KILA LA KHERI STD 7: Siku ya kwanza naingia FORM 1 ninakutana na Jamaa wanatema ung'eng'e kama watoto wa Trump

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,569
15,306
Kwa mara ya kwanza nilikutana na vijana wa kike na wakiume ambao Kiinglish kimelala.

Zoezi la kwanza lilikuwa "Explain about Yourself''
Hapo ilikuwa ni patashika, maana kuna watu hadi tulitungiwa majina kwa kujitutumua kuongea brokeni.
Jamaa walikuwa wanafloo utadhani wamezaliwa Boston.
Nakumbuka kuna kipindi nilitembea nashika mdomo brocken isijenichomoka ghafla nikachekwa, au nikaongea Kiswahili nikavalishwa PEMBE LA NG'OMBE.

Sio sili wale madogo walitupa tabu sana. Wamekariri nyimbo zote za westlife, Boy2Men, Maria Kerry na wakina Celine dione, wanajua kompyuta, wataalam wa kucheza games wakati sisi wakali wakitaa tunajua nyimbo za Muumini Mwinjuma, Kuangalia Movie za Vibanda umiza na Kucheza live games (glori, streetfootball na Karata(mabambo, albastini na unampa mtu joka anakula tano) ). Michezo non-computerized, michezo ya kiswahiliswahili tu.

Daa!!!
Lakini mwisho wa siku Leo kumbe tulikuwa tunaenda safari moja tu.Leo tuko kitaa level kila aliyetoka ni kwa bidii yake tu sio shule aliyopitia. Kwanza wengi hesabu huwa hawajui sana.

wakuu nimekumbuka kidogo Form one yetu, mara ya kwanza kukutana na mtoto wa kitanzania anayejua kugonga ung'eng'e bila kuyumba huku mzee Matunduizi najua Salamu ya Gudimorni tu na mbinu za Kufahulu Kiingereza mtiani wa Necta la saba.

hahahaa
ST KAyumba wenzangu mkifahulu La saba, mkajichanganya na wainglishi msipaniki. Pigeni kaziii
 
Back
Top Bottom