Kila story itamsifia muwindaji hadi pale simba atakapojifunza kuandika

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
968
1,695
Kuna nadharia zaidi ya milioni moja kutoka mataifa na meaneo mbali mbali yenye kusimulia kuhusu uwepo nguvu isiyo ya kawaida , nguvu yenye uwezo wa kuumba na kutoa uhai.(supernatural power ) kutoka kwenye ngano hizo nyingi ndipo zinapo zaliwa dini nyingi ,

Ukiachana na ngano zenye kusimulia vizazi vya Abraham zipo ngano kama , Budha , Zeus Zoran na Anunnaki , zote zina lengo moja.

Ngano zote hizo zina simulia na kueleza namna miungu hao walitokea na namna gani walifanya uumbaji ,
ngano zina simulia namna gani miungu hao wananguvu , namna walishinda vita zao kibabe na jinsi walivyo spesho.

Kama utasoma Ngano za wagiriki zenye kuwasimulia ,zeus Posaidon na Edes au Hercures walivyo hautaacha kuamini kuwa ni wana nguvu zisizo pimika.

Ukiwakuta wana wa Abraham wakiwa wana simulia vizazi vyao na kumuelezea baba yao muumba wa Ardhi na mbingu huwezi kuacha kuelewa kuwa hakuna kama yeye.

Hakuna Ngano hata moja inayo waeleza magwiji hao kama wanyonge walio onewa wasio na maana ,
Na ngano hizo zote hazifanani wala kuingilina kwa namna yoyote ile.

Kwa akili ya kawaida tu kama jambo moja lina simuliwa na watu watato tofauti kwa namna tofauti kabisa basi kuna wanne waongo au wote waongo.

Je, kama wote waongo hizi ngano walizitoa wapi?.

Jibu ni kuwa wapo watu walio kaa wakabuni hizi ngano na wakaja kujaza akilini kwa wasio jua kuandika ngano zao.

Kama wagiriki wana ngano zao , wazungu wana zakwao, waarabu wana zakwao , wachina wanazo pia kivipi wa Africa hawana zakwao?

Wa Afrika hawana ngano kwasababu hawajui kuandika au hawana wakuwaandika?

Kwenye ujenzi wa kizazi imara kinacho fuata kuna mambo matatu ya kuzingatia Malezi, ngano na Elimu.

Mpaka tutakapo jifunza kuandika tutaendelea kuandikwa kama tulio shindwa na wachovu viumbe dhaifu tusio na mbele waka nyuma.

Historia huandikwa na washindi.
 
Utajuaje mythologies za Afrika wakati hujatenga mda wako kuzisoma?

Afrika haijaanza baada ya ukoloni, Afrika ina historia ndefu na ya kuvutia
Licha ya masimulizi mengi ya mababu zetu kupotea kwasababu ya mda au kutohifadhiwa kwenye maandishi au kuharibiwa kwa makusudi au bahati mbaya bado kuna mengi ya kujifunza

Na usisahau, hio inayoitwa misri ya kale haikua ya waarabu, wazungu wala wagiriki

Hao Mafirauni (waliofanywa maadui kwenye ngano za uongo za wayahudi) walikua ni Waafrika, kwa eneo na kwa damu.
 
Tupe moja inayo eleza kuhusu super natural na creation
 
Back
Top Bottom