Kikwete's speech live on TVT

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,556
8,659
..wadau angalieni TVT ndani ya dakika 5..rais anaaza kulkihutubia taifa kwenye sherehe za kuzima mwenge wa uhuru kitaifa arusha ..ilikuwa aanze kuhutubia 10 minutes ago..amemwamuru MC asogeze mbele ili aweze kusoma mawili matatu ya risala ..anajipanga kidogo..nafikiri hataki ku boil tena...kwa hiyo wanaenelea na ngoma ..na wananchi wanaombwa kuwa na utulivu mara rais anapokuja kuhutubia...

capt chiligati waziri wa kazi na vijana anamkaribisha sasa rais aongee na wananchi....

..he seems very careful ..leo anajitahidi kusoma neno hadi neno kwa hutoba aliyoandaliwa....wananchi wanaonekana wako makini sana kumsikiliza as if if wanamtegemea aseme kitu fulani...

still talking on UKIMWI and MADAWA YA KULEVYA....

Wananchi wako kimya na makini sana kupiga makofi..anapokewa na makofi machache tu high table pale anapoahidi kuwahudumia wale wote watakaobainika na ukimwi...

anaongelea MDUDU RUSHWA ..anaongelea namna wanavyoleta reform PCCB kwa kuwapa meno na uwezo wa kufanya kazi ikiwemo budget ,anasema rushwa ndani ya chama ni ruksa kufuatilia...anasema hatawaingilia PCCB NA WASIMUOGOPE MTU...wawe huru..na wakiogopa nitatizo lao si lake.

aanaomba USHIRIKIANO wa wananchi kwa PCB...HAJAGUSIA BUZWAGI..WALA MAWAZIRI ,WALA UFISADI..WANANCHI KIMYA...

Sasa anamalizia hotuba kwa kuongelea AMANI NA UTULIVU kama uridhi wa mwalimu nyerere..anasema vijana wasitumike..na watu wenye maneno matamu..kwani kila kingaracho si dhaabu...anasisitiza hao ni watu wenye UCHU WA MADARAKA,wana TAMAA,wanataka watu WAFE ili wafikie malengo ya kisiasa...

ANASEMA"msitafute uongozi kwa kutumia miili na damu za raia"[mpaka sasa hakuna makofi wala kutoka kwa wananchi]..dhahiri muheshimiwa hapa mwishoni wa hotuba anapowaongelea wapinzani anaonekana kubadilika na kukasirika kidogo....response ya hotuba kwa wananchi pia inawezekana haijamfurahisha tu..wananchi wa arusha always wamekuwa marafiki wake sana lakini leo wanamtazama tu kama sanamu...inamuudhi bila shaka...

anasema wananchi wasiyumbishwe na WASIOITAKIA MEMA TANZANIA...baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura....

anamalizia hotuba kwa kusema ....

MUNGU IBARIKI TANZANIA ....MUNGU IBARIKI AFRIKA ...

AHASANTENI KWA KUNIOSIKILIZA....!!!!

SASA ANAPANDA KWENYE GARI ANAONDOKA[ulinzi ni mkali]

WANANCHI WANABAKI WAMEDUWAAA......

baadaye rais mstaafu ali hassan mwinyi..ambaye katika siku za karibuni amekuwa msaada mkubwa kumsaidia na kumliwaza rais kwa ushauri ataongoza mjadala wa wazi LIVE wa kumuenzi mwalimu....tvt
 
ahsante kwa kutuhabarisha philemon,
inamaana baada ya kuhutubia wananchi hawakupiga makofi hata kidogo?
 
PM, thanks for the pieces. The constitution is on their favour, they will go on stealing the votes, even when the voters 'll vote against them, that is why he is cheecky saying "anasema wananchi wasiyumbishwe na WASIOITAKIA MEMA TANZANIA...baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura...." knowing that they are contolling the ballot boxes; in other words he was saying; as long as we hold the "electoral commission" which will manipulate figures, hata kama wananch watazomea, na hata kama watapiga against, sisi tunajua namna ya kubadilisha in our favour! Kazi bado ipo!!
 
anasema wananchi wasiyumbishwe na WASIOITAKIA MEMA TANZANIA...baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura....
JK anajuaje wapinzani hawaitakii mema Tanzania?

Naamini Watanzania wote wanaitakia mema Tanzania. Tunachotofautiana ni motives zetu kwenye jambo fulani.

Nashukuru bado anasisitiza kuwapa nguvu PCCB, maneno yake aongeze na vitendo kwa kuimarisha sheria ili PCCB wawe na nguvu zaidi.
 
ahsante kwa kutuhabarisha philemon,
inamaana baada ya kuhutubia wananchi hawakupiga makofi hata kidogo?


kasana..ukisoma nyuso za hadhira iliyokuwa pale uwanjani zilikuwa so mixed na butwaa kuanzia kwa viongozi wa jukwaa kuu[ambao labda walikuwa wakiogopa hasira za rais kumshukia yoyote...jamba ambalo halikutokea]..na wananchi waliokuwa wakisubiri rais aseme wanachotaka kukisikia[hatua atakazochokua kwa wala rushwa na hali ya kisiasa ...rais akachagua kugusia hali ya kisiasa in his favor]

hadi mwisho wa hutuba unaweza kusema wananchi wameondoka na maswali ambayo hayana majibu.....nafikiri hii ndio sababu ya hotuba ya rais kutawaliwa na kimya isivyokawaida....

kimya kwenye public speaking ..kinamaanisha KUELEWEKA SANA KWA KUVUTIA HISIA,AU KUTOELEWEKA KABISA KWA KUTOGUSIA MAENEO WATU WANAYOTAKA KUYASIKIA...MASWALI YASIYI NA MAJIBU...
 
Asante sana Phillemon, its very interesting.

Wananchi sasa wanajua wanachokifanya na wanachotakiwa kuambiwa, ukileta maneno matupu yasiyo staili wanakuangalia tu na kukupuuza.
 
Hotba yake nimeiangalia hadi mwisho japo alichelewa sana kufika uwanjani kwani ratiba ilionyesha kuwa shererhe zingeanza saa tano alifika saa saba kasoro robo.

Anajidai kusema kuwa vijana wasiwaunge mkono wanasiasa kwani wanataka kuwatumia kumwaga damu.

huu ni ushahidi kuwa amaanza kugundua kuwa vijana wameanza kuwatosa hao ccm ndio maana leo hotuba nzima iliwalenga vijana.

Pili aliposema kuwa kuna watu hawalitakii mema taifa hili,
1. hivi ni yupi halitakii mema taifa letu kati ya wale wanaosema ukweli na wale wanaoliibia taifa letu.

2. ni yupi anahatarisha amani kama sio yule anayekwenda kusaini mikataba kwa niaba yetu halafu anasaini vituko vya ajabu , buzwagi.

3.vijana , hawa ni kama wale wa wakati wa mwalimu Nyerere, kwani wakoloni nao walianza kutoa haotuba za aina hii kuwa wasiwaunge mkono wapigania haki ila kwa vile watu waliuona ukweli waliamua kumuunga mkono Mwalimu na wenzake.

4.ataweza tuu kuupata uungwaji mkono wa vijana kama ataweza kuwashughulikia wale wote wala rushwa .

Hotuba ya leo alijikita zaidi kwenye kuzungumzia ukimwi na kutoa siri kuwa wanaofadhili ujambazi ni wauzaji wa madawaq ya kulevya, aliuliza swali hili,

je, kwa mtu anayeishi maisha ya kawaida akipewa ama akipata milioni 100 si zinamtosha kuishi maisha yake yote,.

Swali langu kwake hivi wale first eleven walioiba zaidi ya 1.3 trilion wanaenda ama wamezifanyia kitu gani ,

Rais jua kwamba wananchi ndio wenye nchi na wana haki ya kumpa yeyote madaraka ya kuwaongoza, wanaweza kukipa chama chochote kwani wao ndio wenye mamlaka ya mwisho.

Wananchi wa leo wanaona jinsi uchumi unavyoliwa na vigogo huku kila siku wakiimarisha fence zao kwani hawataki hata maskini wasikie harafu ya kile wanachopika ,

Mwalimu ,nyerere angekuwepo leo sijui angeandika kitabu gani , kwani cha mwisho kilikuwa uongozi wetu na hatima ya Tanzania ,je , leo angeandika kuhusu nini.
 
Nashangaa kama hata hajasema wananchi wavumilie MFUMKO WA BEI kwa sababu uchumi umekuwa pasenti bla bla ......! Mwenge hoye!...hata hii pia, labda angepata makofi sana....
 
Nahisi kila mtu kuanzia waandaaji wa hotuba zake na muungwana mwenyewe wamechanganyikiwa.. Ama kweli Slaa kawakamata pabaya!

Jk alivo mtaalamu wa kuuza sura na maneno matamu ambayo humfanya akubalike mbele ya umma leo hii kaanza ishiwa na kukosa mvuto wa kushangiliwa hotuba zake??

Hapa shughuli imeanza si mchezo!
 
JAMANI MIMI Iam worried na JK anakotupeleka! Kweli kabisa, mambo yakiendelea hivi, sioni kama Taifa letu litaendelea kuwa na mshkamano, maana kuna watu wenye nafasi wanajisahau sana, na madhara ni makubwa.

Nilimpigia Kura JK personally, lakini leo ukiniuliza nadhani nitakuwa kama John Edwards wa USA MY VOTE WAS A MISTAKE AND I RENOUNCE IT! Si kwa sababu namchukia raisi wangu, bali nachelea kusema kwamba what he is doing is not in the terms of reference we agreed in 2005 when I elected him!
 
JK akitaka credibility yake irudi kwa wananchi inabidi sio tu kupiga blah blah kwamba anaiimarisha PCCB kwa kuwapa bajeto kubwa bali pia awape uhuru na wasiripoti kwake na badala yake waripoti to either Bunge or Chief Justice. Na baada ya kupewa huo uhuru, PCCB inabidi ianze kwa kumshughulikia MKAPA. This guy is a f#$cken theif, a common freaking thief, kibaka wa kuvishwa tairi na kupigwa moto and he belongs in the gallows. Yeye, mkewe na washirika wake akina Yona. Huyu jamaa inabidi afanyiwe kama Saadam alivyofanyiwa kule Iraq, we need to get rid of him and start afresh. He is the source of all the ills ambazo tunazo hapa Tanzania hii leo na amenichefua zaidi kwa sababu ame betray trust ya Watanzania and worst of all ali-betray trust na love ya Mwalimu Nyerere ambae alimuamini na kumpigia debe ili achukue nchi. His day will come and i hope it is soon.
 
HILI SUALA LA UGUMU WA MAISHA ndilo linalovutia hisia za watu ambao wengi wetu ..tumemuweka madarakani,wananchi wote bila kujali itikadi wanaiona tanzania isiyo na matumaini.

kinachomsaidia rais kupata huruma ya wananchi ni demokrasia ..wananchi wanapiga makelele lakini mwishoni wanakaa kimya wanasema..."ahh lakini tulimshagua wenyewe,sasa tumngoje mwaka 2010".....

kitu kigumu kwa muheshimiwa rais baada ya karibu miaka miwili tu ya utawala wake ni kurudisha imani ya wananchi..ili kuwaridhisha kuwa kweli anaweza kutawala miaka mitano vema..kabla hajafikia kuomba last term tena ya miaka mitano...
 
Haya sasa welcome to the world of spinning....

Hakuna kuspini bali ni kusema ukweli mtupu kutokana na hali halisi kama inavyoonekana machoni mwa Watanzania walio wengi. Huyu jamaa alipata asilimia 80 ya kura za Watanzania katika uchaguzi wa 2005 kwa kutoa ahadi ambazo mpaka sasa ameshindwa kuzitekeleza na wala hakuna dalili ya kufanikiwa kuzitimiza. Watanzania hawaoni dalili yoyote ya ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya wala maisha bora kwa kila Mtanzania. Wanachoona ni kuendelea kutetea maovu, rushwa na ufisadi wa ulioota mizizi ndani ya CCM na siri kali.

Watanzania wanalalamikia upotevu wa $250 millioni katika account ya forex ya BOT, cha kushangaza hakukuwa na uchunguzi mpaka waliposhinikizwa na WB. Wanalalamikia rushwa iliyo wazi katika ununuzi wa rada ya Tanzania, ndege ya Rais, magari ya jeshi na helicopters. Wanalalamikia mkataba wa Richmond, mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania na mingine bado imefanywa siri hadi hii leo. Wanalalamikia ufujaji wa pesa unaofanywa na viongozi wetu wanaotaka kuishi kama Tanzania ni nchi tajiri, mfano ununuzi wa mashangingi ambayo ni magari ya kifahari. Juzi juzi tu tumesikia kwamba kuna baadhi ya mawaziri wanamiliki migodi ya madini na wakati huo huo kuna wananchi waliohamishwa katika maeneo yao yenye dhahabu hadi hii leo hawajalipwa haki wanazostahili baada ya kuhamishwa kwenye makazi yao. Tumesikia jinsi Mkapa na Yona walivyojipatia Kiwira Coal Mining katika mazingira ya kutatanisha na kuwashinikiza TANESCO kusaini mkataba wa shilingi 340 billioni ambao hauna maslahi kwa Watanzania.

Anaonekana hana hoja hivyo kuanza kutisha watu kuhusiana na umwagaji wa damu. Hakuna yeyote anayetaka umwagaji wa damu utokee, bali haki itendeke ili Watanzania waone faida ya rasilimali zao, mafisadi na wala rushwa ambao wana ulafi wa kujilimbikizia mali wafunguliwe mashtaka na pia kufilisiwa mali zote zilizopatikana katika njia za haramu. Watanzania walimwamini kwamba atakuwa mkombozi wao, atakuwa mtetezi wa maslahi ya Watanzania wote, kumbe ni mtetezi wa kundi la watu wachache wanaojiita 'MTANDAO'. Wajiandae kufanya wizi mkubwa sana wa kura hapo 2010 vinginevyo CCM imeshapoteza mwelekeo sio tu watapoteza viti vingi vya wabunge bali pia urais hata kama CCM watamchagua mgombea mwingine hasira za Wananchi katika kila kona ya Tanzania zinazidi kupamba moto.
 
..baada ya kesho rais anaondoka kwenda ITALIA NA UFARANSA kwa zaidi ya siku 8..................[hivi alivyotoka marekani juzi si alifanya stop over ufaransa said kupima afya?? si angemaliza tu na mambo mengine????]
 
..baada ya kesho rais anaondoka kwenda ITALIA NA UFARANSA kwa zaidi ya siku 8..................[hivi alivyotoka marekani juzi si alifanya stop over ufaransa said kupima afya?? si angemaliza tu na mambo mengine????]

nadhani hii ya sasa ni kwenye mkutano flani hivi, na ya juzi kama ulivosema alikwenda kupima afya. Ujue tanzania yenye neema inawezekana, ndio maana kwenda apo ufaransa ni kama mtu kutoka kariakoo kwenda buguruni.....
 
nasikia italy ataonana na wafanyabiashara wa huko.
sijui kwenye ujumbe wake atakuwa na wafanyabiashara pia?
 
Back
Top Bottom