MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,644
- 33,442
Wanabodi,
Leo kwa namna ya pekee niwatakie heri timu ya Pamba FC, wanakawekamo, TP lindanda washinde na kurejea ligi kuu.
Mimi Pamba FC ndio ilikuwa timu yangu ya kwanza kushabikia na kuhudhuria mechi zao Nyamagana enzi hizo. Mchango wa Pamba kwenye soka letu ni mkubwa mno hasa kuibua vipaji vya pekee kutokea kanda ya ziwa. Nafikiri hakuna timu iliyoibua nyota kama Pamba kwa kipindi kirefu sana.
Pamoja na mimi kuwa na asili ya mkoa wa Kagera kutokea wilayani Kyerwa lakini leo hapana naiombea Pamba ishinde na wana Mwanza wajitahidi kuisaidia ili tuirudishe Pamba ile iliyoshinda timu ya shelisheli kwenye kombe la washindi barani Africa goli 12-0.
Kila lakheri wanakawekamo, tupwisa lindanda, Pamba ya Mwanza!! Kagera mniwie radhi kwa leo tuuu!