Kikwete: Waliochochea ukabila ndio wanachochea udini leo...

Kikwete: Waliochochea ukabila ndio wanachochea udini leo...

Status
Not open for further replies.

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
Jamani wana JF

Someni haya asemayo Kikwete sasa kuhusu udini na ukabila kisha mtafakari wenyewe.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


JK: Moto wa dini hautakuwa na mshindi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Oktoba 28, 2012, ameanza ziara ya siku nne kukagua shughuli na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwaambia Watanzania kuwa moto wa dini ambao umeanza kujitokeza katika Tanzania hautakuwa na mshindi.

Rais Kikwete ameanzia ziara yake kwenye Wilaya ya Same ambako amehutubia mkutano wahadhara kwenye eneo la Stendi ya Mabasi ya mjini Same ambapo amewaambia mamia ya wananchi kuwa baada ya watu wasioitakia Tanzania mema kushindwa kuwafarakanisha Watanzania kwa kutumia ukabila sasa wamegeukia dini.

"Kuna watu hawana raha na utulivu na amani ya nchi yetu. Walijaribu kutufarakanisha kwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini. Lakinindugu zangu moto wa dini hautakuwa na wa kuuzima na hautakuwa na mshindi," Rais Kikwete amewaambia wananchi kwenye mkutano huo.

Amewataka Watanzania kuendelea na utulivu wao wa kidini na wakatae kufarakanishwa kwa tofauti za dini.

"Ndugu zangu, siku zote tumekuwa na dini zetu, kila mmoja akiwa na uhuru wake wa kuabudu anachokitaka na kukiamini na kwa namna anavyotaka yeye. Ni muhimu tuendelee kuheshimu tofauti zetu za dini bila kuzigeuza tofauti hizokuwa chimbuko na sababu ya ugomvi."

Rais Kikwete pia amewahakikishia wananchi wa Same kuwa Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji katika maeneo ya wilaya hiyo na wilaya za jirani za Mwanga na Korogwe katika Mkoa wa Tanga.

Amesema kuwa mradi mkubwa wa kusambaza maji katika vijiji 34 katika wilaya hizo kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu utaanza kutekelezwa Februari mwakani. Mradi huo wenye thamani za dola za Marekani bilioni 34 utawahudumia wananchi katika vijiji 14vya Wilaya ya Same na utachukua kiasi cha miezi 18 kukamilika.

Rais Kikwete ataendelea na ziara yake leo, Jumatatu, Oktoba 29, 2012 kwa kuzindua Kiwanda cha Tangawizi kilichoko Mamba Miamba na kufanya mkutano hadhara na wananchi. Baadaye kesho, Rais Kikwete atazindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Asha-Rose Migiro iliyoko Mwanga.

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
29Oktoba, 2012

My Take:
Hivi ni nani aliyekuwa anachochea ukabila kama sio CCM?? Kwahiyo na udini unachochewa na CCM? Je, JK anakishtaki chama chake kwa wananchi???
 
Mwana Mpotevu Hii mbona iko wazi inawalenga CDM moja kwa moja, kwani wao ndio 90% ya viongozi wao wanatoka kaskazini, na sasa wameleta udini chini ya mwamvuli wa kanisa
 
Last edited by a moderator:
When will he stop this bickering and provide leadership? Oooooooooooooooooopsss! My bad! He has never be a leader.
 
Swali alichukua hatua gani kukabiliana na waeneza ukabila???

Amechukua hatua gani dhidi ya waeneza udini???

Kama hajachukua hatua mpaka sasa basi atuambie Rais wa nchi hii ni nani....
 
Message sent and delivered,
WALIOCHOCHEA UKABILA/UKANDA NDIO WANAOENDEKEZA UDINI. BIG UP JK, atleast umeliona tatizo
 
Ndio upeo wa intelijensia ya kikwete....huwa anadanganywa kilasiku yeye ni kusoma tu badala ya kuchunguza,baadae wakishtuka utasikia sleep of tongue.akili ya kuambiwa jumlisha na yako.
 
Hii mbona iko wazi inawalenga CDM moja kwa moja, kwani wao ndio 90% ya viongozi wao wanatoka kaskazini, na sasa wameleta udini chini ya mwamvuli wa kanisa
haya mwana propaganda si ndo kazi yako kupotosha? endeleeni na mchezo wenu lakini hukumu yenu yaja mwaka 2015
 
Acheni hizo yeye kama Rais wa nchi alitakiwa aseme ni kina nani hao Walijaribu kutufarakanishakwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini ili tuwaogope kama CANCER. Tafadhali Rais wetu wewe ni Mkuu na Kiongozi wa Nchi wafichue Bayana hawa watu ili washindwe nia yao hii mbaya ya Hotuba za Chuki kila kukicha.
 
Rais wetu ajifunzi kutokana na makosa.Aliposema wauza madawa ya kulevya anawajua,watu walilalamika mbona hawachukulii hatua zozote. Sasa amekuja na lingine, waliochochea ukabila ndiyo wanaochochea udini leo!!
 
Nchi hii watu wote waimba taarabu, sasa kama rais unayo madaraka ya kuchukua hatua,amebakia kuchana mistari isiyo kuwa na msingi je sisi tusiyo na sauti yoyote kwenye jamii, Mr. president, unakazi kubwa sana mbele yako ya kufanya, hacha blabla, nchi inaingia shimoni!
 
Hivi tulichagueje mtu wa aina hii awe raisi, daa tulilogwa vibaya sana zamani wakati nakua nikajua mtu hadi awe raisi ni lazma awe na uwezo mkubwa sana wa hekima,busaea na kufikiri anachokiongea kumbe ata asie jua anachoingea anaweza kua raisi
 
Ninachompendea rais wangu ni hiki, nae huwa anayaona matatizo kama tunavyo yaona wananchi wake, tofauti tu ni hii, sisi hatuna uwezo wa kuyatatua ila yeye hua anaouwezo lakini hautumii.

Natoa mifano:-
Nape Nnauye ameishawahi kusikika sio mara moja akiwaasa watu wasijuiunge na CDM kwa vile eti CDM ni ya wachagga, mwenyekiti wake alikaa kimyaaaa kabisa akijua ni upepo tu utapita, Radio Imani, vikundi kadhaa vya kiislamu vilifanya mikutano mingi tena hadharani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010, vilisema kwa uwazi kabisa, CDM ni chama cha kidini na Dr. Slaa ni Padre, rais wa wakati huo pamoja na msajiri wa vyama vya siasa walikaa kimyaaaa kabisa.

Twende Igunga, bakwata ikatia timu huko na kuwaasa waislam kutokumchagua mbunge wa CDM (wagombea wote wenye mvuto kumbuka walikua Wakristo pale Igunga) na kuawaelekeza Waislamu wamchague yule mgombea wa CCM, yote hayo serikali ilikaa kimya, mbegu ilipandwa na nyie wenyewe wacha sasa iote na hakika tutavuna hata ambao hatukushiriki kuipanda, ninacho sikitika, wengi mliopanda mbegu hii, wakati wa mavuno wenzetu mnaweza kukimbilia popote, sisi je?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom