Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,330
- 33,954
Kwa watu tunaoamini dhana ya uwepo wa Mungu tunaamini kwamba Ulimwengu umeumbwa na Mungu. Tunaposema Ulimwengu tunamaanisha kwamba Dunia na vyote vilivyomo na vinavyoizunguka dunia.
Maelezo mengi yanaonesha kwamba Dunia imeumbwa kimiujiza na Mungu na inaendeshwa pia katika misingi hiyo hiyo. Lakini wakati fulani huwa nawaza kama kweli kila tukionacho katika dunia na Ulimwengu kimeumbwa na Mungu.
Adam na Hawa waliumbwa na Mungu, lakini hakuna maelezo ya kutosheleza kama watoto wa Adam, yaani Kaini na Habili wake zao walitokana na uumbaji wa Mungu.
Lakini pia wakati mwingine nikiangalia vitu vya ulimwengu huu huwa najiulza kama kweli Nyoka ama na wanyama na wadudu wenyewe sumu kama nyoka waliumbwa na Mungu, ili kiwe nini?
Kwenye baadhi ya vitabu vya dini inaelezwa kwamba "wana Mungu walioana na wana wa ulimwengu" na kuzaliwa viumbe waliokuwa wanaitwa "Wanefili"
Kama kumbe wana wa Mungu walikuta kuna wana wa Ulimwengu, jee hao wana wa Ulimwengu walikuwa wameumbwa na nani? Na jee ulimwengu wakati hao wana Mungu wanakuja ulikuwa kama huu tulio nao sasa ama ulikuwa tofautii?
Hivi na miiba nayo imeumbwa na Mungu na kama ni hivyo ili kiwe nini. Maelfu ya miaka mwanadamu ameishi na Magonjwa tofautitofauti, jee nayo ni uumbaji wa Mungu.
MUNGU aliumba kila kitu kilichomo Ulimwenguni?