Wengi huchukulia mafanikio ya kiuchumi kama baraka kubwa kuliko zote..
Kuna waliobarikiwa elimu lakini uchumi mbovu... Familia nzima imejaa wasomi tena wa kaliba mbalimbali lakini maisha yao hayaeleweki
Kuna waliojaaliwa watoto, yani kwao uzazi sio ishu... Wakigusa tu mtoto... Hii ni baraka, lakini maisha yao ni ya kuungaunga,
Kuna familia zimejaaliwa utajiri na ukwasi wa kutisha lakini kati yao hakuna upendo.. N roho mbaya mwanzo mwisho
Asili ya baraka na laana imo kwenye misahafu na ina historia ndefu huku kuliwa na mifano mingi.
Mfano mmojawapo maarufu sana ni mfano wa mfalme Suleiman... Mtu huyu katika mazungumzo yake na Mungu (kwa njia ya maono na unabii) aliulizwa anataka nini toka kwa Mwenyezi Mungu... Yeye akaomba hekima...! Wengi wetu leo hii wanaomba utajiri, tembelea yale makanisa ya kileo utaona...!
Mungu akampa mfalme Suleiman HEKIMA kama alivyoomba lakini akaongezewa na utajiri... Inasemekana mpaka leo hii hakuna aliyeweza kumfikia Suleiman kwa utajiri na ukwasi
Laana ndani ya baraka za Suleiman mfalme ni ipi?
Dhambi ya asili... Chini ya jua hakuna kiumbe mkamilifu la hata mmoja... Wote ni watenda dhambi na wamepungukiwa na utukufu wa MUNGU
Pale kati patamu.... Suleiman pamoja na hekima zote na utajiri uliotukuka lakini alikuwa dhaifu mno kwenye swala zima la masukubasi.. Inasemekana alikuwa na wake 300 wa ndoa na masuria (nyumba ndogo) idadi kama hiyo.. Ama pengine kuzidi.... Lakini akaja kumtamani mke wa mjakazi wake.... LAANA! na ili apate kummiliki kikamilifu nadhani alimfanyia mjakazi wake figisu mbaya
Zitumie vema baraka na vipawa vyako, usipotoke na kuanguka mazima... Makinika kila penye baraka kuna laana....