FT: Azam Sports Federation Cup | Simba SC 4-0 Pamba FC | Uwanja wa Mkapa (Sasa ni Simba Vs Yanga Nusu Fainali)

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup kuendelea kupigwa leo Mei 14, 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, anakipiga na TP Lindanda Wana Kawekamo Pamba FC, katika hatua ya robo fainali kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali hasa baada ya Pamba FC kutaka kuwavuruga Simba SC katika mipango yao ya kutetea ubingwa huu wa Kombe la Azam Sports Federation Cup.

Kocha wa Simba SC Pablo Franco Martin amesema kuwa anahitaji ushindi hivyo atapanga kikosi kamili kulingana na umuhimu wa mchezo huu.

"Michuano hii hakuna timu rahisi, huu ni mchezo muhimu kwetu tunahitaji kushinda ili kusonga mbele tutapanga kikosi kamili kwa wachezaji wote walio tayari kwa mchezo" amesema Kocha Pablo

Naye Kocha wa Pamba FC Athuman Kairo amesema kuwa wamakuja kupambana kupata matokeo ya ushindi.

"Tumekuja kupambana na Simba SC, tuajua kuwa ni timu kubwa, ngumu, nzuri, lakini sisi kama Pamba FC tunawaheshimu na tutacheza kwa nidhamu ili mwisho wa siku tupate ushindi na kuweza kusonga mbele kwenye nusu fainali" amesema Kocha Kairo.

Yote kwa yote ni dakika 90 za jasho na damu kuamua..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.. Usikose Ukaambiwa.

Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana

..... Ghazwat.....


======================

Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC Vs Pamba FC

00' Naaam mpiraaaaaaa umeanza

03' Peter Banda anashindwa kuweka mpira kambani baada ya kutokea Krosi ya Kibu, ilikuwa hatari lango la Pamba FC.

05' Nafasi nyingine tena kwa simba kushindwa kuandika bao, Mhilu anakosaaaaaa.

07' Bocco na Kibu wanashindwa kutumia nafasi nzuri ya kufunga, Simba hizi nafasi watajutia kama hawatapata ushindi.

10' Yusuf Mhilu tena anashindwa kuunganisha Krosi bomba ya Banda


Pamba FC hawajapata nafasi ya kumfikia golikipa wa Simba, Beno kutokana na mashambulizi yao kuishia kwa mabeki wa Simba SC

18' Jaribio la kwanza kwa Pamba FC kwa shuti kali, lakini golikipa Beno anarukaaaa na kuokoa hatari ile na kuwa Kona ambayo haikuzaa matunda

20' Simba SC 0-0 Pamba FC

Free Kick inapigwa kuelekea Simba SC lakini golikipa Beno, anadaka bila wasiwasi, Pamba FC wameamka sasa.

23' Nafasi nyingine kwa Simba, Bocco, anakosaaaaaa kichwa cha John Bocco kinashindwa kulenga lango, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga.

28' Simba SC wamepata Kona tatu mfululizo bila mafaniko ya kufunga.

33' Salum Sheshe wa Pamba FC anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumvuta Jezi Hussein

37' Robert Makidala anakosa nafasi nzuri ya kufunga, ilikuwa Shambulizi kali kuelekea Simba | wakati huo huo Mohamed Said ameoneshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Kibu

43' Pascal Wawa anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya, Pamba wanacheza eneo lao la nyuma kuwavuta Simba

45' Goooooooooooooaaal gooal
Peter Banda anaipatia Simba bao la kwanza | Simba SC 1-0 Pamba FC

45' Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza

Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili

46' Simba wanafanya mabadiliko, anatoka John Bocco anaingia Meddie Kagere

48' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kibu Denis anafunga bao la pili kwa Simba kwa kichwa, akimalizia mpira uliotoka kwa Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr'

50' Simba wanaendelea kumiliki mchezo.

52' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yusuph Mhilu anaipatia Simba bao la tatu kwa kichwa, amemalizia mpira kutoka kwa Kagere

Ametoka Mzamiru na ameingia Lwanga upande wa Simba SC

74' Mchezaji Mbaruku anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Peter Banda

76' Wawa yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kugongana na mchezaji wa Pamba FC

78' Yusuf Mhilu anapiga shutii lakini golikipa wa Pamba anacheza mpira na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

Pamba wanajibu Counter Attack mbele kuleee lakini golikipa Beno anadaka

88' Goooooooooooooaaal gooal
Yusuf Mhilu anaipatia Simba SC bao la nne | Simba SC 4-0 Pamba FC

90+3'
Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu

Wanamiliki mpira Simba, wanacheza eneo la nyuma, kwake Wawa sasa

Free Kick inapigwa kuelekea Simba SC, inapigwa kulee lakini mpira unatoka nje ya kuwa goal kick

Mpira umekwisha ambapo Simba SC wameibuka na ushindi mnono wa mabao manne kwa bila dhidi ya Pamba FC, na kutinga hatua ya Nusu Fainali

FT: Simba SC 4-0 Pamba FC

Kwa matokeo haya, sasa Simba itakipiga dhidi ya Yanga katika nusu fainali.
 
Simba na Pamba ni kama vile wanakutana mkubwa na mwanae.

Kila la kheri Mnyama ila mjue baada ya mechi hii mtakutana tena na Fiston Mayele akiwa anawasubiri
Mwambie huyo Mayele Inonga Baka amesema "He's not my type( Mayele), bring me another"
 
Yaani mechi haina hata mvuto! Wananchi walio wengi macho na masikio yao yapo kwenye mechi ya kesho Jumapili kati ya Bingwa wa Kihistoria dhidi ya Dodoma Jiji.
 
Wachezaji;

Mugalu

Kanoute

Lwanga

Wapo kamili baada ya kuwa majeruhi, kwahivyo ni uamuzi wa Kocha Pablo kuwatumia kwenye mchezo wa leo.
 
πŠπˆπŠπŽπ’πˆ 𝐂𝐇𝐀 π’πˆπŒππ€ πƒπ‡πˆπƒπˆ π˜π€ ππ€πŒππ€ 𝐅𝐂
1. Beno kakolanya
2. Jimmyson Mwanuke
3. Mohamed Hussein
4. Kenndy Juma
5. Pascal Wawa
6. Mzamiru Yassin
7. Peter Banda
8. Rally Bwalya
9. John Bocco
10. Kibu Denis
11. Yusuph Mhilu
𝐒𝐔𝐁
Ally, Gadiel, Hennock, Lwanga, Sakho, Kanoute, Kagere
 
Kazi kazi

Screenshot_20220514-183142~2.png
 
πŠπˆπŠπŽπ’πˆ 𝐂𝐇𝐀 π’πˆπŒππ€ πƒπ‡πˆπƒπˆ π˜π€ ππ€πŒππ€ 𝐅𝐂
1. Beno kakolanya
2. Jimmyson Mwanuke....
Mkubwa ni Mkubwa tu.
Pamba wanaliwa mapemaaa
 
Back
Top Bottom