Kila mtu anaushambulia mshahara wa mwezi

Habari za humu ndani wanajamii,
Mimi ni mfanyakazi kwa muda wa miaka kadhaa, nimetafakari sana nimeona kuwa kuwa mfanyakazi na kusubiri mshahara, ni wazi kuwa huwezi kuwa tajiri hata siku moja. Zaidi mshahara utakufanya tu ule, yaani uhakika wa watoto kupata mlo unakuwepo, haka kauhakika ndo kanapelekea watu kukimbilia kuajiriwa badala ya kujiajiri.
Ukweli ni kwamba, ukipata mshahara kila mtu anaupangia matumizi; TRA watatoa chao, Mifuko ya jamii itatoa chao, Bodi ya mikopo itatoa chao, vyama mbalimbali km CWT,TUICO, Bima za afya hasa kwa wafanyakazi wa serikali wanakata chao, kunatangazo huwa nalisikia sijui nao wanataka uchangie asilimia moja inaitwa Workers Fund sijui, vinaanzishwa tu ilimradi waukate mshahara.
Hapo hujakopa mkopo wakate rejesho lenye riba.

Hadi hapo huja involve personal expenses za Umeme, pango, chakula, mavazi ya watoto (wewe unaweza kuwa hata na kiatu kimoja tu). Bado ndugu nao watataka support (kumbuka ukiwakatalia wataona unawabania maksudi). Jamani jamani usione tunatembea tunastress nyingi mno...na hii hali ya uchumi ya sasa ndo balaa zaidi...... life is becoming harder and harder!
Hata ukiwa mfanyabiashara hayo yote yapo, na zaidi kuna kupata hasara na kufirisika, lakini hakuna kupata hasara kwenye mshahara labda uongezeke na si kupungua
 
Kuwa na kabiashara kadogo wakati umeajiriwa ni kitu muhimu sana, kwanza unaweza kuchukua mkopo benk kwa dhamana ya ajira na uufanye mtaji wa biashara. Biashara ikishamiri na faida ikiwa nzuri kuliko mshahara unaweza kutumbukiza nguvu zaidi na kuamua kuacha kazi.
 
Yani huo ndio ukweli kabisa. Kuna watu wanatoa majibu mepesi kwenye maswali magumu. Ishu hapa sio kuendekeza starehe bali hali halisi ilivo. Maisha ni magumu sana tusione watu wanakwenda makazini wengine wamependeza ila wingine wangekuambia ilivongumu kuumaliza mwezi tungewaonea huruma. Kila nikiwaza naona bado nina safari ndefu kabisa maana hali inakuwa hovyo kila siku zinavoongezeka. Najipa tu moyo ipo siku namni nitawaka hasa nikiwaangalia walio chini yangu zaidi napata sababu ya kumsukuru Mungu sana. So tusikate tamaa wakuu kujipanga, vipaumbeli, kuthubutu, kujituma, nidhamu binafsi, kumtegemea Mungu ni miongoni mwa vitu vitakavotupa ahueni hapo ktika maisha.
 
Habari za humu ndani wanajamii,
Mimi ni mfanyakazi kwa muda wa miaka kadhaa, nimetafakari sana nimeona kuwa kuwa mfanyakazi na kusubiri mshahara, ni wazi kuwa huwezi kuwa tajiri hata siku moja. Zaidi mshahara utakufanya tu ule, yaani uhakika wa watoto kupata mlo unakuwepo, haka kauhakika ndo kanapelekea watu kukimbilia kuajiriwa badala ya kujiajiri.
Ukweli ni kwamba, ukipata mshahara kila mtu anaupangia matumizi; TRA watatoa chao, Mifuko ya jamii itatoa chao, Bodi ya mikopo itatoa chao, vyama mbalimbali km CWT,TUICO, Bima za afya hasa kwa wafanyakazi wa serikali wanakata chao, kunatangazo huwa nalisikia sijui nao wanataka uchangie asilimia moja inaitwa Workers Fund sijui, vinaanzishwa tu ilimradi waukate mshahara.
Hapo hujakopa mkopo wakate rejesho lenye riba.

Hadi hapo huja involve personal expenses za Umeme, pango, chakula, mavazi ya watoto (wewe unaweza kuwa hata na kiatu kimoja tu). Bado ndugu nao watataka support (kumbuka ukiwakatalia wataona unawabania maksudi). Jamani jamani usione tunatembea tunastress nyingi mno...na hii hali ya uchumi ya sasa ndo balaa zaidi...... life is becoming harder and harder!
Una mke. Pesa ya sokoni. Watoto 2 nauli na ada ya shule. Mchango wa ujirani mwema mtaani kila wiki. Umeme luku. Mpenzi wa gazeti la udaku kila wiki. Mvutaji sigara.
 
Asante! Wewe bado uko shule?! Ukija mtaani punguza expectations, just be simple & flexible.
Haya maisha ya mshara haukutani na mwingine tutafika tumechoka
Mshara: 800,000
NSSF: 10% (80,000)
PAYE: (125,000)
HESLB 8%: (64,000)
TUICO. (42,480)
Mkopo: (178,000)
UMEME: (20,000)
Pango: (150,000)
Surplus: 140,520
Hapo fungu la kumi bado
 
Mtu wangu wa karibu alianza kazi mshahara 300,000. Tulimuuliza utamudu vipi maisha? Alituomba tu msaada wa freezer, alinunua cooler, basi asubuhi akawa anapanda basi na cooler lake la maji ya Kandoro, na Dar kulivyo na joto, mchana maji yamekwisha, bwana mshahara akawa anauwacha bank anasurvive kwa pesa ya maji. Kama utani alinunua kiwanja na amejenga nyumba, yuko kwake sasa hivi.
 
Ndipo maisha yalipofikia hapa Tz, kuna watu wanapambana kufana kupona lakini wanaishia pesa ya kula kodi ya nyumba matibabu hata ada ya watoto ni bahatinasibu.
 
Hata ukiwa mfanyabiashara hayo yote yapo, na zaidi kuna kupata hasara na kufirisika, lakini hakuna kupata hasara kwenye mshahara labda uongezeke na si kupungua
Wahanga wa kuajiriwa utawajua tu
 
Nikiwa mdogo kwenye zile government quarters wazazi walifuga kuku wa kienyeji. Ukisikia kuku anapiga kelele siye siye ujue msure mambo hayajakaa vizuri, menu leo ni chicken. Walistustiri hata wageni wakija ghafla kitweo kilikuwepo, tatizo kideri kipite.
:D:D:D:D
 
Haya maisha ya mshara haukutani na mwingine tutafika tumechoka
Mshara: 800,000
NSSF: 10% (80,000)
PAYE: (125,000)
HESLB 8%: (64,000)
TUICO. (42,480)
Mkopo: (178,000)
UMEME: (20,000)
Pango: (150,000)
Surplus: 140,520
Hapo fungu la kumi bado
Teh! Hakuna namna mkuu.
 
Tatizo watu wamekariri maisha.
Wapo waliojiajiri ila wananidham kubwa sana ye pesa,na wamewekeza kwenye biashara nyingine na hali hii haiwaathiri kivile na maisha yanasonga.

Wapo walioajiriwa,wao starehe tuu,magari,madem,kupombeka,michango ya ajabu,Sasa lazima utafeli tu,maana age haikusubiri,na maisha hayapangwi kwa kiinua mgongo.
Kuajiriwa ni kuzuri sana kama ukijipanga na kujitambua na kuwa mzuri kwenye ku save,basi utatoboa tu
Wewe unazungumza bila utafiti nipe unafuu wa mtumishi mwenye mshara wa laki sita amepanga nyumba ya shs 70'000 kwa mwezi anakaa ubungo kazini kwake posta. Ana familia ya mke na watoto 3. ata-save kiasi gani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom