Kikwete: Sina tatizo na uwepo wa Serikali tatu Tanzania!

Jk anadharau xana,anadhani ulaya ndo anaongea na wasomi huku alikuwa anaongea na mbumbumbu.
 
Jk ni kiongozi wa kisiasa......kati ya sifa inayomjenga mwanasiasa bora ni ile ya wepesi wa kuzisoma alama za nyakati,kwenye hilo nampongeza na inamtofautisha na viongozi wengine waliomtangulia ambao wako tayari kufa na msimamo hata kama hauna manufaa kwake na jamii inayomzunguka!!!!
Mtu kukana alichokisema siku chache zilizopita ndio una mwita mwanasiasa bora
!! Ata mtoto wa chekechea anaweza kufanya hivyo.

Mwanasiasa bora asingeonyesha msimamo wake kwenye bunge la katiba.
 
....napata uchungu sana huyu jamaa anavyovuruga nchi yetu. Kika kukicha anakuja na kauli za kutuchanganya tu kwa maslahi ya chama chake....
 
j.k ni mnafiki ndumilakuwili mkubwa na ndiye anayevuruga mchakato wa katiba!

Wewe ndugu yangu pole sana,ulikuwa wapi?Kikwete ndiye aliyekubali mchakato wa katiba mpya,ni Kikwete ndiye aliyemteua Warioba ambaye ni mwanachama wa CCM,na Warioba ndiye liyekusanya maombi,sasa tatizo la Kikwete li wapi?si angenyamaza na mambo ya katiba mpaka muda wake uishe,si angemchagua mtu ambaye angeweka mawazo ya CCM ndani ya rasimu,ambayo ingedai wananchi wanataka serikali mbili?usimlaumu mtu bila kufikiri,fikiri kwanza,acha uvivu wa fikra!
 
Hii ni tofauti na alichosema kwenye bunge la katiba!

Hakuna tofauti, tatizo wanachadema ikiwa pamoja na wewe hamuelewi neno "demokrasia". Elimu ya uraia inahitajika zaidi.

Kwa kukusaidia ni kwamba alichosema Bungeni ni jinsi yeye anavyoamini kuwa serikali Mbili ndio njia muafaka kwa maendeleo ya watanzania. Alichosema London ni kwamba kama wananchi wataamua serikali tatu, yeye atayakubali maamuzi ya wananchi na atafanya kazi nao kwa maendeleo ya Tanzania. Kiswahili kigumu au demokrasia ni ngumu.

Mfano hai: Uchaguzi mkuu 2010 CHADEMA waliamini kuwa Raisi ajae katika uchaguzi huo atakuwa mtu anayeitwa " Dr Slaa". Lakini wananchi wakasema vinginevyo na kumpeleka ikulu Kijana anayeitw "Kikwete". CHADEMA WAKAsema hawatafanya nae kazi. Ingekuwa kama ndio Slaa amechaguliwa ,Kikwete angepanda jukwaani na kusema nimekubali maamuzi ya wananchi na nitafanya kazi na Slaa. Hivi huu ndio undume la kuwili.

Du CHADEMA mnaniacha hoi. Jamani mtaharibu nchi.
 
JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua.

Inaonekana CCM ni wabishi sana na JK alishaona serikali tatu hazikwepeki.

Duh! umenunua usanii wake? Lakini sivyo alivyoagiza kwenye bunge la Katiba!
 
Huyu jamaa ni mnafiki sana!

Mnafiki ni mtu mwenye kauli mbili tofauti katika makundi mawili tofauti. Kimsingi, mnafiki anapotoa kauli mbili tofauti katika makundi mawili tofauti, huwa ameliona kundi mojawapo kuwa ni kundi la wajinga! Na katika issue hii, JK amewaona Watanzania walioko London, kuwa ndiyo wajinga wasiofuatilia habari za nyumbani kwao, na hivyo ni rahisi kudanganywa!!!! Poleni!!!!!!!
 
JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua.

Inaonekana CCM ni wabishi sana na JK alishaona serikali tatu hazikwepeki.
Hana lolote. Ole wako ufanye ishu na jk. Utaishia kuona mauzauza tu.
 
JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua.

Inaonekana CCM ni wabishi sana na JK alishaona serikali tatu hazikwepeki.

Ni kwel hata mim nimemsikia
 
Nyie ndio wanafiki kwani hamjui wala hamkuelewa alichokisema, acheni upotoshaji.
 
mr wind....jk amesoma upepo,..kuna mtu mmoja kiongoz serikalin aliniambia usimwamin sana jakaya ni kigegeu na huogopa lawama.
 
mnafiki huyo si juz tu katupiga mkwara, shwn kubwa

Huyu ni Rais wetu, ni nembo ya Taifa letu ukimtusi yeye umeitusi Tanzania yetu acha tabia yako sio nzuri heshimu nembo za Taifa letu. Kama mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi ni kweli alikosea sana kuhutubia yale aliyohutubia. Mfano kukataa kwamba mbunge aliyeumwa miez sita mfululizo aendelee kua mbunge hapa alikosea sababu ubunge ni uwakilishi sio ajira, wananchi wanahitaji uwakilishi bungeni hivyo katiba ingeruhusu aondolewe ubunge na nafasi yake achukue yule aliyemfuatia kwa idadi ya kura na huyu mbunge aendelee na matibabu kisha apewe stahiki zake kwa kipindi cha miaka mitano ya ubunge wake itakua ni msaada mkubwa kibinadamu kwake kuliko kuendelea kuwanyima uwakili wananchi. Hilo moja na kitendo ha kusisitiza msimamo wa serikali mbili kwa CCm ni kufuta maana ya bunge la katiba maana kama msimamo ni kwamba tetea hata kama ni kibaya we tetea tu
 
Msimamo wa CC M ni serikali 2 kukubli 3 ni kudefeat purpose kwa huyu mkulu wa nchi ni kweli alikimbia critical questions sababu anajua kule kizazi cha kina Babu kipo kule maswali yangekua magumu sana hivyoo akaamua kukaa kati kwenye mind zao, huyu mkulu ni mwanadiplomasia hasa, ni style ya chura mbele amesimama ukizungua ukimcheki kwa nyuma amekaa
 
Ingekuwa vyema athari za serikali tatu zingeanishwa sambamba na athari za serikali mbili tuone;
Wala hilo sio tatizo, infact JK alikiri bungeni kwamba athari za serikali mbili zipo na akazitaja, japo alidanganya Bunge kwamba "zimebaki kero tatu."

Tatizo ni je, hizo athari, ama "kero," ama matatizo ya serikali mbili suluhisho lake ni nini?

JK kaikandia ripoti ya Tume kwamba tume yenyewe imesema kuna changamoto za serikali tatu ilizozipendekeza na haijatoa "majawabu thabiti." Okay then, "majawabu thabiti" ya matatizo ya serikali mbili ni yepi??? Na kama yapo majawabu, na CCM wanayo majawabu, ni kwa nini hawaja ya apply kwa miaka 50? Matatizo si yapo toka 1964? Na wamekuwa na dola toka 1964?
 
Wewe akili yako bado kabisa,hat mtoto au mwendawazim angesikiliza hotuba ya kikwete angegundua kama huyu anayeongea mbele yake m dumilakuwili.
 
Hakuna tofauti, tatizo wanachadema ikiwa pamoja na wewe hamuelewi neno "demokrasia". Elimu ya uraia inahitajika zaidi.

Kwa kukusaidia ni kwamba alichosema Bungeni ni jinsi yeye anavyoamini kuwa serikali Mbili ndio njia muafaka kwa maendeleo ya watanzania. Alichosema London ni kwamba kama wananchi wataamua serikali tatu, yeye atayakubali maamuzi ya wananchi na atafanya kazi nao kwa maendeleo ya Tanzania. Kiswahili kigumu au demokrasia ni ngumu.

Mfano hai: Uchaguzi mkuu 2010 CHADEMA waliamini kuwa Raisi ajae katika uchaguzi huo atakuwa mtu anayeitwa " Dr Slaa". Lakini wananchi wakasema vinginevyo na kumpeleka ikulu Kijana anayeitw "Kikwete". CHADEMA WAKAsema hawatafanya nae kazi. Ingekuwa kama ndio Slaa amechaguliwa ,Kikwete angepanda jukwaani na kusema nimekubali maamuzi ya wananchi na nitafanya kazi na Slaa. Hivi huu ndio undume la kuwili.

Du CHADEMA mnaniacha hoi. Jamani mtaharibu nchi.

Argument ya watu ni kuwa muda wa kutoa maoni kwake kama raia ulishakwisha. Pili ni kuwa akiwa kama mkuu wa nchi alikuwa na uwezo kuwaita tume na kuwanong'oneza jambo hili musiliweke mapema kabla halijatoka hadharani.Tatu watu wanalalamika kuwa hotuba ilijaa maelelezo ya NEC/ CC, kwamba haikutoa ile inayoitwa kuunganisha wajumbe ili wawe timu moja. Hayo ndo baadhi ya malalamiko jumla ukiwasikiliza watu mbalimbali huko mitaani.
 
Huyu ni Rais wetu, ni nembo ya Taifa letu ukimtusi yeye umeitusi Tanzania yetu acha tabia yako sio nzuri heshimu nembo za Taifa letu. Kama mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi ni kweli alikosea sana kuhutubia yale aliyohutubia. Mfano kukataa kwamba mbunge aliyeumwa miez sita mfululizo aendelee kua mbunge hapa alikosea sababu ubunge ni uwakilishi sio ajira, wananchi wanahitaji uwakilishi bungeni hivyo katiba ingeruhusu aondolewe ubunge na nafasi yake achukue yule aliyemfuatia kwa idadi ya kura na huyu mbunge aendelee na matibabu kisha apewe stahiki zake kwa kipindi cha miaka mitano ya ubunge wake itakua ni msaada mkubwa kibinadamu kwake kuliko kuendelea kuwanyima uwakili wananchi. Hilo moja na kitendo ha kusisitiza msimamo wa serikali mbili kwa CCm ni kufuta maana ya bunge la katiba maana kama msimamo ni kwamba tetea hata kama ni kibaya we tetea tu

Umeongea point kaka. Kutukana siyo jambo jema, tujenge tabia ya kuchangia kistaarab uli kujenga hoja, mh. ndiye mkuu wa nchi, heshima yake apewe, akikosea watu wachangie kwa facts kuwa hapo mh ulikosea, kama ambavyo alivyokoaea mwishoni siku ile ya uzinduz wa Bunge la Katiba.
Mwanzoni mwa hotuba yake ilikuwa ni nzuri, kosa ni pale aliposema serikali 3 hakubaliani nazo, aliposema serikali2 ndo safi, alipoanza kuipa Zanzibar kila ombi lake, na dosari nyingine kwenye ile hotuba!
 
Back
Top Bottom