Kikwete ukithubutu; thubutu

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Kikwete kama katika sherehe za mei mosi mwaka huu utaalikwa kama mgeni rasmi, na katika hotuba yako ukathubutu kuzungumzia nyongeza mpya ya mshahara basi huna budi kuthubutu kuwambia wafanyakazi hatima ya pesa zao za DECI.

Ndiyo! Pesa walizopeleka DECI ambazo serikali ilizichukua.

Ni wafanyakazi hawa hawa na waatnzania wengine walikwenda kukopa katika mabenki mbalimbali na kuzipeleka DECI wakitaraji kuvuna. wengine walichukua akiba au pato lao la ziada na kulipeleka DECI.
Serikali mlipojulishwa kuwa DECI ni kama upatu, mkachukua hatua ya kuisimamisha. VEMA.
Lakini mlikuwa na wajibu wa kuzirudisha fedha mikononi mwa wanachama wote wa DECI kila mtu apewe haki yake.

Kwanini hamjawarudishia watanzania pesa zao hadi sasa?

Kwanini mnazivuta siku hadi kesho?

Mabilioni hayo mmeyafanyia nini?


Warudishieni wafanyakazi na watanzania wengine fedha zao "walizopanda" DECI.

Rais Kikwete thubutu sasa kulizungumzia suala la DECI katika hotuba yako ikiwa tu utathubutu kuzungumzia maslahi ya wafanyakazi.
 
''Hiyo sija.... sija..... sija....sijaiweka kwe... kwe.... kwenye ajenda.
 
yaelekea na ww ni majeruhi wa DECI pole sana.

Wewe! Usichokoze watu, watakuvamia. Wengine walitegemea kuporomosha bonge ya majumba kwa mavuno ya DECI, wewe unataka kuleta maumivu.
Mwache Rais ajisemee.
 
Wachungaji wa makanisa si ndo waliwatapeli!? mambo mengine yanafuata taratibu za kisheria.! sasa tuendelee kutapeliwa na babu wa loliondo.!
 
Kikwete hana jeuri ya kupandisha mishahara! Hazina yake haina pesa! wameshindwa ubunifu! na zile ahadi tele katika ilani ya CCM zitatekelezwa na pesa zipi?! na hao viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanafanya negotiation na Maiti maana hana uwezo wa kuleta faraja kwa wafanyakazi?! kwanza aliwatukana sana wakati ule na hakuna siku aliyowaomba msamaha!. Theyare foolish!. wakati wanaomba nyongeza kima cha chini kiwe 350,000 wakati ule mafuta (Petrol/diesel) ilikuwa sh 1500/1600Tsh. Sasa Petrol ni 2000 na zaidi! sijui watataka kima cha chini kiwe 600,000Tsh? wameliwa!!
 
Wachungaji wa makanisa si ndo waliwatapeli!? mambo mengine yanafuata taratibu za kisheria.! sasa tuendelee kutapeliwa na babu wa loliondo.!

Mkuu, wakati taratibu za kisheria zinaendelea kwanini waathirika wasirejeshewe fedha zao? Washitaki waanzilishi wa DECI na si wanachana wa DECI..

Kule "site" wanasema mabilioni ya DECI yametumika kupunguza nakisi ya bajeti ya serikali ya JK. Wengine wanasema kuna watu wamejilipa posho. Na mwingine akasema CCM walitumia kwenye uchaguzi. Sijui lipi ni kweli.

Lakini, hata wakijarudishiwa 2015, je itakuwa katika thamani ya 2010? Au ndiyo itafanana na ya wazee wa East Afric Community?
 
Kikwete hana jeuri ya kupandisha mishahara! Hazina yake haina pesa! wameshindwa ubunifu! na zile ahadi tele katika ilani ya CCM zitatekelezwa na pesa zipi?! na hao viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanafanya negotiation na Maiti maana hana uwezo wa kuleta faraja kwa wafanyakazi?! kwanza aliwatukana sana wakati ule na hakuna siku aliyowaomba msamaha!. They are foolish!. wakati wanaomba nyongeza kima cha chini kiwe 350,000 wakati ule mafuta (Petrol/diesel) ilikuwa sh 1500/1600Tsh. Sasa Petrol ni 2000 na zaidi! sijui watataka kima cha chini kiwe 600,000Tsh? wameliwa!!

Penye nyekundu kuna neno.
 
Tafadhali! Ninajiheshimu, naheshimiwa na ninawaheshimu watu. Pinga mawazo yangu kwa hoja lakini si kunitusi. Naomba, unitake radhi.

Mkuu peleka report abuse kwa mods...huu sio utu kabisa!!nimekerekwa infact
 
Ni kweli Myamahodzo! hapo pana neno. Thanks kwa kuliona.

Mkuu tuko pamoja. Lakini hoja yangu katika hilo ni kuwa hazina ni choka mbofu, utawezaji kuwalipa nyongeza ya mshahara wakati hata wa sasa malipo ni mgorogoro (mgogoro)?
 
Hadi sasa hajaweza kuthubutu kulizungumzia la DECI wala waziri wake hakuna aliyelizungumzia. It had happen and proved that hakuna nyongeza ya mshahara(kwa maana ya mshahara mpya) iliyofanywa na serikali yake. Wamesababisha ongezeko la bei za vitu, wafanyabiashara wakiamini mishahara imepanda. Wananchi wanaumia. Wamewadanganya watumishi wa umma wa kitanzania yeye na Baraza lake. TUCTA need to have a say again concern this kind of cheating.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom