Kikwete: Sitarajii Urais kutenganishwa na Uenyekiti wa Chama

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,893
2,000
Rias Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amesema hatarajii kuona utaratibu tofauti katika CCM tofauti na ule uliozoeleka

Kawaida ndani ya CCM, Rais ndio huwa Mwenyekiti wa CCM ambapo Rais Kikwete amesema wanafanya hivyo kuepusha migongano inayoweza kutokea kwa mwenyekiti kutofautiana na Rais

Amesema hayo zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuwa na Mkutano Maalumu wa CCM

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Magufuli amefariki Machi 17 kwa ugonjwa wa moyo
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,392
2,000
Kama kuna jambo zuri kabisa kwa Tanzania kutokea ni hili la kutenganisha kofia za rais na mwenyeketi wa chama. Tena hili linafaa kuwa kwenye sheria za vyama vya siasa ili i apply kwa vyama vyote hata huko mbeleni vikija kushika nchi.
 
msomi kutoka znz

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
266
1,000
Shida ni ilele, kitabu ni kile kile kimefunguliwa kurasa mpya tu. Hamtaki mawazo mbadala, mawazo kinzani.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,879
2,000
Kikwete mbona anampigia sana mama apate uenyekiti? Alianza kwa kusema "ukiwa Rais na mwenyekiti wa chama unakuwa na nguvu sana." Bila shaka mama atakuwa mwenyekiti lakini Kwanini Kikwete anapiga kampeni?
 
Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,286
2,000
Rias Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amesema hatarajii kuona utaratibu tofauti katika CCM tofauti na ule uliozoeleka

Kawaida ndani ya CCM, Rais ndio huwa Mwenyekiti wa CCM ambapo Rais Kikwete amesema wanafanya hivyo kuepusha migongano inayoweza kutokea kwa mwenyekiti kutofautiana na Rais

Amesema hayo zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuwa na Mkutano Maalumu wa CCM

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Magufuli amefariki Machi 17 kwa ugonjwa wa moyo
Itakuwaje Mwenyekiti wa CCM akiwa tofuti na Rais?
 
Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,286
2,000
Kikwete mbona anampigia sana mama apate uenyekiti? Alianza kwa kusema "ukiwa rais na mwenyekiti wa chama unakuwa na nguvu sana." Bila shaka mama atakuwa mwenyekiti lakini Kwanini Kikwete anapiga kampeni?
Anaunga mkono juhudi
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
18,167
2,000
Kwa hiyo kuna mjinga anafikri Ccm inaweza kufanya tofauti na ilivyozoeleka?
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,597
2,000
Ukiona minon'gono kama hii inaanza ujue kuna sababu chini ya kapeti, muda utatoa majibu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom