Kikwete: Waliochochea ukabila ndio wanachochea udini leo...

Status
Not open for further replies.
ingawa hii haimtoi ktk hao wachochezi.Bado sijui atatuambiaje kuwa Ponda na Farid walikuwa wakihubiri ukabila na ni kabila gani?Sijui hajui mkoa aliochagua kuyasema hayo unamaana kubwa sana kufikisha ujumbe wa ukanda unaohubiriwa na CCM dhidi ya CDM.Kwa paltforma aliyotumia na timing yake ni wazi kuwa yeye ndio alikuwa anakamilisha mahubiri ya ukabila kwa kuongezea udini.Badala afikiri kwanini waislam wenzake ndio wamefanya waliyofanya na posible mahubiri ni kutoka mikitini na CCM yenye ushawishi wa wazee wa kiislam.

Rais asiye na tofauti na waziri wake asiyejua nchi zilizojenga muungano wa tanzania na Kusoma mwaka kwa Kiingereza ni aibu kwa watanzania.

Nadhani CDM wanahitaji sasa mshambulia kama walivyopiga kwa mkapa na Sita.Ili KIkwete awe useless kabisa huku akibaki kuwa rais.
 
Wonders shall never end!:confused:

Kuna uzi niliwahi kuchangia kuwa Tanzania kama nchi ni ajabu jipya la dunia. Hatuna haja ya kuupigia kura mlima kilimanjaro mara ngorongoro au serengeti maana nchi yeneyewe tayari ni one of the new world wonders
 
Swali alichukua hatua gani kukabiliana na waeneza ukabila???

Amechukua hatua gani dhidi ya waeneza udini???

Kama hajachukua hatua mpaka sasa basi atuambie Rais wa nchi hii ni nani....
Nape alishatamka hadharani kwamba hawezi kujiunga na Chadema kwa sababu yeye sio mchaga.Hata kukana aliyosema Nape akikufanyika

Kikwete alipoingia madarakani alisema hatawavumilia viongozi wanaotoa majibu ya mkato lakini leo yeye ndio amekuwa kinara!!
 
Naomba tumuache huyu Mzee sorry huyu kijana wa watu amalize tu kwa amani maana naona hata anachokiongea hakieleweki sasa.
 
Kumbe hata UAMSHO imeanzia kwenye ukabila wa CDM. Hawa watafiti wa IKULU nawapa heko.
 
Moja kwa moja wameguswa CDM kwa sababu wao asilimia kubwa ya viongozi wao ni kutoka kanda ya kaskazini, kanda zingine wanataka wapate kura tu.
 
Udini aliuanzisha yeye mwenyewe kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, alipokuwa akilalamika kuwa kuna udini bila ya kuwa na uthibitisho alikuwa akipalilia makaa kwa wale wote aliokuwa akitaka wamchague kwa kigezo hicho.
 
anajua kuwa wanajiandaa kuandamana ijumaa na alhamis? Ili kuwatoa waislam wenzake waliochoma makanisa na kuiba sadaka?
 
Mantiki ya hii taarifa ni nini na imelengwa kwa nani? Mbona mimi naiona inahang hang tu, kwanini hii isingeandikwa tu na waandishi wa habari wa magazeti waliopo eneo la tukio? Inaelekea kurugenzi ya mawasiliano Ikulu haina cha kuandika hivi sasa hadi itoe taarifa za aina hii?
 
Hii mbona iko wazi inawalenga CDM moja kwa moja, kwani wao ndio 90% ya viongozi wao wanatoka kaskazini, na sasa wameleta udini chini ya mwamvuli wa kanisa

chini yaa mwamvuli wa kanisa ndio kuchoma moto makanisa? mlevi tu huyu mpuuzeni!
 
Preliminary test: CHADEMA suspected
Observation: CHADEMA UDINI elements observed.
Conclusion: Kwenye udini, CHADEMA heavily PRESENT!
 
Message sent and delivered,
WALIOCHOCHEA UKABILA/UKANDA NDIO WANAOENDEKEZA UDINI. BIG UP JK, atleast umeliona tatizo

Pathetic...unashangalia JK kuliona 'tatizo'....wakati 'haoni' jinsi ya kulitatua?! Hatashindwaje kuliona tatizo aliloli'invent' mwenyewe!? Hiyo statement ya ikulu imeonyesha jinsi yeyote anavyokabiliana au hata kujaribu kukabiliana na hilo tatizo?! Tunachotaka ni jinsi gani atalitatua hilo tatizo alilolisababisha mwenyewe, na sio kuliona...halafu mbayuwayu mnashangilia!
 
Hii kurugenzi ya mawasiliano ikulu ni very incompetent. Wanaongelea Dola BILIONI 34, ambazo ni bajeti ya nchi hii kwa miaka kadhaa. Labda walikuwa wanamaanisha Milioni 34.
 
Status
Not open for further replies.
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom