Kila mtu amekuwa mtaalamu wa computer!

Kila mtu amekuwa mtaalamu wa computer!

kabiriga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
1,163
Reaction score
1,213
Kuwa na ujuzi au elimu Fulani ni taaluma iwe ya kusomea au kujifunza kwa mtu anayejua vizuri taaluma hiyo. Lakini kinyume na hayo utakuta watu wengi kuonekana au kujifanya wana taaluma ya computer, ingawa sio kweli!

Mtaani VIJANA wengi na ata watu wazima wakishanunua au kumilikishwa komputer iwe ya Mpakato au ya mezani wakajua kutumia baadhi ya mifumo na ata kujua kidogo kufunga na kufungua shehemu mojawapo ktk computer kwao ni tiketi ya kujifanya wanaujuzi wa computer.

Ujuzi ni kwenda mbali zaidi ya kumiliki au kumilikishwa chombo husika, utawasikia wakisema computer hii imeharibika kitu Fulani lakini ukihoji wadadavue kwa undani wanaishia kujing'ata au kutoa majibu yasiyo na mantiki ya kifani.

Kujua kufomati au kubadili mfumo mmojawapo katika computer yako haina maana unaijua computer, kwa Kila mtaalamu ujuzi ni kufanya kitu kwa sababu na sio KWA kuiga au kukopi wengine wanafanyaje bila kuzingatia sababu ya msingi ya mabadiliko ktk computer husika.

Kwa wale walovamia fani za watu wajitafakali waachane na kuwadanganya watu Kuwa ni wajuzi wa computer kwani wanaharibu komputer za watu wengine. Vinginevyo waende shule wajifunze computer ni pana na ina fulsa Kubwa ya ajira.
 
Hayo mambo ya kila kijitatizo kidogo umwone fundi yalikuwa zamani. kuna vitu vingine hauitaji kumwona technician unaweza troubleshoot mwenyewe, inaonekana ndugu yangu wateja wamepungua pole sana, elimu ya computer imekuwa sana na watumiaji wameongezeka kwa hiyo usilalame hapa.
 
Anachokisema mkuu hapo juu ni kweli kabisa.. sawa inatakiwa kama mtumiaji wa kitu chochote uwe unajua jinsi ya kutatua mambo madogomadogo.. ila kwa hali ilivyo sasa huko mitaani si nzuri kila kona fundi kompyuta na ukienda na tatizo lolote lile hata kama adapter haichaji utaambiwa kuformatt.

Mi nlishenda sehem kununua tu kitu kingine nikakuta mtu amepeleka PC yake adapter inapiga shoti wakambia inabid kuformatt.. nilishangaa sana.. so anachosema ni sahihi.. sio wote ila wengi wa hawa vijana mitaani wanaojiita mafundi ni shida tupu..

kama kweli wanania wanatakiwa kujifunza zaidi.. tatizo unakuta hata mda wa kukaa kufungua tu online kujifunza vitu zaidi wengi wao ni games au picha za ajabu tu wakati wanainternet full time..
 
Hayo mambo ya kila kijitatizo kidogo umwone fundi yalikuwa zamani. kuna vitu vingine hauitaji kumwona technician unaweza troubleshoot mwenyewe, inaonekana ndugu yangu wateja wamepungua pole sana, elimu ya computer imekuwa sana na watumiaji wameongezeka kwa hiyo usilalame hapa.

kweli kaka upo sahihi, but kuna watu wengi nowday hua wanajifanya ni mafundi haswa upande wa hardware hua wanaharibu sana hili suala nakutana nalo mara nyingi sana kwa upande motherboard, na husababisha hasara kubwa sana kwa mwenye mali.

MFANO, kuna baadhi ya laptop acer mini zikileta black screen hapo inabidi ku-update bios kwa utu aliye-kariri ataacha ku-repair display processor na hapo ndio unakua mwisho wa computer kumbe tatizo lilikua ni ku-update bios kwa kutumia usb so hapo tatizo linakua kubwa sana inabidi kubadili motherboard.

Ushauri. kama computer yako ina tatizo kama sio mzoefu haswa masuala ya hardware jaribu vitu vidogo kama, kufuta vumbi, kubadili ram, hdd, processor, sound card, kwa complex issues kama kubadili ic, ac, capacitor, power unit, power diode, kupima components kwenye motherboard ni vizuri hizo kazi waachiwe wenye hiyo fani il kuepika hasara.
 
kabiriga You Deserve like !
sadly am using JF wapsite at this moment.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha! naona una bif na wazee wa kuformat kwa kila tatizo...
Watu wakikosa ajira vitu kama hivi lazima viwepo mbona, kuformat wanapiga hela maana atakuchaji hadi softwares kuinstall upya, hahaha
 
Eboo, Alaa ww huoni maendeleo hayo kila mtu fundi computer mm issue ndogondogo na solve mwenyewe na si mm watu wengi tuu ikiwa issue kubwa ndo uwende kwa fundi kwa issue za hardware na mnakimbiwa mafundi kwa tamaa zenuu ukenda kitu kidogo unaambiwa bonge la bei shida yote ya nn
 
mh hv labda mtu ame mute sauti ya computer je na hili nalo linahitaji fundi computer?
 
kitu mnachoshindwa kutofautisha hapa ni kuwa mafundi wengi kuwepo mtaani hatukatai kwani ni maendeleo kwa nchi na ndo tunavyotaka na pia bado kuna umuhimu wa kila mtumiaji wa kitu chochote kile (sio computer tu bali hata gari, redio tv,na vitu vingine vya kawaida) kujua jinsi ya kutatua matatizo madogo madogo ya kifaa chake ambapo naamini wengi wetu ndo tupo hivyo..

Tatizo linalokuja hapa ni kuwa kuna yale matatizo ambayo kwa mtumiaji wa kawaida hawezi hata ukimwelekeza hawezi kukuelewa ni lazima aonane na mtaalamu wa mambo hayo..mfano mtu hajawai kufungua pc yake hata siku moja leo cmos betri imetokea imekwisha nguvu inabidi abadilishe ataanzia wapi kufungua?

sasa unakuta mtu kama huyu pengine kila akiwasha pc yake anakuta time na date havipo sawa..kila siku anaset upya hajui tatizo nini anaenda kwa fundi ..fundi anamwambia inabidi tu formatt hii...haya mtu wa watu anakubali...wanaformatt bado tatizo liko pale pale anaambiwa harddisk au ram mbovu anajikunja mtu wa watu ananunua bado tatizo lipo palepale...mapaka anakata tamaa...

Shida hii inasababishwa na hawa watu wanaoharibu taaluma za wenzao..ndo maana nikasema hii ni taaluma wazi..mtuyoyote anaweza kuwa fundi ili mradi tu aongeze ujuzi...wajifunze!! sikuhizi mbona hata huitaji kwenda kukaa miaka mitatu darasani kama tulivyofanya wengine zamani ilimradi tu una internet na nia ya kujifunza..vitu vingi vipo free online..

Skuiz watu wengi sana wanaogopa kupeleka pc zao kwa mafundi...mfano mzuri mimi nina ujuzi wa kutosha wa pc ila sijawahi kufungua hata kibanda cha kutengeneza pc (sababu ya plans zangu) saiz nipo kama IT kwa kampuni binafsi ila nakutana na watu wengi sana ambao wao ndo wananitafuta niwatengenezee pc zao zinapopata matatizo...

wengine hata sijui wamenijuaje(si kama najisifia ila nataka tueleweshane) na ukiwaelekeza kwa mafundi wanagoma kabsaa yani na wanasema kabisa nilishapeleka wameshindwa afu mi nikienda kuangalia unakuta ni kitu cha kawaida kabiss ambacho hata mtu anaetaka kujifunza ukisearch google tu 10 mins unatatua tatizo..labda kama huna vifaa na kuna kipindi hata hao mafundi wenyewe wengi wao huwa wananitafuta niwafanyie baadhi ya kazi sababu hawajui...Sasa shida yote ya nini...??

Si wajifunze tu....?? ugumu uko wapi...unaenda kwa fundi pc unakuta mda wote ana internet ila yupo facebook anachat tu..au anacheza game au uanaangalia porn, muvi au music mda wote akiwa hamna mteja..wakatihata baadhi ya technical term za pc hazijui...kutenga hata 10mins tu za kujifunza hawezi unategemea nini..??Wacha tuwaseme bana ..wabadilike...!!
 
Kila kitu kipo kwenye mtandao Kila kitu tena hadi video bure huko YouTube.

Tatizo watu hawana hobby ya kujisomea. Kagua simu za wanafunzi kama utakuta app ya wikipedia huko ni bahati lakini hutakosa picha za hovyo hovyo Na miziki ya Kila namna!
 
Next ........ Next ........ finish . any body can do
na hizo next....next ndo zinazoongoza katika kuleta matatizo kwenye pc za watu...mtu ana click next tu bila hata kuchnguza hata kidogo kumbe anainstall na ma program mengine hatari kwa pc yake afu baadae anaanza kulia..!!
 
duh. mtu ameweka ram ya ddr2 5300 kwenye mobo inayo support maximum speed 4200. pc imegoma kuwaka anasema hii pc ni mbovu inachagua ram....... na ni fundi wa computer...
 
weli mkali mi mwenyewe ushanisaidia insue kibao kupitia jukwaa hili matatizo ambayo wazee wa kuformart walikuwa wakishindwa unakuta tatizo dogo wenyewe watakuambia lazima tu format nilikuta eneo flani kwa wazee wa kuformat mteja pc yake ile taskbar location on screen imeamia juu wanamwambia lazima kuformat.
 
na hizo next....next ndo zinazoongoza katika kuleta matatizo kwenye pc za watu...mtu ana click next tu bila hata kuchnguza hata kidogo kumbe anainstall na ma program mengine hatari kwa pc yake afu baadae anaanza kulia..!!
Mkuu sijui nini, kwa kuwa haupo kibishara I hope nitapata msaada mzuri wa ushauri...

I have Dell Laptop. Tatizo ni kwamba, ninapojaribu kuiwasha, huwa inatoa mlio wa kugonga na hivyo kushindwa kuwaka mara moja. Huu mlio huwa ni endelevu, nilishawahi ku-count nione utaishia wapi lakini hadi nafika 15, mlio ulikuwa unaendelea bila laptop kuwaka. Inapotokea hali kama hiyo, basi ni lazima niitekenye sana ndipo finally itawaka.

The question is: are you familiar with that problem? Do yu have any recommendation... kwa maana fundi unayemfahamu anayeweza ku-deal na issue kama hii? Nalazimika kuuliza kwanza coz' siku nyuma nimeshawahi kupoteza laptop mara mbili baada ya kuzipeleka kwa fundi! Good enough, wakati huo nilikuwa na uwezo wa kupata pesa ya chapchap na kuweza nunua nyingine pindi laptop inaponifia. For the time being, mnh! So, naogopa nisije nikapeleka kwa fundi kichwa kichwa na matokeo yake ndo nikashindwa moja kwa moja hata kuiwasha kwa kuitekenya na hivyo kusimamisha shughuli zangu moja kwa moja! Kama nitapata highlights, I hope hata ninapokutana na fundi, naweza kulinganisha maelezo yako na yake hata kama hayawezi kuwa sheria! Mathalani, ikiwa unasema tatizo is probably motherboard halafu yeye anasema tatizo ni DVD Rom basi bila shaka hapo busara itakuwa ni kumwambia "okay, nitakucheki basi mambo yakishakaa level...!"

Anyway, BETTER TO BE SAFE THAN SORRY!
 
Last edited by a moderator:
Alafu kitu kingine hawa vijana wameshusha ghalama ya kuservice computer na kuformat zamani miaka ya 2004 wakati nimetoka India kusoma hapa town kuformat computer tulikuwa tuna chaji siyo chini ya laki moja na nusu mpk laki mbili inategemea na mtu lakini siku hizi hawa watoto wanaformat kwa sh elfu tano? Jamani hata Microsoft wanasema kufanya installation isiwe chini ya USD 50 yani mpaka inauma Sana.
 
Mie sioni tatizo iwapo mtu anajua tatizo na anaweza kulishughulikia.Shida inakuja kwa wale wanaobahatisha!
 
Alafu kitu kingine hawa vijana wameshusha ghalama ya kuservice computer na kuformat zamani miaka ya 2004 wakati nimetoka India kusoma hapa town kuformat computer tulikuwa tuna chaji siyo chini ya laki moja na nusu mpk laki mbili inategemea na mtu lakini siku hizi hawa watoto wanaformat kwa sh elfu tano? Jamani hata Microsoft wanasema kufanya installation isiwe chini ya USD 50 yani mpaka inauma Sana.

First time nafanyiwa installation ndo nililipa hela hiyo mkuu' madogo kweli wameharibu game' ukiongea nao fresh mpaka buku tatu unafanyiwa installation..
 
Kuna jamaa kanifuata juzi kaniletea laptop yake anadai haoni data zake toka itoke kwa fundi,nikamuuliza tatizo lilikuwa nini mpaka akapeleka kwa fundi akasema sauti ilikuwa inakoroma.
Nilipoichunguza nikakuta kumbe huyo fundi kaiformat na kuweka OS upya na sasa sauti ndo haitoki kabisa,tatizo la hardware fundi kashughulikia software.
Nikaona atanichosha bure nikamwambia mpelekee fundi wako mwambie tatizo ni hili na hili basi..
 
mh hv labda mtu ame mute sauti ya computer je na hili nalo linahitaji fundi computer?
Hilo si tatizo la kiufundi ni tatizo la mtumiaji binafsi,mtumiaji anajua kutumia computer kwa kiwango gani.Tatizo wengi wanasema wanajua computer ila in reality hawajui.Lakini kama ukienda kwa fundi na wewe hujui kama umemute sauti kama ananjaa zake acha uchagie walau kidogo.Basic computer troubleshooting knowledge ni muhimu.
 
Back
Top Bottom