KILA LA KHERI STD 7: Siku ya kwanza naingia FORM 1 ninakutana na Jamaa wanatema ung'eng'e kama watoto wa Trump

wala usipime mkuu, nakumbuka wakati naanza form one milambo tabora alikuwepo msukuma 1 wa bariadi anajiita form ten, alinipa shs 1 na kusema anataka sigara 5, kipande kimoja cha sabuni kisha nirudishe chenji yake shs 100, ikabidi zinitoke za kwangu na shs 100 nikampa, ilikuwa mwaka 1991, wale watoto wa kikwete hawajakumbana na haya mambo,enzi hizo tunaitwa nyoya, sorokoto, nguruwe, kwani akili zetu zilikuwa zinafananishwa na nguruwe, manake tukiulizwa what is the molecular formula hatujui hivyo tukawa tunafananishwa na nguruwe,
Mkuu umenikumbusha tabora mambo ya sorokoto hahahaha
 
M ninachokumbuka ni siku ya kwanza kuingia darasa la kwanza baada ya kumaliza vidudu, nilienda na ubabe wangu wa vidudu matokeo yake nilirud nyumb na manundu ya kutosha usoni, Mather aliumia sana ila kuanzia bro , sister na mshua kila wakiniangalia nilivyovimbishwa wanakufa kwa kicheko. Yule jamaa alienipigaga drsn alikua hamnazo ila sijui kaptia njia gan huko asaiv ni mjeda, kwa kpgo kile JKT limepata mtu hawakukosea
hahaha, Darasa la Kwanza. Tulikuwa tumerundikwa darasa moja linavumbi na madesk kma mawili hivi.
Kuna kadogo kabisa tulizinguana kakanipiga ngumi ya pua damu zikatoka mkuu.
Nilionekana mnyonge sana maana kale kadogo kalikuwa kwa umbo dogo ndio kamwisho kwa urefu.
Kama unavyojua Utotoni ukitolewa damu ndio umepigwa hata, umdunde opponent hadi azimie, kama hajatoka damu WEWE UMEPIGWA.

hahaha
 
mkuu ulikuwa kibonge nini?
hapana mkuu, yule jamaa ni kukosa tuu ubinadam, alikua kanizd miaka mitano, yan alinipga mpk nikaingia kwenye mto huku nikiogelea kama chura, haikutosha akanifuata humo humo, nikaona isiwe tabu mbio nimejaaliwa nikatoka mbio nikakimbilia nyumb moja hv niliingia mpk chumbn kwa watu bla hodi nikajifcha mvunguni, wakanihfadh mpk nguo zikakauka ndo nikapewa mtu anisindkze home
 
Mkuu umenikumbusha tabora mambo ya sorokoto hahahaha
Tabora boys mkuu au Mirambo. maana hap boys lazima ubukue vya kutosha. Mtaani uswazi mtoto akienda Tabora Boys au shule maalumu ni tukio la kusimamisha mtaa enzi zangu.
 
hahahahaha
 
Mkuu umenikumbusha tabora mambo ya sorokoto hahahaha
we acha mkuu, unakutana na form 2 wale wababe na miaka ile ilikuwa inasoma mijitu kama baba zetu, unakuta limepewa adhabu ya kufyeka kiunga, nyoya ukikatiza unapewa kwanja yeye ndio anakuwa kama msimamizi, utafyeka lote, na usiku wakati wa kulala unafatwa, wanakata chandarua kisha mipira ya kuzibulia choo ndio zinakuwa fimbo, we acha tu, baada ya miaka 20 nilienda kutizama na kitanda nilichokuwa ninalala nikapiga sana story na wale mayanki, nikawaachia na pesa ya kununulia soda, walifurahi sana, tangu 1994 nimerudi tena 2015
 
hapana mkuu, yule jamaa ni kukosa tuu ubinadam, alikua kanizd miaka mitano, yan alinipga mpk nikaingia kwenye mto huku nikiogelea kama chura, haikutosha akanifuata humo humo, nikaona isiwe tabu mbio nimejaaliwa nikatoka mbio nikakimbilia nyumb moja hv niliingia mpk chumbn kwa watu bla hodi nikajifcha mvunguni, wakanihfadh mpk nguo zikakauka ndo nikapewa mtu anisindkze home
Mkuu unajua nipo kwenye daladala
 
Tabora boys mkuu au Mirambo. maana hap boys lazima ubukue vya kutosha. Mtaani uswazi mtoto akienda Tabora Boys au shule maalumu ni tukio la kusimamisha mtaa enzi zangu.
Mi nilikua mnyinge sana shule ya isevya sec kule mlikua nyie boys mnaibuka kuchukua watoto kule hahahah
 
Mi nilikua mnyinge sana shule ya isevya sec kule mlikua nyie boys mnaibuka kuchukua watoto kule hahahah
mkuu uwezo wangu na washule yangu ya msingi ulikuwa ni wa kuungaunga mkuu. huko tulikuwa tunapatamani tu, lakini tuliishia shule za mchangani hapohapo mjini kwetu. Huko Mboka sikusomea
 
Early 1960s with mates Hayati Joseph Mungai and Prof Peter Mahmoud Msolla

Malangali Secondary Siku zinaenda Kwa kasi
Kipindi hicho mzee wangu (baba) yupo around 10 yrs, nami nilikuwa bado kiunoni mwake.
Acha nikupe heshima yako mzee.
 
Mimi nimeenda form one English imelala kichwani, sema kipindi nasoma hapakuwa na kuonewa onewa. Full kudeka. Kila mwisho wa mwezi visiting day. Unaletewa makuku, keki za Sunkist , karanga, bluband na mikate. Nafungia kwenye tranka hadi vinaota ukungu.
Kwa uchoyo nilikuwa nambari moja.
Mtoto wa kizazi cha digital inabidi usalimie wakubwa dark angel
 
Kwa mara ya kwanza nilikutana na vijana wa kike na wakiume ambao Kiinglish kimelala.

Zoezi la kwanza lilikuwa "Explain about Yourself''
Hapo ilikuwa ni patashika, maana kuna watu hadi tulitungiwa majina kwa kujitutumua kuongea brokeni.
Jamaa walikuwa wanafloo utadhani wamezaliwa Boston.
Nakumbuka kuna kipindi nilitembea nashika mdomo brocken isijenichomoka ghafla nikachekwa, au nikaongea Kiswahili nikavalishwa PEMBE LA NG'OMBE.

Sio sili wale madogo walitupa tabu sana. Wamekariri nyimbo zote za westlife, Boy2Men, Maria Kerry na wakina Celine dione, wanajua kompyuta, wataalam wa kucheza games wakati sisi wakali wakitaa tunajua nyimbo za Muumini Mwinjuma, Kuangalia Movie za Vibanda umiza na Kucheza live games (glori, streetfootball na Karata(mabambo, albastini na unampa mtu joka anakula tano) ). Michezo non-computerized, michezo ya kiswahiliswahili tu.

Daa!!!
Lakini mwisho wa siku Leo kumbe tulikuwa tunaenda safari moja tu.Leo tuko kitaa level kila aliyetoka ni kwa bidii yake tu sio shule aliyopitia. Kwanza wengi hesabu huwa hawajui sana.

wakuu nimekumbuka kidogo Form one yetu, mara ya kwanza kukutana na mtoto wa kitanzania anayejua kugonga ung'eng'e bila kuyumba huku mzee Matunduizi najua Salamu ya Gudimorni tu na mbinu za Kufahulu Kiingereza mtiani wa Necta la saba.

hahahaa
ST KAyumba wenzangu mkifahulu La saba, mkajichanganya na wainglishi msipaniki. Pigeni kaziii
mkuu ilikuwa mwaka gani huo
 
Baba yangu huwa ananihadithia alikuwa anatembea km 15 kwenda shule hapo bado kurudi.
Aise nyie wahenga mlitaabika sana.
Mzee wangu alikuwa anatembea14KM shule, Mimi nilipoanza la 1 tulikuwa tunatembea 7KM, yaani nikiamka 12 asubhi nakimbia na ule umande ili niwahi kuhesabu namba. Hafu nafika shuleni ninelowa balaa. Enzi zetu walimu wote wamepitia JKT akikupa walikuwa wakakamavu, mchakamchaka usipikimbia darasani huingii.
 
Mimi nimeenda form one English imelala kichwani, sema kipindi nasoma hapakuwa na kuonewa onewa. Full kudeka. Kila mwisho wa mwezi visiting day. Unaletewa makuku, keki za Sunkist , karanga, bluband na mikate. Nafungia kwenye tranka hadi vinaota ukungu.
Kwa uchoyo nilikuwa nambari moja.
Hahahaha
 
Back
Top Bottom