Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Ulikuwa Raisi wa JMTZ, Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama wa nchi hii, kwa kifupi ulikuwa kila kitu hapa TZ na hakuna uamuzi uliofanywa uliogusa nchi bila ya wewe kuridhia na ulikuwa kwenye hiyo nafasi kwa miaka 10, hivyo basi hauhitaji kuprove chochote kwa yoyote yule ndani ya nchi hii, nafasi uliyokuwa nayo ni nadra sana mpaka leo hii kwa zaidi ya miaka 50 ni watu watano (5) TU waliobahatika kuipata!
Hauhitaji tena kupata cheo fulani ili iprove chochote, nakushauri achana na media kama ukiweza hata waambie wasikuandike tena mara sijui Kikwete aula hapa, mara sijui Kikwete aalikwa pale inaleta picha kama kuna kitu unajaribu kuprove, achana na hayo mambo kuwa kama Mzee Mwinyi au Mkapa wamesemwa mangapi lkn hata siku moja hawakujaribu kumjibu mtu yoyote yule kwani wanajua kwamba kuwa Raisi wa nchi ni privilege ambayo wanapewa wachache sana Dunia hii na hao wanaopiga domo kamwe hawawezi kuipata!