KILA LA KHERI STD 7: Siku ya kwanza naingia FORM 1 ninakutana na Jamaa wanatema ung'eng'e kama watoto wa Trump

hapana mkuu, yule jamaa ni kukosa tuu ubinadam, alikua kanizd miaka mitano, yan alinipga mpk nikaingia kwenye mto huku nikiogelea kama chura, haikutosha akanifuata humo humo, nikaona isiwe tabu mbio nimejaaliwa nikatoka mbio nikakimbilia nyumb moja hv niliingia mpk chumbn kwa watu bla hodi nikajifcha mvunguni, wakanihfadh mpk nguo zikakauka ndo nikapewa mtu anisindkze home
Hahahaha
 
Hahahahaaa daaa huu usi(kimasai) ni mtamu balaa.Maisha ya u form one magumu Sana aisee.Huwa sipendi hata kukumbuka.
 
Mzee wangu alikuwa anatembea14KM shule, Mimi nilipoanza la 1 tulikuwa tunatembea 7KM, yaani nikiamka 12 asubhi nakimbia na ule umande ili niwahi kuhesabu namba. Hafu nafika shuleni ninelowa balaa. Enzi zetu walimu wote wamepitia JKT akikupa walikuwa wakakamavu, mchakamchaka usipikimbia darasani huingii.
Daah jamani. Halafu zamani palikuwaga na umande siku hizi hamna.
Miaka ipi hiyo ulisoma mkuu
 
we acha mkuu, unakutana na form 2 wale wababe na miaka ile ilikuwa inasoma mijitu kama baba zetu, unakuta limepewa adhabu ya kufyeka kiunga, nyoya ukikatiza unapewa kwanja yeye ndio anakuwa kama msimamizi, utafyeka lote, na usiku wakati wa kulala unafatwa, wanakata chandarua kisha mipira ya kuzibulia choo ndio zinakuwa fimbo, we acha tu, baada ya miaka 20 nilienda kutizama na kitanda nilichokuwa ninalala nikapiga sana story na wale mayanki, nikawaachia na pesa ya kununulia soda, walifurahi sana, tangu 1994 nimerudi tena 2015

Unamkumbuka Moddy Babu na Moddy White...
Moddy White aliniwekea ultimatum ya kukatiza mitaa ya Chemchem .... halafu ndo mitaa ya kuoga na emergency class.
 
Nakumbuka nilihama shule toka mwanza kwenda dar. Kimwanza mwanza nilikuwa nakuwa wa 15 kati ya wanafunzi 60 nilivyofika dar nikawa wa mwisho darasan.
Leo hii vijana waliokuwa tano bora nimewaajiri kwenye kampuni yangu. Yehova yire
 
Nakumbuka nilihama shule toka mwanza kwenda dar. Kimwanza mwanza nilikuwa nakuwa wa 15 kati ya wanafunzi 60 nilivyofika dar nikawa wa mwisho darasan.
Leo hii vijana waliokuwa tano bora nimewaajiri kwenye kampuni yangu. Yehova yire
uko vizuri mkuu. wambie vijana wachape kazi,
 
Nakumbuka siku ya Kwanza naikanyaga ardhi ya shule moja ya wasichana iliyopo hapa mjini dar...na bag langu la Revlon mama kanijazia madaftari 24..nimefika shule nimechoka nimevimbaa..alafu kufika shule napewa t-shirt la njano Yani walizidi kunivimbisha na lazima ulivae siku hiyo ya Kwanza..nililia nilivyo sipendi rangi za njano Mimi.

Katika pitapita zangu nikakutana na vitoto vinapiga un'gen'ge balaa ..vingine vimemaliza St Mary vingine Green acres na enzi hizo hizo shule zilikua motooo..naona vinachekelea kuvaa t-shirt za njano wakati mwenzao nimetoka kulia..nilitamani nivibamize.
 
Nakumbuka siku ya Kwanza naikanyaga ardhi ya shule moja ya wasichana iliyopo hapa mjini dar...na bag langu la Revlon mama kanijazia madaftari 24..nimefika shule nimechoka nimevimbaa..alafu kufika shule napewa t-shirt la njano Yani walizidi kunivimbisha na lazima ulivae siku hiyo ya Kwanza..nililia nilivyo sipendi rangi za njano Mimi.

Katika pitapita zangu nikakutana na vitoto vinapiga un'gen'ge balaa ..vingine vimemaliza St Mary vingine Green acres na enzi hizo hizo shule zilikua motooo..naona vinachekelea kuvaa t-shirt za njano wakati mwenzao nimetoka kulia..nilitamani nivibamize.
Duh, naona umeamua kuidisi rangi ya njano
 
Nakumbuka mwanza sec.hiyo ndo nimeanza kidato cha kwanza miaka hiyo nimetoka shule ya msingi kampani ya wacheza kamari tupu,nimefika shule nina kama mwezi nikapata kampani ya wacheza kamari muda wa vipindi tukaenda kwenye darasa moja lilikuwa linajengwa tukaanza kamari kama kawaida.muda si muda nikaona mtu anachungulia kupitia kwenye tundu lililokuwa chini ya ukuta,mimi kwa haraka haraka nikajua mwanafunzi analeta u spy,aisee niliokota mchanga nikarusha kwenye tundu nilisikia tu kilio cha "mungu wangu" kumbe alikuwa madam mmoja mwalimu wa advance.Ilikuwa ni mtafutano dakika 2 nyingi tulikuwa tushachakazwa na lundo la viranja na wababe wengine mixer walimu.tulikula fimbo siku hiyo sitasahau.
 
pale arusha sec sitasahau..siku moja tumeingia shift ya mchana..kikawaida shift yetu form one tulikua tunaingia na form 4,siku hiyo form four hawakuwepo coz walikua na mtihani ya mock..so kuna mwalimu wa zamu alikua anaitwa mollel akanipa kazi ya ukiranja wa muda..nikashindwa kuwaambia wanafunzi wenzangu mguu pande, mguu sawa kwa kiingereza..asee wenzangu walicheka hatari.
 
wala usipime mkuu, nakumbuka wakati naanza form one milambo tabora alikuwepo msukuma 1 wa bariadi anajiita form ten, alinipa shs 1 na kusema anataka sigara 5, kipande kimoja cha sabuni kisha nirudishe chenji yake shs 100, ikabidi zinitoke za kwangu na shs 100 nikampa, ilikuwa mwaka 1991, wale watoto wa kikwete hawajakumbana na haya mambo,enzi hizo tunaitwa nyoya, sorokoto, nguruwe, kwani akili zetu zilikuwa zinafananishwa na nguruwe, manake tukiulizwa what is the molecular formula hatujui hivyo tukawa tunafananishwa na nguruwe,

Form one Nilikuwa mwaka 1990
 
Mimi nimeenda form one English imelala kichwani, sema kipindi nasoma hapakuwa na kuonewa onewa. Full kudeka. Kila mwisho wa mwezi visiting day. Unaletewa makuku, keki za Sunkist , karanga, bluband na mikate. Nafungia kwenye tranka hadi vinaota ukungu.
Kwa uchoyo nilikuwa nambari moja.

Umesoma English medium,Hongera yako kuchelewa kuzaliwa
 
Back
Top Bottom