KILA LA KHERI STD 7: Siku ya kwanza naingia FORM 1 ninakutana na Jamaa wanatema ung'eng'e kama watoto wa Trump

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,571
15,321
Kwa mara ya kwanza nilikutana na vijana wa kike na wakiume ambao Kiinglish kimelala.

Zoezi la kwanza lilikuwa "Explain about Yourself''
Hapo ilikuwa ni patashika, maana kuna watu hadi tulitungiwa majina kwa kujitutumua kuongea brokeni.
Jamaa walikuwa wanafloo utadhani wamezaliwa Boston.
Nakumbuka kuna kipindi nilitembea nashika mdomo brocken isijenichomoka ghafla nikachekwa, au nikaongea Kiswahili nikavalishwa PEMBE LA NG'OMBE.

Sio sili wale madogo walitupa tabu sana. Wamekariri nyimbo zote za westlife, Boy2Men, Maria Kerry na wakina Celine dione, wanajua kompyuta, wataalam wa kucheza games wakati sisi wakali wakitaa tunajua nyimbo za Muumini Mwinjuma, Kuangalia Movie za Vibanda umiza na Kucheza live games (glori, streetfootball na Karata(mabambo, albastini na unampa mtu joka anakula tano) ). Michezo non-computerized, michezo ya kiswahiliswahili tu.

Daa!!!
Lakini mwisho wa siku Leo kumbe tulikuwa tunaenda safari moja tu.Leo tuko kitaa level kila aliyetoka ni kwa bidii yake tu sio shule aliyopitia. Kwanza wengi hesabu huwa hawajui sana.

wakuu nimekumbuka kidogo Form one yetu, mara ya kwanza kukutana na mtoto wa kitanzania anayejua kugonga ung'eng'e bila kuyumba huku mzee Matunduizi najua Salamu ya Gudimorni tu na mbinu za Kufahulu Kiingereza mtiani wa Necta la saba.

hahahaa
ST KAyumba wenzangu mkifahulu La saba, mkajichanganya na wainglishi msipaniki. Pigeni kaziii
 
wala usipime mkuu, nakumbuka wakati naanza form one milambo tabora alikuwepo msukuma 1 wa bariadi anajiita form ten, alinipa shs 1 na kusema anataka sigara 5, kipande kimoja cha sabuni kisha nirudishe chenji yake shs 100, ikabidi zinitoke za kwangu na shs 100 nikampa, ilikuwa mwaka 1991, wale watoto wa kikwete hawajakumbana na haya mambo,enzi hizo tunaitwa nyoya, sorokoto, nguruwe, kwani akili zetu zilikuwa zinafananishwa na nguruwe, manake tukiulizwa what is the molecular formula hatujui hivyo tukawa tunafananishwa na nguruwe,
 
Ila sitasahau, kuna ngosha mmoja alitoka Maganzo dogo yuko fomu One wakati tuko 5/6 boarding, pamoja na kuonewa kote kwa form one Akajitosa KUGOMBEA URAIS WA SHULE.

hahaha tatizo alikuwa kikojozi balaa. Ila sound ni mbaya ukimpa sikio lazima akutapeli. Tangu siku hizo wasukuma siwachukulii poa kabisa.. Anaweza kuongea kishambakishamba ukamdharau kuja kustuka kumbe Yuko smart na makini kuliko maneno yake anayoongea kizembekizembe. Hasa wale wa mwambao wa simiyu.
Yule dogo alikuwa ni balaa aliwateka kiakili kuanzia form one wenzake, viongzi wa wanafunzi na waalimu. Ndio Form one pekee jasiri niliwahi kumshuhudia
 
hahahaha, sie hata timu ya mpira form one hata ucheze kuliko ronaldo, yani hawakufirkii kabisa, tuliwahi cheza na madarasa yote na tukawatoa kamasi lakini kulikuwa hamna njuka hata 1 katika timu ya shule
 
Kama wewe umesoma enzi hizi za gemu na kompyuta , basi ni wale wale kizazi ambacho hawachapwi viboko wala hawakoromewi na mwalimu ukifanhya hivyo tuu chochote chaweza kutokea. Enzi za mwalimu tulitumia slide rule , four figure kufanya calculation. Hata hivyo hao waongea ngeli ni mbwembwe tuu maana bongo wengi hatujui. Ukimwambia aongee kiswahili ndio atachanganya ma u know kibao lakini mbane sawa aongee chenyewe tupu ndio utacheka. Mwanzoni ataanza kwa mbwembwe kama anaongea lafudhi ya kimarekani huku vidole akiongesha ishara ya inverted comma hasa wanawake, lakini baada ya dakika 3 msamiati unaanza kupotea na kuanza kuchanganya tense. Bongo bana!! hivi nani alifuta yale mashindano ya wanavyuo Africa ya " ZAIN INTERUNIVERISITY CHALLANGE?" maana ilikuwa raha kweli kweli wanafunzi wa bongo wakuiliza wanajibu PASS, PASS
 
hahaha
mkuu hii ilikuwa ni jioni ya miaka ya Tisini na asubuhi ya miaka ya elfu mbili.
Four figure tumetumia. japo log 2 ilikuwa inafahamika ni 0.3010
Hayo mambo ndiyo yalikuwa yanaingia.
Mwenyewe mara ya kwanza kuiona PC ilikuwa ni internent cafe nikaenda kushangaa monitor. nilijua monitor ni kiongozi wa darasa.
Bakora nimekula sana hadi damu ila sikufa mkuu.
 
hahahaha, sie hata timu ya mpira form one hata ucheze kuliko ronaldo, yani hawakufirkii kabisa, tuliwahi cheza na madarasa yote na tukawatoa kamasi lakini kulikuwa hamna njuka hata 1 katika timu ya shule
hao jamaa walikwa wamezidi unoko.
Ubabe wa kinamtemi myugumba huo ulikuwa unaua Vipaji. Eti jambo zuri halliwezi kufanywa na NYOYA.
 
wala usipime mkuu, nakumbuka wakati naanza form one milambo tabora alikuwepo msukuma 1 wa bariadi anajiita form ten, alinipa shs 1 na kusema anataka sigara 5, kipande kimoja cha sabuni kisha nirudishe chenji yake shs 100, ikabidi zinitoke za kwangu na shs 100 nikampa, ilikuwa mwaka 1991, wale watoto wa kikwete hawajakumbana na haya mambo,enzi hizo tunaitwa nyoya, sorokoto, nguruwe, kwani akili zetu zilikuwa zinafananishwa na nguruwe, manake tukiulizwa what is the molecular formula hatujui hivyo tukawa tunafananishwa na nguruwe,
Upo form one hata sijazaliwa.
Heshima yako mkuu
 
hahaha eti form 10
 
Mimi nimeenda form one English imelala kichwani, sema kipindi nasoma hapakuwa na kuonewa onewa. Full kudeka. Kila mwisho wa mwezi visiting day. Unaletewa makuku, keki za Sunkist , karanga, bluband na mikate. Nafungia kwenye tranka hadi vinaota ukungu.
Kwa uchoyo nilikuwa nambari moja.
 
dah mi nilikuwa naletewa madaftari na vitabu -inakera mno
 
Mimi nimeenda form one English imelala kichwani, sema kipindi nasoma hapakuwa na kuonewa onewa. Full kudeka. Kila mwisho wa mwezi visiting day. Unaletewa makuku, keki za Sunkist , karanga, bluband na mikate. Nafungia kwenye tranka hadi vinaota ukungu.
Kwa uchoyo nilikuwa nambari moja.
hii itakuwa IST hii. Ada mil40 kwa muhula wakati wenzako elfu Kumi tu lakini kuilipa mbinde hadi Unatumwa ulete mzazi na mboko juu.
hahaha
 
Back
Top Bottom