Kila nikimkumbuka naumia roho!

Sangari

Senior Member
Oct 31, 2011
172
58
Ndugu wana JF kwanza kabisa poleni na majukumu. Shida yangu ni hii, mimi ni mwanaume, mwaka jana mwezi wa 12 nilikutana na mpenzi wangu humu jf, tukafanya mawasiliano tukafahamiana vizuri. Tukapanga siku ya kuonana, nikatoka Moshi kwenda Dar kuonana nae akanipokea vizuri sana. Alikuwa mzuri wa sura na kimtazamo alionekana kabisa kuwa tayari kwa maisha ya ndoa. Pia kwenye vigezo tulivyopeana kila mtu aliridhika na mwenzie. Kweli nilimpenda sana na yeye vivyo hivyo. Mwezi wa kwanza mwaka huu tulianza rasmi kuwa wachumba na tukapanga kwenda kutambulishana kwa wazazi. Siku moja katika ofisi niliyokuwa nafanyia kazi ilivamiwa na majambazi usiku, vikaibwa vitu vya ofisi ikiwemo check ya shilingi milioni 10, computer 2 na baadhi ya nyaraka za ofisi. Pia niliibiwa laptop yangu. Nakumbuka Siku hiyo jioni mimi nilikuwa wa mwisho kutoka ofisini kwani wenzangu walinitangulia. Hivyo kesi ikawa imeniangukia nikajikuta mimi na aliyekuwa mlinzi wa ofisi yetu tunapelekwa rumande. Tulikaa rumande kwa muda wa wiki mbili bila dhamana. Baadae nilitoka rumande kesi ikawa inaendelea, roho iliniuma sana kwa kuhusishwa na ujambazi. Wazazi wangu walichukia sana kwa kitendo hicho na waliona hakuna haja ya malumbano na mwenye ofisi wakaona waingilie kati na kuongea na mwenye ofisi na kumlipa gharama zote za vitu vilivyoibiwa isipokuwa nyaraka hazikupatikana. Kesi ikawa imeisha nikarudi nyumbani. Wakati haya yote yanatoke mpenzi wangu alikuwa hana taarifa kwani simu zangu zilizimwa na mdogo wangu niliekuwa naishi nae hadi nilipotoka rumande. Mpenzi wangu alinitafuta sana hadi akakata tamaa. Baada ya hayo yote nilimpigia mpenzi wangu kumweleza yaliyonitokea lakini hakuamini na aliniambia wazi kuwa namdanganya. Nilijaribu kumwelewesha akawa hanielewi. Baada ya kuona hivyo nilijikuta namuongelesha kwa hasira na ukali uliomfanya akakata mawasiliano. Hadi leo ninavyoandika simu yake haipatikani wala humu Jf simuoni tena. Nimejaribu kuPM lakini inaonekana alishabadisha ID yake. Ombi langu kama yuko humu jf namuomba anisamehe tuendelee na mahusiano yetu. Pia awe na imani tu kuwa ni kweli haya mambo yalinitokea kwani kuna kipindi nilimpa mdogo wangu cm akaongea nae lakini alidai kwa nini hakupewa taarifa wakati haya mambo yanatokea. Wana Jf nisaidieni nifanyeje ili nipate kuwasiliana na huyu mpenzi wangu niliempenda sana. Pia nilikiri kwa kumuomba samahani kwania nilijikuta niko mikononi mwa polisi ghafla. Asanteni!
 
hee,kumbe mapenzi jf yapo?nilikuwa sijui,maybe ipo siku na mimi nitapata wangu humu.hongereni na ujumbe ameshaupata,maybe ameshapata mwengine jf.si unajua tena mambo ya jf,kila mtu anatafuta mchumba.seriously,mimi siamini mapenzi ya humu,maybe i'm wrong,pole kijana kwa yaliyokukuta.na bi shost msamehe,mwenzio unamuumiza.mpaka anakutafuta live humu,ujue anakupenda
 
Pole kwa yote, labda it wasnt meant to be na kama mtu hataki kuwa muelewa, huwezi jua umeepushwa na nini, endelea kuvumilia kama moyo wako unakuambia hivo, kama ni wako ni wako tu.
 
Mpenzi wangu alinitafuta sana hadi akakata tamaa. Baada ya hayo yote nilimpigia mpenzi wangu kumweleza yaliyonitokea lakini hakuamini na aliniambia wazi kuwa namdanganya. Nilijaribu kumwelewesha akawa hanielewi. Baada ya kuona hivyo nilijikuta namuongelesha kwa hasira na ukali uliomfanya akakata mawasiliano. Hadi leo ninavyoandika simu yake haipatikani wala humu Jf simuoni tena. Nimejaribu kuPM lakini inaonekana alishabadisha ID yake.

Hapo kwa red pamenishangaza sana! kweli mapenzi ya dot.com ni so delicate jamani!!! yaani uvumilivu zero kabisa!
-Yaani wiki 2 tu tayari mtu kaishakata tamaa kiasi hicho
-Halafu sababu yenyewe ya kuchukua uamuzi kama huo ni ndooogo!

Pole mkuu, nakutakia kila la heri ktk jitihada zake za kumrudisha. Lakini ukiona vipi kubali tu matokeo aisee ili ufungue ukurasa mpya manake unaweza kuwa unahangaika hapa bure kumbe mwenzio tayari kaishaanzisha mahusiano na mtu mwingine, chezea dot.com!
 
Dah! Na hizi penssion hadi 55-60 baba kazi unayo! Kama unapajua kwao funga safari usiogope!
 
aisee, kumbe inawezekana ukabahatisha mchumba hapa JF eeh.... but wachumba wenyewe wamekaa kimachale ile mbaya, yaani no communications within two weeks unapigwa chini fasta.....au ndiyo mulitiple online fiancees, akiona mmoja hasomeki anahamia kwingine pronto
 
Ujumbe keshaupata kama yumo humu. Lkn ulishindwaje hata kumjulisha week zote mbili hata kama ulikuwa rumande???.
 
hee,kumbe mapenzi jf yapo?nilikuwa sijui,maybe ipo siku na mimi nitapata wangu humu.hongereni na ujumbe ameshaupata,maybe ameshapata mwengine jf.si unajua tena mambo ya jf,kila mtu anatafuta mchumba.seriously,mimi siamini mapenzi ya humu,maybe i'm wrong,pole kijana kwa yaliyokukuta.na bi shost msamehe,mwenzio unamuumiza.mpaka anakutafuta live humu,ujue anakupenda
me nimekuzimikia kisukari....naomba nafasi kwa mtima wako:A S-heart-2:
 
Last edited by a moderator:
mkuu pole sana sana.

Jamani kama huyu kaka anasema ukweli wee mdada wa jf hebu mrudie mwenzio lol! hivi unaijua thamani ya kupendwa? angalia usije acha mbachao kwa msala upitao. wala usikimbilie kulia ukakuta kushoto kumebomoka funguka kama unaona humtak tena mweleze achukue time yake lol!

hebu ni pm id.
 
Kumbe JF kiila kitu kinawezekana!!!!!! ila majeruhi wa mapenzi hatukawii kuwapata! Pole. Madame B umepotea sana siku hizi!
 
Last edited by a moderator:
Duh!! Tunakuombea tu huyo jamaa aelewe. Ushauri wangu jamaa afanye utafiti ajiridhishe na hiyo habari yenyewe. Mapenzi huuma kama ugonjwa. Pole sana
 
hii stori mwanzoni imenipa uzuni esp kwnye kusingiziwa lakini uyo demu ndo kaja kunibore mazima amekutafuta sana kivipi asiweze kupata taarifa japo kwa rafiki wa karibu???, assume yeye ndo kapoteza bahati ya kuwa na wewe, wanawake wako wengi sana wenye kila sifa it just the matter of time.period
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom