Kikwete: Tunapinga mapinduzi

Kikwete: Tunapinga mapinduzi

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,510
11264897_985217191496946_5495266874619484895_n.jpg

Hivi ni kweli hawa viongozi wetu wana akili kwenye bongo zao? Eti wanapinga mapinduzi ya wajeda hapo BURUNDI. Kwahiyo inamaana wanaunga mkono machafuko yaliyokuwa yanaendelea na kusababisha vifo vya wananchi wa Burundi? Wajeda wameamua kuzima jaribio la uvunjwaji wa sheria uliotaka kufanywa na huyu kijana PIERE.

Kwa njia waliyotumia (MAPINDUZI JAPO HAYARUHUSIWI) lkn imesaidia na wananchi wameshukuru na amani itarejea. lakni namshanga huyu mwenyekiti wa kikao cha jana cha marais kujadili kutokukubali mapinduzi yaliyosaidia kufuta fikra potofu za kutaka kuvunja sheria halali.

Napata mashaka yaliyotokea BURUNDI huenda nasi hapa tujiandae kwa kutokana na usanii unaofanywa na serikali hii wajeda wanaweza kufanya yao kama walivyofanya wajeda wa BURUNDI.
 

Attachments

  • kagame.jpg
    kagame.jpg
    35.2 KB · Views: 2,912
hiiviii KAGAME, MUSEVEN watashauri kitu gani wakati wenyewe nao ndio walewale wavunjaji wakuu wa hizo sheria. MU7 mpaka leo hataki kukutoka madarakani anataka afie hapo. kwahiyo uamuzi wa WAJEDA ni muhimu sana kwa viongozi wasanii kama hawa.
 
Sizani kama kuna kiongozi afrika mwenye akili timamu.sasa huyu nae anaongea nini,au anafikiri hii nchi Ni ya familia yake?
 
Siungi Mkono Kwa Yaliyofanyika Burundi Kwani Najua Wajeda Nao Wakionja Madaraka Inaweza Kuwa Ni Tabia Kwamba Hata Jambo Ambalo Linaweza Kutatuliwa Kwa Njia Ya Mezani Wao Wanaweza Kuchulia Kama Ni Mambo Magumu Ila Kwa Burundi Ni Sahihi Lakiwa Wafanye Haraka Kurejesha Utawala Wa Kidemokrasia
 
Wakimbizi walio sajiliwa kigoma wamefika elf 19 na bado wengine wako Nyarugusu! Sasa kupinga haya Mapinduzi unahitaji uwe fisadi na element za kigaidi! Otherwise haya Mapinduzi ni ya kurejesha amani Burundi sioni tatizo hapo
 
Ameniboa sana alipotoa hotuba yake ya kulaani mapinduzi haya kwa lugha ya KIINGEREZA wakati wanasema wanataka lugha ya kutumika kwa EAC iwe ni kiswahili.
 
wakimbizi walio sajiliwa kigoma wamefika elf 19 na bado wengine wako myarugusu! Sasa kupinga haya mapinduzi unahitaji uwe fisadi na element za kigaidi! Otherwise haya mapinduzi ni ya kurejesha amani burundi sioni tatizo hapo

hao wamekuja kwa kazi maalum ya kusadia chama october 15
 
ameniboa sana alipotoa hotuba yake ya kulaani mapinduzi haya kwa lugha ya kiingereza wakati wanasema wanataka lugha ya kutumika kwa eac iwe ni kiswahili.

aliongea vile ili wakubwa zake waliomtuma kazi wamsikilize anaongea nini
 
Kuhisi siyo dhambi. Yanaweza tokea hata bongo kwa hutuba hile ya mkuu wa kaya nina mashaka. Maana ata dalili za maandalizi ya uchaguzi hayapo.
 
Back
Top Bottom