Kila baraka ina laana ndani yake

Kila baraka ina laana ndani yake

Hakuna baraka wala hakuna laana wala karma hayo mambo yote uliyoyataja yapo tu...na kuna watu wana almost kila kitu wanachokitaka au wako kwenye process za kukipata including mimi
 
Sawa, lakini pia Imeandikwa " Baraka Za mwenyeHaki hazichangamani na huzuni"
Je huo mstari unamaana gani labda??
 
Kama kumbukumbu zangu ziko poa aliyemtamani na kumchukua mke wa mtumishi wake kwa kumfanyia zengwe afe hakua Suleiman Bali alikua babake na Suleiman (Daudi ) ndo alifanya ivoo kwa askari wake aliitwa uria

Daudi Aliweka order jamaa (uria) awekwe Mbele sehemu ya vita vikali ili afe na kweli akafa

Then huyo mwanamke aliyechukuliwa na Daudi ndo baadae akamzaa Suleiman baada ya mtoto wake wa kwanza kufa

Anyway thanks for good lesson
Asante sana kwa ufafanuzi, nasikia pia Suleiman alifuata nyayo hizi za baba yake... Like fadha like son... Bado natafuta ithibati
 
Sawa, lakini pia Imeandikwa " Baraka Za mwenyeHaki hazichangamani na huzuni"
Je huo mstari unamaana gani labda??
Yes ni baraka za Mwenyezi Mungu sio za mwanadamu, zinapoenda kwa mwanadamu asiye mkamilifu lazima kuna mahali atakengeuka na kuharibu
 
Hakuna baraka wala hakuna laana wala karma hayo mambo yote uliyoyataja yapo tu...na kuna watu wana almost kila kitu wanachokitaka au wako kwenye process za kukipata including mimi
OK sawa asante na hongera sana
 
hakuna kazi ngumu kama ya kuwaongoza wanaadamu, hakuna nabii ambae hakupata shida katika kutangaza neno la mungu, mwanaadamu siku zote anapoona umemzidi huangalia kasoro zako ili akukosowe, ijapokuwa kile ambacho anachokipata kutoka kwa aliemzidi ni kikubwa kuliko kuangalia udhaifu, ndio wengine wajifanyao wajanja na hawataki kuona kuwa binaadamu wako tofauti na wamezidiana hubuni njia tofauti za kujitetea, leo hii utasikia kama kuna makosa basi tujifunze kutokana na makosa, huwezi kuendelea au kupiga hatua yoyote kama utafuata methali hii, mungu alivyowachagua watu ambao watafikisha neno lake miongoni mwa wanaadamu hakuwaumba tofauti, aliwaumba wakiwa ni wanaadamu kama tulivyo sisi, wanamapungufu ya kiubinaadamu kama tulivyo sisi, sisi tunaumwa na wao wanaumwa, sisi tunakula na wao wanakula, na mengi mengimeyo, hawakuwa malaika leo hii ukimuangalia nabii mussa alikuwa na kasoro ya kimaumbile katika lafidhi yake, alikuwa hayapati vizuri maneno, na ndio maana kuna dua alikuwa akiomba kila siku ( rabbi-shrahlii swadrii, wayassirly amri, wahlul-uqdata min lisaanii, wajaally waziira min ahly, yafqahuu qaulii) alikuwa akiomba mungu amjaalie na uwezo wa kupata lafudhi nzuri mbele ya umma wake na akaomba amjaalie msaidizi katika jamaa zake na ndio maana mungu akamteulia haroun kuwa msaidizi wake, hii ni dua tangu nabii mussa mpaka leo hii waislamu huisoma hasa kwa masheikh wanaotangaza neno la mungu, sasa ukisema unataka kumtoa kasoro nabii mussa kwa kutokuwa na lafudhi nzuri kuliko wewe ukajiona wewe ni bora kuliko yeye, jaribu kwanza kuangalia historia yake, asili ya nabii mussa kukosa lafudhi nzuri ni kutokana siku aliotafuna kaa la moto, mussa baada ya kufikishwa kwenye kasri la firauni, ikumbukwe tayari firauni alishatoa amri kila mtoto wa kiume atakaezaliwa auwawe, eti kisa aliota ndoto kuna mtoto atazaliwa na kuja kuupindua utawala wake, na firauni kama ilivyo kwa watoto wengine aliowauwa na mussa pia hakuaminika mbele ya firauni, ndipo alipotoa rai ya kujaribiwa kama kweli anayo akili inayoweza kuwa sababu ya yeye kuja kumpindua, liliwekwa kaa la moto na tende, nabii mussa aliekewa mbele yake achague, na kwasababu alikuwa mtoto hakuwa na akili hiyo, alitaka kuchaguwa tende lakini ghafla mwenyezi mungu akamteremsha malaika wake jibril akaukwepesha mkono na kuupeleka kwenye kaa la moto, halikuwa chaguo la mussa lilikuwa chaguo la mungu, kaa la moto lilikuwa na madhara makubwa kwake lakini hiyo ni mipango ya mungu, ni binaadamu wachache sana wenye uthubutu ya kujishusha mbele ya wengine, hata kama wamezidiwa vipi na siku zote asiekubali kushindwa si mshindani ni bepari.
 
Asante sana kwa ufafanuzi, nasikia pia Suleiman alifuata nyayo hizi za baba yake... Like fadha like son... Bado natafuta ithibati
Kuwazungumza mitume na manabii kunataka nidhamu na uadilifu wa hali ya juu sana.

Kwangu mwenendo huu naona si sahihi na ni kuwashushia heshima ukijumlisha watu hawana ushahidi juu ya haya wayasemayo.

Tuwekeni kila kitu mahala pake viongozi.
 
Inshallah... Radhi kwa kupotoka
 
Wengi huchukulia mafanikio ya kiuchumi kama baraka kubwa kuliko zote..
Kuna waliobarikiwa elimu lakini uchumi mbovu... Familia nzima imejaa wasomi tena wa kaliba mbalimbali lakini maisha yao hayaeleweki
Kuna waliojaaliwa watoto, yani kwao uzazi sio ishu... Wakigusa tu mtoto... Hii ni baraka, lakini maisha yao ni ya kuungaunga,
Kuna familia zimejaaliwa utajiri na ukwasi wa kutisha lakini kati yao hakuna upendo.. N roho mbaya mwanzo mwisho
Asili ya baraka na laana imo kwenye misahafu na ina historia ndefu huku kuliwa na mifano mingi.
Mfano mmojawapo maarufu sana ni mfano wa mfalme Suleiman... Mtu huyu katika mazungumzo yake na Mungu (kwa njia ya maono na unabii) aliulizwa anataka nini toka kwa Mwenyezi Mungu... Yeye akaomba hekima...! Wengi wetu leo hii wanaomba utajiri, tembelea yale makanisa ya kileo utaona...!
Mungu akampa mfalme Suleiman HEKIMA kama alivyoomba lakini akaongezewa na utajiri... Inasemekana mpaka leo hii hakuna aliyeweza kumfikia Suleiman kwa utajiri na ukwasi

Laana ndani ya baraka za Suleiman mfalme ni ipi?
Dhambi ya asili... Chini ya jua hakuna kiumbe mkamilifu la hata mmoja... Wote ni watenda dhambi na wamepungukiwa na utukufu wa MUNGU
Pale kati patamu.... Suleiman pamoja na hekima zote na utajiri uliotukuka lakini alikuwa dhaifu mno kwenye swala zima la masukubasi.. Inasemekana alikuwa na wake 300 wa ndoa na masuria (nyumba ndogo) idadi kama hiyo.. Ama pengine kuzidi.... Lakini akaja kumtamani mke wa mjakazi wake.... LAANA! na ili apate kummiliki kikamilifu nadhani alimfanyia mjakazi wake figisu mbaya

Zitumie vema baraka na vipawa vyako, usipotoke na kuanguka mazima... Makinika kila penye baraka kuna laana....

Barikiwa mtumishi
 
Kumbe suleiman alikuwa zaidi ya Bilgert !!!!
 
Mkuu naomba nitagi na mm kwenye ilo andiko la miaka saba nataman sana kulisoma
 
Nani kaiona video ya gwajima.? Nitaweka hapa kwa ruhusa maalum
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom