mdesi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 1,366
- 2,202
Habari za humu ndani wanajamii,
Mimi ni mfanyakazi kwa muda wa miaka kadhaa, nimetafakari sana nimeona kuwa kuwa mfanyakazi na kusubiri mshahara, ni wazi kuwa huwezi kuwa tajiri hata siku moja.
Zaidi mshahara utakufanya tu ule, yaani uhakika wa watoto kupata mlo unakuwepo, haka kauhakika ndo kanapelekea watu kukimbilia kuajiriwa badala ya kujiajiri.
Ukweli ni kwamba, ukipata mshahara kila mtu anaupangia matumizi; TRA watatoa chao, Mifuko ya jamii itatoa chao, Bodi ya mikopo itatoa chao, vyama mbalimbali km CWT,TUICO, Bima za afya hasa kwa wafanyakazi wa serikali wanakata chao, kunatangazo huwa nalisikia sijui nao wanataka uchangie asilimia moja inaitwa Workers Fund sijui, vinaanzishwa tu ilimradi waukate mshahara.
Hapo hujakopa mkopo wakate rejesho lenye riba.
Hadi hapo huja involve personal expenses za Umeme, pango, chakula, mavazi ya watoto (wewe unaweza kuwa hata na kiatu kimoja tu).
Bado ndugu nao watataka support (kumbuka ukiwakatalia wataona unawabania maksudi).
Jamani jamani usione tunatembea tunastress nyingi mno...na hii hali ya uchumi ya sasa ndo balaa zaidi. Life is becoming harder and harder!