Kikwete: Sina tatizo na uwepo wa Serikali tatu Tanzania!

j.k ni mnafiki ndumilakuwili mkubwa na ndiye anayevuruga mchakato wa katiba!

Wewe ndio mnafik, huo mchakato umevurugika wapi na nini alichokifanya Jakaya Kikwete kukufanya wewe uandike huo utumbo?
 
Kwahiyo ameamua aanze kujirudishia matusi aliyomtukana Jaji Warioba, sasa kwanini akasemee mbali huko?

Una kiwanda cha uongo, hayo matusi yako wapi?

Hivi hamkumsikia Kikwete siku anahutubia bunge kuwa mkitaka Serikali tatu basi ziwe imara?

Nawashangaa sana kwa uongo mnaozuwa.

Magwanda mnajidanganya kuwa kukiwa na serikali tatu mtashika dola? Mawe!
 
JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua.

Inaonekana CCM ni wabishi sana na JK alishaona serikali tatu hazikwepeki.
zamlock
===>Huyo sio mtu wa kumwamini hata siku moja,anayasema hayo kwa wazungu kwa sababu ya njaa,akija huku ameshabadiliki.
 
Last edited by a moderator:
Vyo vyote itakavyo kuwa ila TANGANYIKA muihimu sana.!!!!

Sure, Zanzibar ilitumeza muda mrefu sana. Cha ajabu Shivji juzi ameamua kutoka mhadhara kwa kiwango cha layperson ati Tanganyika ilikuwa mkusanyiko tu wa makabila mbalimbali na bustani ya Waingereza lakini Zanzibar ilikuwa ikijulikana kama nchi miaka 200 kabla ya wakoloni. Profesa uchwara kabisa! Ati kwa sababu Tanganyika ilikuwa mkusanyiko wa makabila mbalimbali haistahili kuwa nchi?
 
kwa mtu mwenye elimu isiyo ya spoon feeding basi suala la serikali tatu hawez kubishana nalo.
Kikwete alijua anaongea na watu wenye akili zao na peo zao, hivyo hakutaka kuonekana mbayuwayu na ndio maana akajibu hivyo.
Alipokuwa na vilaza aliongea yanayoendana na vilaza na ndio maana vigeregere vilikuwa havikauki pale dodoma
 
Sasa wewe ulitaka muungano uvunjike na yeye yupo madarakani?

we sister nimefuatilia post zako nyingi na nnachokiona bado hujawa na fikra huru.
Kuna watu unasubiri wakishasema basi we unafuata nyuma bila hata kufikiria nini kinachofuatia.
Nakufananisha na shabani wa kanjibai.
 
JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua.

Inaonekana CCM ni wabishi sana na JK alishaona serikali tatu hazikwepeki.


Kazi za wanasiasa ni kucheza na akili za wanaowatawala
 
Inavyoonekana watu ama kwa kupotosha au kutojua wanachanganya issues.

Wakati anahutubia bunge la katiba aliweka bayana kwamba wenye wajibu juu ya muundo wa serikali upo kwa wabunge,alichofanya Kikwete ni kutaadharisha juu ya uwezo wa serikali ya tatu bila kuwa na vyanzo vya kuaminika vya mapato yake.

Pale BBC alikuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari, hivyo alichosema pale ni kuwa IKIWA wananchi wataamua serikali tatu ,yeye atakuwa hana njia ye yote ya kuzuia, bali kutekeleza maamuzi ya wanachi. Sasa hapo undulumila kuwili wa Kikwete uko wapi.

haya kasema nani kwenye uzinduzi wa bunge la katiba. "Serikali tatu subirini mimi nikiondoka madarakani"
 
Back
Top Bottom