Kikwete: Viongozi tuna matatizo siyo wananchi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,351
33,187
RAIS Jakaya Kikwete amesema Watanzania hawana matatizo katika kulinda amani ya nchi, bali viongozi ndio wenye matatizo yanayohatarisha amani hiyo.

Rais Kikwete aliyasema hayo mjini Kigoma jana katika sherehe za kuhitimisha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2010.

Aalisema katika siku za hivi karibuni kumekuwa na kauli mbalimbali za viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi zinazohatarisha amani ya nchi.

"Watanzania hawana matatizo isipokuwa matatizo yapo kwetu sisi viongozi, ndio wenye matatizo,"alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete aliongeza kuwa, "Tukiwachochea kufanya vurugu watafanya, tukiwachochea kuvunja amani watavunja, tukiwachochea kwa udini na ukabila amani ya nchi itatoweka."

Kikwete aliwataka wanasiasa wenzake kuwapa Watanzania haki zao bila ya kuwabagua kwa makabila, rangi, dini, itikadi zao za kisiasa au maeneo wanayotoka.

"Kuna msemo usemao kuwa kuku mtetea hawiki, akiwika mchinje kwani anafanya uchuro, au kuna wale waislaamu wasemao mwanamke hawezi kuwa imamu. Kwani sisi tunatafuta imamu sisi tunatafuta mbunge hapa, diwani,"alisema Kikwete.

"Tuache siasa kwa siasa, dini kwa dini na kabila kwa kabila na tusiingize ukabila katika siasa kama tunataka tuishi vizuri,"aliongeza rais Kikwete.

Aliwataka Watanzania wasidanganyike na kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa huku akiwataka wanasiasa kuacha kuwadanganya Watanzania badala yake watumie sera za maendeleo kushindana.

"Kwani hatuwezi kupiga kampeni bila ya kudanganya? Tusiwe wanasihasa tuwe wanasiasa, tushindane kwa sera za madaraja, umeme au maji na hayo mingine tuwaachie wananchi wenyewe waamue,"alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisema, "Tukiwadanganya Watanzania na mkakubali kudanganywa, majuto ni mjukuu, mtajuta kwani yatatokea tu, tusijidanganye. Tukitahadharisha wanalalamika, je tusitahadharishe? Unataka tuache damu imwagike?."

"Nyinyi watu wa Kigoma mna mfano mzuri wa madhara ya ukabila na udini kwa sababu mmekuwa mkiishi na wakimbizi. Sasa mnataka Chadema na CCM wakipigana polisi wasije? Hapana hawawezi kuwaacha mkapigana lazima watakuja," alisema Rais Kikwete.

Kuhusu mapambano dhidi ya malaria Rais Kikwete alisema yapo katika hatua nne, ambapo ya kwanza ni kutibu kwa kutumia dawa mseto (ACT), pili kujikinga kwa kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa na tatu kwa kutumia unyunyizaji wa dawa ya kuua mbu majumbani (IRS), ambapo tayari wameanza na mkoa wa Mara.

"Tutanyunyiza dawa nchi nzima katika mikoa na wilaya zote ili kuhakikisha mbu yeyote akiingia ndani ya nyumba anakufa kabla ya kumfikia mwanadamu," alisema Rais Kikwete.

Lakini Rais Kikwete alisema mkakati wao dhidi ya malaria umeenda mbali zaidi kwa kuamua kujenga kiwanda cha dawa ambayo itatumiwa kuwafuata mbu hao katika mazalia yao.

"Tayari fedha zimeshalipwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho. Wenzetu Zanzibar wamefanikiwa sasa mimi ninayetoka Bagamoyo naenda kwa jahazi Zanzibar kama nikishindwa kutokomeza nitakuwa naambukiza malaria Zanzibar,"alisema Kikwete.

Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu ulikuwa na kauli mbiu ya kutokomeza ukimwi, malaria na kufanikisha uchaguzi wa huru, wa amani na salama.

chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Hongera rais kwa mkakati wa kutokomeza maralia maana hili ni tatizo kubwa kwa nchi yetu
 
woga na vurugu ni halisia! Wapinzani kuhisi wataibiwa kura ni halisia! CCM kupata hofu ya upinzani na kuhakikisha watashinda kwa kishindo ni halisia! wananchi kutokuamini matokeo ya uchaguzi ama kuona uchaguzi sio wa haki ni halisia. Sasa, vyama vyote viwe makini! Matokeo lazima yabebe hisia hizi kuhakikisha amani baada ya uchaguzi unapatikana.
 
tatizo ni wewe si yeye, yeye anawakumbusha tuu hasa nyie wakatoliki wa chadema vichwa vigumu

mtabadilisha sana sauti za vilio mwaka huu.....mlianza na sauti ya kwanza,naona mko ya nne na bado zaidi ya week mbili sasa tuwamwage.
yeye ndiye tatizo, anahubiri udini kwa zaidi ya wiki sasa.....!mnaona udini ni kutomchagua Kikwete? mbona tulivyokuwa tunamchagua hamkulia udini? kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu....mbinu hizo chafu za dini na makabila na uzawa ndo ilikuwa silaha ya kikwete kuwashinda wenzake ndani ya ccm 2005...leo hii analia na udini ambao haupo.

watu hawampendi yeye binafsi na sio kwa sababu ya dini yake? mwambieni aendelee kueleza sera asilie na mambo ambayo hayapo.

tunaambiwa damu inshaanza kumwagwa Musoma na Hai....mkuu amekaa kimya anaimba udini tu,na shimbo wake aliyesema yuko timamu kukabiliana amenyamaza bado, au mnafikiri damu ni ya wachichiem ila kwa wanachadema ni maji? be realistic you people!!!

taasisi zake zimeoza, ona yalimkuta mengi juzi na mwanae....ona aliyokumbana nayo askofu Mokiwa,askofu mzima anapelekewa rushwa kavukavu na serikali inanyamaza. nchi hii kuna mtu imemshinda,wenye akili hatuwezi kunyamaza tu lazima tufanye kitu october 31.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema Watanzania hawana matatizo katika kulinda amani ya nchi, bali viongozi ndio wenye matatizo yanayohatarisha amani hiyo.

Rais Kikwete aliyasema hayo mjini Kigoma jana katika sherehe za kuhitimisha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2010.

Aalisema katika siku za hivi karibuni kumekuwa na kauli mbalimbali za viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi zinazohatarisha amani ya nchi.

"Watanzania hawana matatizo isipokuwa matatizo yapo kwetu sisi viongozi, ndio wenye matatizo,"alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete aliongeza kuwa, "Tukiwachochea kufanya vurugu watafanya, tukiwachochea kuvunja amani watavunja, tukiwachochea kwa udini na ukabila amani ya nchi itatoweka."

Kikwete aliwataka wanasiasa wenzake kuwapa Watanzania haki zao bila ya kuwabagua kwa makabila, rangi, dini, itikadi zao za kisiasa au maeneo wanayotoka.

"Kuna msemo usemao kuwa kuku mtetea hawiki, akiwika mchinje kwani anafanya uchuro, au kuna wale waislaamu wasemao mwanamke hawezi kuwa imamu. Kwani sisi tunatafuta imamu sisi tunatafuta mbunge hapa, diwani,"alisema Kikwete.

"Tuache siasa kwa siasa, dini kwa dini na kabila kwa kabila na tusiingize ukabila katika siasa kama tunataka tuishi vizuri,"
aliongeza rais Kikwete.

Aliwataka Watanzania wasidanganyike na kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa huku akiwataka wanasiasa kuacha kuwadanganya Watanzania badala yake watumie sera za maendeleo kushindana.

"Kwani hatuwezi kupiga kampeni bila ya kudanganya? Tusiwe wanasihasa tuwe wanasiasa, tushindane kwa sera za madaraja, umeme au maji na hayo mingine tuwaachie wananchi wenyewe waamue,"alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisema, "Tukiwadanganya Watanzania na mkakubali kudanganywa, majuto ni mjukuu, mtajuta kwani yatatokea tu, tusijidanganye. Tukitahadharisha wanalalamika, je tusitahadharishe? Unataka tuache damu imwagike?."

"Nyinyi watu wa Kigoma mna mfano mzuri wa madhara ya ukabila na udini kwa sababu mmekuwa mkiishi na wakimbizi. Sasa mnataka Chadema na CCM wakipigana polisi wasije? Hapana hawawezi kuwaacha mkapigana lazima watakuja," alisema Rais Kikwete.

Kuhusu mapambano dhidi ya malaria Rais Kikwete alisema yapo katika hatua nne, ambapo ya kwanza ni kutibu kwa kutumia dawa mseto (ACT), pili kujikinga kwa kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa na tatu kwa kutumia unyunyizaji wa dawa ya kuua mbu majumbani (IRS), ambapo tayari wameanza na mkoa wa Mara.

"Tutanyunyiza dawa nchi nzima katika mikoa na wilaya zote ili kuhakikisha mbu yeyote akiingia ndani ya nyumba anakufa kabla ya kumfikia mwanadamu," alisema Rais Kikwete.

Lakini Rais Kikwete alisema mkakati wao dhidi ya malaria umeenda mbali zaidi kwa kuamua kujenga kiwanda cha dawa ambayo itatumiwa kuwafuata mbu hao katika mazalia yao.

"Tayari fedha zimeshalipwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho. Wenzetu Zanzibar wamefanikiwa sasa mimi ninayetoka Bagamoyo naenda kwa jahazi Zanzibar kama nikishindwa kutokomeza nitakuwa naambukiza malaria Zanzibar,"alisema Kikwete.

Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu ulikuwa na kauli mbiu ya kutokomeza ukimwi, malaria na kufanikisha uchaguzi wa huru, wa amani na salama.

chanzo: Gazeti la Mwananchi

Ni kweli aliyoyasema mheshimiwa,, leo nimeunga mono hoja yake.

Mungu Ibariki Tanzania
 
tatizo ni wewe si yeye, yeye anawakumbusha tuu hasa nyie wakatoliki wa chadema vichwa vigumu

teh teh teh duhh mbona hii kali ni chadema tuuuu au umeigeuza kumbe ni CCM maana huko ndiko nako kujua zaidi hata ya Chadema maaaana huku CCM kuna vilaza baraaaa na niwabishi na wenye fitna na unafiki na uchu wa madaraka kupindukia

bora umesema!
 
no ONE lyk JK guys hawa wengine wana uchu na ruzuku tu hakuna chochote,kwanini mfunge macho kuangalia aliyoyafanya jamani??tuwe wakweli huyu mropokaji Slaa hana mpya...
 
Back
Top Bottom