Kila mwenye kuvuta pumzi ya bure, na apite hapa kusifu na kushukuru

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,175
22,694
Salaam, Shalom!

Hakuna cha bure yupo MMILIKI, mtoaji, Muumba wa vyote.

Sisi WANADAMU kwa ujumla wetu, masikini kwa tajiri, mgonjwa Kwa mzima, mrefu Kwa mfupi, mweupe Kwa mweusi nk nk tunavuta PUMZI ya uhai Bure kabisa.

Wema Kwa waovu, tunapata Bure PUMZI ya uhai.

Wenye dini kwa wapagani, tunaye Mungu mmoja atupaye Pumzi ya uhai Bure.

Wote Kwa nafasi zetu, tupite katika Uzi huu kumshukuru Mungu Kwa Kila nama atakayokujalia kumsifu na kumshukuru.

Ukiquote mstari wa Neno la Mungu, ni sawa, ukiweka wimbo ni sawa, ukishukuru Kwa maneno ya kinywa chako ni sawa, na hata ukisema tu "ASANTE", yatosha.

Karibuni🙏
 
Haya
 

Attachments

  • Screenshot_20231128-015042_1.jpg
    Screenshot_20231128-015042_1.jpg
    57.6 KB · Views: 4
(Ayubu 41:11).

"Ni nani aliyetangulia kunipa Ili nimlipe?

Kila kilicho chini ya Mbingu chini ni changu."

Ahsante ee Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,

Kumbe vyote vilivyomo ULIMWENGUNI ni vyako, pokea sifa hizi na utukufu EE MUNGU MKUU mtakatifu.

Amen.
 
Hawana akili nawapa za uso.

Kajibadilisha kuwa mwanadamu, ili ajiue mwenyewe(yeye ni Mungu hawezi kufa), ifanyike sadaka kwake yeye mwenyewe.

Huoni hadithi hizo?
Wanaelewa basi? Eti tulizaliwa tukakuta hivyo, na sisi tukafata mkumbo,na watoto wetu lazima wafate.

Ukisema akili hawana,utaonekaana mbaya. Kama aloleta hayo mwendawazimu? Si wao yale yale tuuu
 
(Zaburi 95.)

1: Njooni, tumwimbie BWANA, Tumfanyie shangwe MWAMBA wa Wokovu wetu,

2: Tuje mbele zake Kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe Kwa Zaburi.

3: Kwa kuwa BWANA ni Mungu Mkuu,

Na MFALME mkuu juu ya miungu yote.

4: Mkononi mwake zimo bonde za Dunia,

Hata vilele vya milima ni vyake.

5: Bahari ni yake, Ndiye aliyeifanya,

Na mikono yake iliumba Nchi kavu.

6: Njoni tuabuduo, tusujudu ,tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

7: Kwa maana ndiye Mungu wetu,

Na sisi tu watu wa malisho yake.

Na Kondoo za mkono wake,

ingekuwa heri Leo, msikie sauti yake.

8:Msifanye migumu mioyo yenu,
Kama vile huko Meriba,
Kama siku ya Masa jangwani.

9: Hapo waliponijaribu baba zenu,

Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

10: Miaka arobaini, nalihuzunika na kizazi kile,

Nikasema, hao ni watu waliopotoka mioyo,

11: Nikaapa Kwa hasira yangu,

Wasiingie rahani mwangu.

Aaameeen🙏
 
(Zaburi 148:1-14),

1: Haleluya, msifuni BWANA Kutoka Mbinguni,

Msifuni katika Mahali palipo juu,

2: Msifuni, Enyi Malaika wake wote.

Msifuni, majeshi yake yote,

3: Msifuni, jua na mwezi,

Msifuni, nyota zote zenye mwanga,

4: Msifuni Enyi Mbingu za mbingu,

Nanyi maji mlioko juu ya Mbingu,

5: Na vilisifu Jina la BWANA ,Kwa maana aliamuru vikaumbwa,

6: Amevithibitisha hata milele na milele,

Ametoa amri, Wala haitapita,

7: Msifuni BWANA Kutoka nchi,

Enyi nyangumi na vilindi vyote.

8:Moto, na mvua ya mawe,theluji na MVUKE,

Upepo wa dhoruba, ulitendalo neno lake,

9: Milima na vilima vyote,

Miti yenye matunda na mierezi yote.

10: Hayawani na wanyama wafugwao,
Vitambaavyo na ndege wenye mbawa.

11: Wafalme wa Dunia na watu wote,
WAKUU, na makadhi wote wa Dunia,

12: Vijana waume, na wanawali,

Wazee na watoto,

13: Na walisifu Jina la BWANA.

Maana Jina lake pekeake limetukuka,

Adhama yake, I juu ya nchi na Mbingu,

14: Naye amewainulia watu wake pembeni,

SIFA za utakuwa wake wote,

Wana wa Israeli, watu Walio karibu naye,

Haleluya.

Amen.🙏
 
Back
Top Bottom