Kikwete wewe Ulikuwa Rais wa Nchi, come on, Man!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786

Ulikuwa Raisi wa JMTZ, Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama wa nchi hii, kwa kifupi ulikuwa kila kitu hapa TZ na hakuna uamuzi uliofanywa uliogusa nchi bila ya wewe kuridhia na ulikuwa kwenye hiyo nafasi kwa miaka 10, hivyo basi hauhitaji kuprove chochote kwa yoyote yule ndani ya nchi hii, nafasi uliyokuwa nayo ni nadra sana mpaka leo hii kwa zaidi ya miaka 50 ni watu watano (5) TU waliobahatika kuipata!

Hauhitaji tena kupata cheo fulani ili iprove chochote, nakushauri achana na media kama ukiweza hata waambie wasikuandike tena mara sijui Kikwete aula hapa, mara sijui Kikwete aalikwa pale inaleta picha kama kuna kitu unajaribu kuprove, achana na hayo mambo kuwa kama Mzee Mwinyi au Mkapa wamesemwa mangapi lkn hata siku moja hawakujaribu kumjibu mtu yoyote yule kwani wanajua kwamba kuwa Raisi wa nchi ni privilege ambayo wanapewa wachache sana Dunia hii na hao wanaopiga domo kamwe hawawezi kuipata!
 
Kweli kujibizana na Lissu na Kubenea ni kujishushia hadhi..
 
Mkuu Salute,
Umezungumza jambo muhimu sana na lenye akili. JK sasa awe low!
 
Duh, ushauri mzuri na wa haja. Lakini kuna mambo huwezi kukaa kimya, mfano UDA kuuzwa kiutata chini ya utawala wake alafu majamaa yanaibuka na ushahidi wa kampuni binafsi ya mahesabu iliyochunguza uuzwaji huo na kugundua kuwa jina la dogo wa miaka nane ni mmoja wa wakurugenzi. Kukanusha au kukubali hili ni lazima mkuu!
 
Ulikuwa Raisi wa JMTZ, Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama wa nchi hii, kwa kifupi ulikuwa kila kitu hapa TZ na hakuna uamuzi uliofanywa uliogusa nchi bila ya wewe kuridhia na ulikuwa kwenye hiyo nafasi kwa miaka 10, hivyo basi hauhitaji kuprove chochote kwa yoyote yule ndani ya nchi hii, nafasi uliyokuwa nayo ni nadra sana mpaka leo hii kwa zaidi ya miaka 50 ni watu watano (5) TU waliobahatika kuipata!

Hauhitaji tena kupata cheo fulani ili iprove chochote, nakushauri achana na media kama ukiweza hata waambie wasikuandike tena mara sijui Kikwete aula hapa, mara sijui Kikwete aalikwa pale inaleta picha kama kuna kitu unajaribu kuprove, achana na hayo mambo kuwa kama Mzee Mwinyi au Mkapa wamesemwa mangapi lkn hata siku moja hawakujaribu kumjibu mtu yoyote yule kwani wanajua kwamba kuwa Raisi wa nchi ni privilege ambayo wanapewa wachache sana Dunia hii na hao wanaopiga domo kamwe hawawezi kuipata!
Ngoja nikufundishe saikolojia kidogo. Kuna kaka mmoja alikuwa anaishi kwenye nyumba ya urithi self contain. Mazingiri yalikuwa machafu, takataka kila mahali na nyumba ilikuwa chafu bila mpangilio. Siku moja ndugu yake akaja likizo na kwa sababu ilikuwa ni nyumba ya urithi akajiunga kuishi pale. Baada ya mwezi mmoja akawa amefanya usafi, nyumba amepaka rangi na maua kila kona. Kwa kifupi ikapendaza tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Kila kona watu wakawa wanamsifia na kumshangaa yule ndugu yake mchafu. Je, unafikiri yule jamaa mchafu ataishi kwa amani? Jibu ni hapana. Na Kikwete anasumbuliwa na hilo. Anataka ku-prove kuwa hakuwa mzembe kama mnavyodhani.
 
Amejibizana na nani kwani! Hivi yule raisi wa mioyo ya malofa na wapumbavu ameacha kujinyea kwenye kadamnasi?
 
Duh, ushauri mzuri na wa haja. Lakini kuna mambo huwezi kukaa kimya, mfano UDA kuuzwa kiutata chini ya utawala wake alafu majamaa yanaibuka na ushahidi wa kampuni binafsi ya mahesabu iliyochunguza uuzwaji huo na kugundua kuwa jina la dogo wa miaka nane ni mmoja wa wakurugenzi. Kukanusha au kukubali hili ni lazima mkuu!
. Mbona Mkapa alibebeshwa Kiwira akakomaanao mpaka wakanyamaza?. Awe mpole tuu.
 
Kwa aliyoyafanya mpaka kuiacha nchi taabani, katu hatapata utulivu wa nafsi.
 
Back
Top Bottom