leo imetangazwa kuwa kikwete amehairisha safari yake ya ughaibuni ili kuhani msiba wa Kanumba.naomba kujua alitaka kwenda wapina kufanya nini,je msiba wa mtu kama kanumba unaweza kumfanya Rais wa nchi kuahirisha safari??je hizi safari za huyu mtu zina manufaa gani kwa taifa kama anapanga kusafiri na kuhairisha ghafla??huyu mtu ana akili au amepewa nguvu nyingi anazo shindwa kudhibiti???
Acheni vurugu, nchi inahitaji fedha ya kutosha kwa sasa kuliko kipindi kingine, kama kuna sehemu ya kzitafuta na zitafutwe tu. Tazama chaguzi ndogo zinavyotugharimu, bunge linakuja kesho tu na bado lile la bajeti, kuna uchaguzi wa arusha unakuja na maeneo mengi. We need enough fund.
Kwa hiyo wewe unafikiri hizo pesa zinaweza patikani nje tuu? Unajua maana ya budget au ni aina gani ya budget inayotumika Tanzania? Nyie ndo mnapigia kura watu kwa kuangalia sura eti nzuri baadala ya uwezo
leo imetangazwa kuwa kikwete amehairisha safari yake ya ughaibuni ili kuhani msiba wa kanumba.naomba kujua alitaka kwenda wapina kufanya nini,je msiba wa mtu kama kanumba unaweza kumfanya rais wa nchi kuahirisha safari??je hizi safari za huyu mtu zina manufaa gani kwa taifa kama anapanga kusafiri na kuhairisha ghafla??huyu mtu ana akili au amepewa nguvu nyingi anazo shindwa kudhibiti???
Acheni vurugu, nchi inahitaji fedha ya kutosha kwa sasa kuliko kipindi kingine, kama kuna sehemu ya kzitafuta na zitafutwe tu. Tazama chaguzi ndogo zinavyotugharimu, bunge linakuja kesho tu na bado lile la bajeti, kuna uchaguzi wa arusha unakuja na maeneo mengi. We need enough fund.
Habari za kusikitisha sana ambazo BC imeweza kuzithibitisha kupitia vyanzo mbalimbali zinapasha kwamba muigizaji Steven Kanumba, amefariki dunia alfajiri hii jijini Dar-es-salaam.
Mpaka hivi sasa haijathibitishwa rasmi chanzo cha kifo cha msanii huyo ambaye alijizolea sifa kibao katika tasnia ya filamu nchini.BC inaendelea kufuatilia.Tunachoweza kuthibitisha hivi sasa ni kwamba ni kweli amefariki na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Muhimbili jijini Dar-es-salaam.
Tutaendelea kuwaleteeni habari kadiri tunavyozipata.
Pumzika Kwa Amani Steven Kanumba. UPDATES: Ni wazi kwamba habari ya msiba wa muigizaji Steven Kanumba imeshtua wengi.Sio tu Kanumba alikuwa muigizaji mwenye kupendwa na wengi hususani kupitia kazi yake ya uigizaji,bali pia alikuwa mhimili muhimu katika maendeleo ya tasnia nzima ya uigizaji wa filamu nchini(Bongo Movies).
Pengine ni mshtuko huo ambao unasababisha kuwepo na maneno mengi mengi tofauti huko mitaani kuhusiana na kilichosababisha kifo cha msanii huyo nguli. Hivi sasa kila mtu anasema lake. Wengine kwa nia nzuri na masikitiko ya dhati na wengine kwa nia mbaya za kuchafuana.Si sahihi.
Wakati maneno mengi yakiendelea kutapakaa mitaani,habari ambazo tumeweza kuzithibitisha kutoka kwa vyanzo ambavyo kwa namna pekee vinaweza kuaminika na huku majibu kamili yakisubiri uchunguzi wa kifo(post-mote-rm),tunachoweza kuthibitisha ni kwamba Steven Kanumba amefariki alfajiri ya leo.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo,kilichotokea ni kwamba Steven alikuwa nyumbani na mtu ambaye inaaminika sasa kwamba wana uhusiano wa kimapenzi.Mtu huyo ni msanii mwingine wa filamu Elizabeth Michael almaarufu kwa jina la Lulu.Walikuwa nyumbani hapo baada ya kutoka katika starehe zao(yasemekana walifika mpaka Maisha Club).Walipokuwa hapo nyumbani pakatokea kutoelewana baina ya wapenzi hao wawili(chanzo inasemekana na simu aliyopokea Lulu kutoka kwa mtu mwingine).Ugomvi huo ukaelekea chumbani.
Mdogo wa marehemu Kanumba,anapasha kwamba wakiwa huko chumbaani waliendelea na malumbano.Baada ya muda Lulu akatoka na kumwambia kwamba Kanumba amedondoka.Alipoingia akakuta ni kweli kadondoka na mara moja akatoka kwenda kumchukua daktari.Aliporudi naye(wakati huo Lulu akawa ameshaondoka),uamuzi wa busara ukawa ni kumkimbiza hospitali.Kwa bahati mbaya,mauti yakawa tayari yameshamkuta.
Mpaka hapo ndipo nadharia(theories) mbalimbali zinapoanza kwamba inawezekana katika ugomvi baina yake na Lulu palitokea kushikana na huenda Kanumba akadondoka na kujigonga mahali.Inasemekana wawili hao wote walikuwa wametumia kinywaji.Pamoja na hayo watu walioshuhudia mwili wa marehemu Kanumba wanasema hakuwa na majeraha yoyote ya wazi wazi kuashiria kuumia.Yawezekana ameumia kwa ndani.Hili litathibitishwa na ripoti kamili ya kifo.
Hivi sasa mitpango na taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwake,Sinza karibu na Vatican Hotel.
leo imetangazwa kuwa kikwete amehairisha safari yake ya ughaibuni ili kuhani msiba wa Kanumba.naomba kujua alitaka kwenda wapina kufanya nini,je msiba wa mtu kama kanumba unaweza kumfanya Rais wa nchi kuahirisha safari??je hizi safari za huyu mtu zina manufaa gani kwa taifa kama anapanga kusafiri na kuhairisha ghafla??huyu mtu ana akili au amepewa nguvu nyingi anazo shindwa kudhibiti???
Kwa hiyo wewe unafikiri hizo pesa zinaweza patikani nje tuu? Unajua maana ya budget au ni aina gani ya budget inayotumika Tanzania? Nyie ndo mnapigia kura watu kwa kuangalia sura eti nzuri baadala ya uwezo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.