Kila kitu mjini unanunua

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,420
40,405
Si lazima kuishi mjini kama hujajiwekea biashara ndogo ndogo zinazokuingizia kipato kama sio biashara kubwa; kwa sababu, kila kitu mjini unanunua, kwa mfano:-
  • Chumvi unanunua
  • Nyanya unanunua
  • kitunguu unanunua
  • mchicha unanunua
  • nyama unanunua
  • kuku unanunua
  • mchele unanunua
  • unga unanunua
  • maji unalipia
  • umeme unalipia
  • nguo unanunua
  • majani ya chai unanunua
  • pilipili unanunua n.k
Kwa kifupi, kila kitu unanunua; hakuna unachokizalisha wewe kutoka kwenye shamba lako au 'workshop' yako.

Je leo hii, ile 'chanel' inayokupa hela ikifa, na wewe si utakufa?

Kwa sababu hutoweza kununua chochote ata mchicha wa shilingi 50.

Mjini cha bure ni shikamoo tu, pamoja na habari za sasa hizi au umeshindaje?
 
Back
Top Bottom