaliza kero nyingine za jijini, ikiwemo foleni.
Kauli ya Dewji, aliyekuwa anazungumza kwa hisia kauli, huku akisisitiza wabunge kuacha kudandia mambo kwa lengo la kupata umaarufu aliouita wenye kuwajenga zaidi kisiasa badala ya kuwanufaisha wananchi wa kawaida, imeibuka huku kukiwa na mjadala mkali tangu kupandishwa kwa nauli za kivuko cha Magogoni.
Jumapili iliyopita, Dk. Magufuli alitangaza kuwa, serikali imeamua kupandisha nauli hiyo kutoka kati ya sh 50 na Sh 100 hadi sh 200 kwa safari moja ya kivuko hicho, kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu. Alisema nauli iliyokuwapo ni ya tangu mwaka 1997, huku nauli ya vivuko vingine zaidi ya 30 nchini imekuwa ikipanda mara kwa mara.
Magufuli alisema kivuko cha Magogoni kimekuwa kikitoza nauli za chini ikilinganishwa na Chato, kinachotoza sh 300, Pangani Sh 200, Kisorya Sh 300, Lugolora Sh 500, Nyakarilo Sh 300, Chato-Bukombo Sh 2,000, Kirambo sh 500 na Utete Sh 300, huku wanafunzi wakisafiri bure.
Sambamba na upandishaji nauli kwa watu, pia nauli ya magari imepanda ambapo madogo yatatozwa Sh 800 na Sh 1,500, pick up sh 1,000 na Sh 2,000 na yale ya kuanzia tani tatu na nusu Sh 5,000 hadi Sh 7,500.
TUESDAY, JANUARY 03, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG
Tatizo ni kuweka siasa kwenye kila kitu, katika WABUNGE hawahawa kuna mmoja alimuwakia Prof Tibaijuka juu ya wakazi wa Jangwani eti hatakubali wapiga kura wake wanyanyaswe, hao hao wamechukuliwa na mafuriko juzi wengi wakapoteza Mali na maisha Yao. Mbunge yule Yukon wapi sasa? Jiji hili kutwa lina kero kibao; foleni, usalama, ujenzi holela, sewage system mbovu...kwa nini wabunge hawaungani kukabili shida hizo kwa kuiwekea pressure serikali kutatua matatizo hayo kwa mji huu mkuu wa nchi kibiashara? kwani like it or hate it, Dar is the heartbeat of this country! Dar deserves better than this...
Hivi zile Boat za Azm Dewji ziliishia wapi?...maana nakumbuka Mh POMBE alizikomalia kweli kweli