Kila tunachokiona Ulimwenguni kimeumbwa na Mungu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,035
33,515
Kwa watu tunaoamini dhana ya uwepo wa Mungu tunaamini kwamba Ulimwengu umeumbwa na Mungu. Tunaposema Ulimwengu tunamaanisha kwamba Dunia na vyote vilivyomo na vinavyoizunguka dunia.

Maelezo mengi yanaonesha kwamba Dunia imeumbwa kimiujiza na Mungu na inaendeshwa pia katika misingi hiyo hiyo. Lakini wakati fulani huwa nawaza kama kweli kila tukionacho katika dunia na Ulimwengu kimeumbwa na Mungu.

Adam na Hawa waliumbwa na Mungu, lakini hakuna maelezo ya kutosheleza kama watoto wa Adam, yaani Kaini na Habili wake zao walitokana na uumbaji wa Mungu.

Lakini pia wakati mwingine nikiangalia vitu vya ulimwengu huu huwa najiulza kama kweli Nyoka ama na wanyama na wadudu wenyewe sumu kama nyoka waliumbwa na Mungu, ili kiwe nini?

Kwenye baadhi ya vitabu vya dini inaelezwa kwamba "wana Mungu walioana na wana wa ulimwengu" na kuzaliwa viumbe waliokuwa wanaitwa "Wanefili"

Kama kumbe wana wa Mungu walikuta kuna wana wa Ulimwengu, jee hao wana wa Ulimwengu walikuwa wameumbwa na nani? Na jee ulimwengu wakati hao wana Mungu wanakuja ulikuwa kama huu tulio nao sasa ama ulikuwa tofautii?

Hivi na miiba nayo imeumbwa na Mungu na kama ni hivyo ili kiwe nini. Maelfu ya miaka mwanadamu ameishi na Magonjwa tofautitofauti, jee nayo ni uumbaji wa Mungu.

MUNGU aliumba kila kitu kilichomo Ulimwenguni?
 
Tunaambiwa kuwa Mungu alipomaliza kuumba aliona vyote alivyoviumba ni vyema!! Ilikuwaje akaumba kiumbe kinachohitaji sumu ili kujilinda?
Hakika vyote alivyoviumba ni vyema
Malaika aliyeasi ndiye alileta ubaya duniani
Alimwambia nakutupa duniani na walio wako watakufuata
 
Kwa watu tunaoamini dhana ya uwepo wa Mungu tunaamini kwamba Ulimwengu umeumbwa na Mungu. Tunaposema Ulimwengu tunamaanisha kwamba Dunia na vyote vilivyomo na vinavyoizunguka dunia.

Maelezo mengi yanaonesha kwamba Dunia imeumbwa kimiujiza na Mungu na inaendeshwa pia katika misingi hiyo hiyo. Lakini wakati fulani huwa nawaza kama kweli kila tukionacho katika dunia na Ulimwengu kimeumbwa na Mungu.

Adam na Hawa waliumbwa na Mungu, lakini hakuna maelezo ya kutosheleza kama watoto wa Adam, yaani Kaini na Habili wake zao walitokana na uumbaji wa Mungu.

Lakini pia wakati mwingine nikiangalia vitu vya ulimwengu huu huwa najiulza kama kweli Nyoka ama na wanyama na wadudu wenyewe sumu kama nyoka waliumbwa na Mungu, ili kiwe nini?

Kwenye baadhi ya vitabu vya dini inaelezwa kwamba "wana Mungu walioana na wana wa ulimwengu" na kuzaliwa viumbe waliokuwa wanaitwa "Wanefili"

Kama kumbe wana wa Mungu walikuta kuna wana wa Ulimwengu, jee hao wana wa Ulimwengu walikuwa wameumbwa na nani? Na jee ulimwengu wakati hao wana Mungu wanakuja ulikuwa kama huu tulio nao sasa ama ulikuwa tofautii?

Hivi na miiba nayo imeumbwa na Mungu na kama ni hivyo ili kiwe nini. Maelfu ya miaka mwanadamu ameishi na Magonjwa tofautitofauti, jee nayo ni uumbaji wa Mungu.

MUNGU aliumba kila kitu kilichomo Ulimwenguni?
Ndiyo! Mungu aliumba kila kitu kilchoko ulimwenguni.
Tena k/ kitu kina lengo lake maalumua kuumbwa kwake
Yawezekana wewe ukaona leo Nyoka hana tija kuwepo kwake,,lakini nikuulize ,Ivi wewe Kuwepo kwako kunatija gani kwa viumbe wengine akina Nyoka ,Wanyama mwitu na Miti ya msituni zaidi ya uharibifu wako?
Je wajua lengo wewe Kuwepo kwako?

rejea zama za ujima, Almasi na Tanzanite zilikuwa na kazi gani zaidi ya Kete za kuchezea bao?

Kwenye gesi ya Sulfur palionekanapana mzimu,na kwa hiyo watu wali pakimbia,
lakini leo ni eneo la kuchimba gesi adhimu ya kutengenezea mbolea na dawa.
Elimu zetu zikiongezeka hakuna kisicho na maana duniani.
Mungu ana hekima katika kila kitu,ila elimu zetu juu ya vitu bado ni ndogo mno.
Utaja ona pengine sumu ya nyoka ndo dawa ya corona,utatamani na wewe ufuge nyoka nyumbani ili uwe na dawa kwa njia rahisi
 
Na shetani alieumbwa na Mungu alionekana kuwa uumbaji wake ulikuwa mwema, SASA HAKO KA CHEMBE CHEMBE KA UASI KALITOKA WAPI?
 
Kila unachokiona duniani kipo ,si kwa bahati mbaya,bali kiko katika mpango mzima wa Mungu tena wenye hekima.

Mungu hakuiweka dunia kuwa pahali pa kula batta tuu ila ni sehemu ya ku struggle na Maisha,Imani,na mazingira yaliyotuzunguka.
Kisha Mungu akatupa Akili na Elimu ya Vitabu vya Kiroho ili kutupa msaada wa kupambana na Vitatu hivyo.
Huyo sheta ni sehemu ya Mpango mzima wa Mungu kwa ajili ya kuwapatia Uimara wa kumuabudu Mungu hawa wapambanaji.Kwa vile tumepewa uhuru wa kutenda mema na mabaya, na tumepewa utambuzi wa kiakili,na Matamanio ya kupenda mambo mazuri tuu na kuchukia mabaya hapo ndipo lipo pewa shetani nafasi ya kuwavuta atakaowaweza kwa Ushawishi wake.Vitabu vikatuwekea wazi hila za kishetani, na lengo la Mungu kwetu wanadamu.

Na ndo maana watakao Mkubali na kumtii Mungu atwapa zawadi ya Msamaha wa matelezo yake.
Na wale watakaoleta kiburi nakuacha KumtiiMungu na Kuto muamini ,hao watachezea kisago bila ya Huruma.

Dunia ya malaika ndiyo isiyokuwa na Uasi wala Matakwa ,wao hufanya mambo kama Robot
 
44. Zinamtakasa (Mwenyezimungu) mbingu zote saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu namna ya kutakasa kwake(Kumsifu ). Hakika Yeye(Allah) ni Mpole na Mwenye maghfira kwa viumbe(wanadamu).
 
Kwa watu tunaoamini dhana ya uwepo wa Mungu tunaamini kwamba Ulimwengu umeumbwa na Mungu. Tunaposema Ulimwengu tunamaanisha kwamba Dunia na vyote vilivyomo na vinavyoizunguka dunia.

Maelezo mengi yanaonesha kwamba Dunia imeumbwa kimiujiza na Mungu na inaendeshwa pia katika misingi hiyo hiyo. Lakini wakati fulani huwa nawaza kama kweli kila tukionacho katika dunia na Ulimwengu kimeumbwa na Mungu.

Adam na Hawa waliumbwa na Mungu, lakini hakuna maelezo ya kutosheleza kama watoto wa Adam, yaani Kaini na Habili wake zao walitokana na uumbaji wa Mungu.

Lakini pia wakati mwingine nikiangalia vitu vya ulimwengu huu huwa najiulza kama kweli Nyoka ama na wanyama na wadudu wenyewe sumu kama nyoka waliumbwa na Mungu, ili kiwe nini?

Kwenye baadhi ya vitabu vya dini inaelezwa kwamba "wana Mungu walioana na wana wa ulimwengu" na kuzaliwa viumbe waliokuwa wanaitwa "Wanefili"

Kama kumbe wana wa Mungu walikuta kuna wana wa Ulimwengu, jee hao wana wa Ulimwengu walikuwa wameumbwa na nani? Na jee ulimwengu wakati hao wana Mungu wanakuja ulikuwa kama huu tulio nao sasa ama ulikuwa tofautii?

Hivi na miiba nayo imeumbwa na Mungu na kama ni hivyo ili kiwe nini. Maelfu ya miaka mwanadamu ameishi na Magonjwa tofautitofauti, jee nayo ni uumbaji wa Mungu.

MUNGU aliumba kila kitu kilichomo Ulimwenguni?
Yapo ya kutisha zaidi na hayaonekani kwa macho, lakini yote ni kazi ya Mungu wetu.
 
Muumbaji aliumba muumbwaji na muumbwaji aliongeza viumbwaji.
Hili linafikirisha kidogo.
Mungu aliweka mifumo ya kila kitu alichokiumba namna kitakavyo 'survive' na 'reproduce'
Kwa maana Hiyo Bado Mungu anaendelea kuumba kwa kupitia hiyo mifumo aliyoiweka.

1. Litakase jina la Mola wako Mlezi(mchungaji na msimamizi wa kila kitu na matendo yao) aliye juu kabisa,

2. Aliye umba (kila kitu), na akaweka sawa (mifumo yake),

3. Na ambaye amekadiria na akaongoa(Kwa kukiongoza kila kiumbe na nfume wake wa kuishi,kula,kuongezeka,na mazingira yanayofaa kwa uwepo wake hicho kiumbe)

Kwa hiyo ni juu yetu sisi wanadamu ku 'study' viumbe vya Mungu kwa kujiongezea maarifa (Elimu) kwa elimu hiyo tutaweza kuboresha maisha yetu ya kila siku.
Ndo maana Waliolifahamu hili (wazungu) kila siku wako pembe zote za dunia kufanya research ya kila kiumbe na kuandika taarifa zake na kuleta ugunduzi mbali mbali wa kimaisha.
WAAFRIKA YATUFAA TUJIONGEZE,DUNIA HUENDELEA KWA 'RESEARCH'
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom