Kikwete yuko Vietnam


Kwa hiyo ingekuwa mwalimu yuko hai angemwambia jamaa "wewe ni mpumbavu!" Kwa vile kila siku viongozi wetu wanasema tuyaenzi maneno ya mwalimu hivyo hili nalo tulienzi? Mie simo!
 
Duh!!! we jamaa kweli huna akili kabisa, hiyo ziara ya Mh. Mbowe ilikuwa ni ya Kiserikali, ya kichama au ya kibinafsi? na je ziara hiyo imegharamiwa na fedha za serikali?

Chagua mwenyewe jibu sahihi...
 
Kwani anaomba kwa ajili ya familia yake msoga?#think wisely

Hapana. Ila ni sawa na kuwa na mke kila siku anaomba mboga kwa jirani ilihali friji imejaa mboga ila ni mvivu wa kupika. Atakuwa anakuaibisha wewe na familia yako.
 

Hii habari ya kuomba umeipata wapi mkuu? Ivi unadhani bila kuwa na wawekezaji wakutosha tutapiga hatua za haraka? Jk anatafuta wawekezaje kwenye sekta muhimu,,china amepata wawekezaji kwenye reli ya kati,,tusubiri na Vietnam atakuja na wawekezaji wa aina gani ili tupige hatua..acheni kubeza kila kitu hizo nchi za asia mashariki hazikuendelea tu hivi hivi...
 
Wanapishana na Mbowe alikuwa hapo Oman kwa sultan anakula bata kwenda mbele.

teh teh teh

Kwa akili yako unaona hili jambo ni siasa! Hapa tunazungumzia kikweta rais wa tanzania, gharama ya safari ya rais si sawa na hata ya waziri, sasa wewe unaleta mambo ya mbowe m/k wa chadema wakati hapa anazungumzia kikwete rais wa tanzania, una akili wewe?
 
hawa jamaa wanasema wanamuenzi Nyerere,Nyerere sera yake ni ujamaaa na kujitegemea wao ni KUTEMBEA NA KUOMBA
 
Hapana. Ila ni sawa na kuwa na mke kila siku anaomba mboga kwa jirani ilihali friji imejaa mboga ila ni mvivu wa kupika. Atakuwa anakuaibisha wewe na familia yako.

Hata kama anaomba kwa ajiri yetu,tumemtuma akaombe?.Kwanini asituulize kwanza kama hili jambo tunalifurahia?.Na mbona akipata ha itishi vyombo vya habari kutuonyesha alicholeta?
 

Halafu Zitto anashangaa uKAWA kufanya mkutano jangwani na kudai ndio walitakiwa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima. Zitto and CCM are pathetic!
 
Mbowe alikuwa South Africa akaunganisha Oman kisha akarudi Dar es Salaa, leo kaenda Hai.

Mbowe anatumia hela yake. Huyo 'baba' yako na wajimba zako wanatumia hela ya walipa kodi. Halafu eti hajui kuwa yeye ndiyo sababu kwa nini Tanzania ni maskini.
 
Na wewe nenda Kenya ukiwa ndugu zakk kama 200 hivi ili umpiku Kikwete maana naona unawasha sana kila ukisiki Rais kasafiri.

Safari zake zina faida ndogo kwa wananchi ambao hawapati mlo wa uhakika kwa siku. Na zinatumia gharama nyingi zisizo za lazima. Sasa kama kwa wakati mmoja kuna misafara ya watu 300 wote kwa gharama za walipa kodi unadhani kwa nini nchi isiwe maskini? Kifupi nchi haina vipaumbele, ni ubinafsi tu ndio umetawala. Yawezekana na wewe ndio miongoni mwa wale waliopo kwenye misafara kila siku hupati muda wa kuona wala kujua kama kuna watanzania wanakosa mahitaji ya kila siku.
 
NASA wangemweka kuwa dereva wa Apolo ili apasue anga vizuri
 
Na wewe nenda Kenya ukiwa ndugu zakk kama 200 hivi ili umpiku Kikwete maana naona unawasha sana kila ukisiki Rais kasafiri.

Kwa mawazo yako, hatuna haki ya kuhoji safari zake?hatuna haki ya kujua safari hizo zina tija kiasi gani kwa watz?unadhani JK anasafiri kwa pesa za nani kama si zetu...sisi ndo walipakodi tunatakiwa kuhoji kila kitu.Hii siyo maisha binafsi ya mtu Tunazungumzia taasisi inayotumia pesa zetu...fikiri kabla ya ku...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…