Kila akitibuana na mke wake lazima akutane na mabalaa

Kila akitibuana na mke wake lazima akutane na mabalaa

Huyu mkuu anatakiwa kusitisha mahusiano ya aina yoyote na huyo mke kama nymb kajenga mke atoke kama amepanga amwachie chumba na vyote vilivyomo aondoke na watoto akaanze maisha mapya na pia hapaswi kuwa na mawasiliano naye kabisa anavyo mtumia pesa anaunganisha mnyororo wa mikosi ya hawara zake atachelewa kupata maendeleo
Kabisaa, mke anakiri kwamba wakikorofishana na mumewe lazima mabalaa yamtokee mumewe ila anadai na yeye hajui kwanini na kamshauri mumewe kama vipi aende kwa Sangoma
 
Mkewe ndio baraka yake.. Awe mpole atafute amani na mke wake, mambo yataenda!
Mkuu,
Walioiona dunia na kufanikiwa kukamilisha uchunguzi wanasema " CHARITY BEGINS AT HOME"
sio kukwaruzana tu hata kama mnaibiana kwa siri kutembea nje tayari balaa zipo ila wengi hawajui.
Mungu alifanya maagano na mwanadamu, alimpa mwanamke mume na mume alimpa mke washirikiane na waheshimu uhusiano huo kwa sababu ni Agano.
 
Hilo liko wazi kabisa, hata mkewe anajua, ila mumewe akimuuliza mkewe kwanini kila inapotokea kutoelewana ndani ya nyumba lazima akutane na majanga anasema hajui. Mume ni mfanyabiashara ya nafaka.

Mara nyingi ikitokea akasafiri pasipokuwa na maelewano na mke wake safari inakuwa ngumu sana, mara apoteze pesa mara apoteze mizigo mara aibiwe mara usumbufu usio wa kawaida kwa watoza ushuru na mambo mengine mengi.

Ni mwezi wa pili sasa tangu mume ahame nyumbani kwake kwa hasira baada kutokea ugomvi mkubwa na mkewe, pesa ya matumizi huwa anatuma lakini mitihani anayopitia ndio kama nilivyoeleza hapo juu.

Msaada wenu tafadhali.
Amludie MUNGU tu Mungu hakumuumba mwanadam aje asafiri na nyota ya mtu mwingne bwana tafakari
Mungu kamuumba mwanadamu ili ategemewe yeye sio aumbe wanadam wategemeane tena haipo hiyo kila mtu ana nafsi yake inayowaza peke yake hata kama wameona kila mtu ana mawazo na na mafikilio yake

Amen
 
Mkewe kicheche sana ugomvi wao huanzia hapo...
Haya maelezo mbona uliyaficha na hukuyaweka kwenye thread ya kwanza ili watu wapate picha halisi na kukupa ushauri kwa mapana yake?

Kama keshaapa kutorudi tena, hakuna haja ya kumshauri. Akomae na msimamo wake tu.
 
Mkewe ndio baraka yake.. Awe mpole atafute amani na mke wake, mambo yataenda!
Huyo sio mke ni agent wa shetani nashauli umuache mara moja ni mchawi. ukirudi kwake anakuua.
 
Mkewe kicheche sana ugomvi wao huanzia hapo,mara ya mwisho mume kazifuma msg za mkewe kwenda kwa mchepuko,ndipo akaamua kuondoka nyumbani kwake na kumwacha mke na watoto wao watatu, na ameapa kutorudi tena, je arudi awe tayari kuvumilia ushenzi wa mkewe kwasabu ya nyota?
Huyu hana nyota bali ni mchawi. bora kufirisika mali kulimo kufirisika nafasi yako katika familia.
 
Hii kitu ndiyo iliyokuwa inaifanya ndoa ya ndugu wangu wa karibu kudumu. Yaani jamaa akimtimua mkewe tuu biashara inayumba vibaya mno. Sasa kuna kipindi mume akahisiwa na uhusiani na house girl. Make akaondoka na mtoto jamaa akaenda kulala kwa mama mkwe mlangoni akisema hatoki mpaka mkewe arudi ilikuwa balaaa......ikabidi mke arudi jamaa alijaza watu kwa kelele mlangoni akimtaka mkewe....lakini wana familia wanajua kuwa it was all abt business mke ana nyota ya biashara lakini asiifanye yeye afanye mume akifanya yeye hapati faida kama akifanya mumewe
 
Unafikiri hii inatokana na nini hasa?
 
wakigombana mkewe huchepuka hivyo uchafu wa zinaa humrudia mumewe, ogopa sana ukisafiri then mkeo agongwegongwe aisee hiyo safari matunda yake hupungua, je nini kinapunguza yaweza kuwa vitu kama hivyo na ajali pia
 
Huyo jamaa ni wewe!.

Fuata ushauri wawadau humu ndani maana kwamaelezoyako unajua vituvingi kuhusu hilo tukio.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom