Kikwete: Ni mwaka wa Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Ni mwaka wa Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Tofty, Jan 1, 2011.

 1. T

  Tofty JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Source: Mwananchi Newspaper Kikwete: Ni mwaka wa Katiba mpya

  Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya. Katika salamu zake za mwaka mpya kwa Taifa jana, Rais Kikwete alisema "...nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano".

  Alisema jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote vikiwemo vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wote, katika kutoa maoni "wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao".

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwa kufanyiwa maamuzi. "Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika,"alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema lengo la kuandikwa kwa Katiba mpya ni kuiwezesha nchi kuwa na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne na kwamba mchakato huo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kwamba Katiba inayokusudiwa ni ile itakayolipeleka taifa miaka 50 ijayo kwa salama, amani, umoja na kuwepo maendeleo makubwa zaidi.

  "La nne ambalo tulilokubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya Nchi yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye Katiba yetu ya sasa tuliyoachiwa na waasisi wa taifa letu, imeifanyia nchi yetu mambo mengi mazuri na kuifikisha Tanzania na Watanzania hapa tulipo," alisema KIkwete na kuongeza:

  ".....mwaka 2011, nchi yetu inatimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, miaka 47 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na miaka 47 ya Muungano wa nchi zetu mbili. Yapo mabadiliko mengi yaliyotokea katika nyanja mbalimbali za maisha ya nchi yetu na watu wake katika kipindi hiki. Kwa ajili hiyo ni vyema kuwa na Katiba inayoendana na mabadiliko na matakwa na hali ya sasa".

  Alisema ana matumaini kwamba mchakato huo utaendeshwa kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya Tanzania na mazoea yetu ya kujadiliana bila kugombana.

  "Wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na pawepo kuvumiliana kwa hali ya juu pale watu wanapotufautiana kwa mawazo,"alisema Rais Kikwete na kuonya kuwa pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana.

  "Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa,"alisema.

  Alitoa wito kwa Watanzania wenye maoni yao kujiandaa kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huo na kutoa maoni ambayo yatawezesha nchi kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa ya sasa na ya miaka 50 ijayo.

  Tangazo la Rais Kikwete kuhusu kuanza kwa mchakato wa kuandikwa kwa upya kwa Katiba, ni faraja kwa makundi mbalimbali ya kijamii ambayo tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Oktoba 31, 2010 yamekuwa yakitoa wito wa kaundikwa kwa Katiba mpya.

  Moto wa kudai katiba mpya, uliwashwa na Chadema Novemba mwaka jana, baada ya kutangaza kutotambua kura zilizomweka madarakani Rais Kikwete. Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilianza mchakato wa kushikiza kuundwa kwa katiba mpya kwa kususia hotuba ya Rais Kikwete wakati wa akizindua Bunge la Kumi.

  Pia wabunge pamoja na viongozi wa chama hicho walisusia sherehe za kuapishwa kwa Rais. Katika kuendeleza madai hayo, hizi karibuni mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chadema John Mnyika aliwasilisha hoja binafsi kwenye Ofisi za Bunge, hoja iliyokuwa na lengo la kudai katiba mpya.

  Hivi karibuni pia, CUF walifanya maandamano ya kuwasilisha rasimu ya katiba mpya kwa waziri wa Katiba na Sheria. Pia viongozi mbalimbali wastaafu, walipo madarakani wamekuwa wakieleza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

  Miongoni mwa waliojitokeza adharani na kuunga mkono uwepo wa katiba mpya ni pamoja na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye , Jaji Mkuu Mstaafu na Agostino Ramadhani, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu pamoja na waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye aliahidi kumshauri Rais juu ya suala la kuundwa kwa Katiba mpya.

  Madai ya Katiba mpya pia yamewahi kutolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuwa mabaya, akitoa mfano wa mapungufu ya katiba ya sasa kuwa ni rais kupewa madaraka makubwa.

  Lakini akiwa Ikulu kwenye hafla ya kuapishwa Jaji Mkuu Mpya, Mohamed Othman Chande, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Frederick Werema, alisema kuwa haona haja ya kuandikwa katiba mpya badala yake katiba iliyopo, iwekewe viraka.

  “Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa,” alisema Jaji Werema.

  Wakati huohuo, Rais Kikwete ameutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa maadhsimisho ya miaka 50 ya Uhuru ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 9 Desemba, 2011 ambapo kutafanyika sherehe kubwa na za aina yake nchi nzima na wananchi kushirikishwa kikamilifu.

  "Kwa kutambua umuhimu wa aina yake wa maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2011, tumekubaliana na viongozi wenzangu serikalini kuwa tusherehekee siku hiyo kwa uzito unaostahili," alisema.

  Kadhalika Rais alisema jambo jingine ni kufanyika kwa tathmini ya kina ya mafanikio tuliyoyapata na tahmini hizo kuandikwa katika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwa vizazi vijavyo.

  "Vitabu na nyaraka hizo vitakuwa kumbukumbu zenye manufaa makubwa kwa wenzetu watakaokuwepo mwaka 2061 wakati wa kusherehekea miaka 100 ya Uhuru wa Tanzania Bara" alisema na kuongeza kuwa pia yatafanyika maonyesho maalum katika Uwanja wa Maonyesho wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na kote mikoani kwenye viwanja vya maonyesho, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  mimi sidanganyiki.
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red sielewi-anayeelewa anieleweshe jamani?????? Katiba mpya na katiba viraka kwa wakati mmoja?????????????????Au baada ya maoni kukusanyawa (kwa miaka 5) halafu ndipo safari ya kuandkia katiba mpya inaanza na kukamilika baada ya miaka 10 kuanzia sasa???????????? Kama ni hivyo basi huu siyo utashi wa kisiasa!!!!!!!!!!?????????????
   
 4. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo ulitakaje mkuu? Asiongelee kuhusu katiba?
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nami vivyo hivyo.
   
 6. m

  mzambia JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Watu wengine bwana dowans ya nini wkt ag ashafunga jalada. Bora katiba mupya ili hizo nguvu walizonazo saa hizi kufunga mijadala zisiwepo na dowans tutaifufua upya tu mkuu
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Sina imani na JK kabsaaaaaa
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  corporal .... mwaka huu mikutano na mijadala ya katiba itakuwa mingi sana.... wasiwasi wangu ni hilo tumbo lako....utaimudu kweli... unahitaji kupunguza virushwa tumbo lipungue...
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nyie ndio ambao unaonyeshwa jua mchana kweupee , na unaliona then unaulizwa hilo nini unasema huo ni mwezi, Shame on you !
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono mkuu,suala la katiba ndo kila kitu,madudu yote ya kina werema ni sababu ya katiba mbovu tuliyonayo.Tuongeze pressure kwenye issue ya katiba.
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  ohoo, issue iliopo sasa ni dowanas ila mkuu anaanza kuzungumzia katiba! teh teh teh :)
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280

  naskia anaunda kamati itakayoongozwa na mwanasiasa aliyebobea.

  hivi bunge letu kazi yake ni kupewa ma-v8 na posho tu?
   
 13. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kwa vile Waziri Sita aliapa kuwa atahakikisha fedha za walipa kodi hazitalipwa kwa mafisadi wa kampuni tata ya Dowans, tunamwomba atuambie amesalimu amri au bado anajipanga?
   
 14. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya ishughulikiwe na Tume ya kuteuliwa na Bunge kuliko na wawakilishi wengi wa wananchi na wala rais Kikwete asijiingize kutaka kuweka madalali
   
 15. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Ivi ni lazima kuanzisha sredi ata kama huna cha kuandika!
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Shukrani ya Punda mateke?
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jf siku hizi magreat thinker wamekwisha, yaani mtu anaanzisha thread utadhani..................
  Heri ya mwaka mpya
   
 18. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa bunge inaweza ikawa good idea, lakin pia inaweza ikawa ni kitu kibaya sana ukilinganisha wabunge wa CCM ni wengi hivyo kila kura na kila jambo wakiamua linweza tu kupita hata wapinzani wapige makelele. swala la mhimu ni kuwa ni tume huru tu ambayo itashirikisha wadau waina zote.
   
 19. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jana JK Alisema
  Ndugu wananchi;
  Mwaka 2010 haukuwa na utulivu wa kutosha kwa upatikanaji wa umeme. Mara kadhaa kumekuwepo na matukio ya kukatika na mgao wa umeme kutokana na uharibifu wa mitambo ya kuzalisha umeme hasa katika kituo cha Songas na vituo vya TANESCO. Pamoja na hayo tatizo la msingi ni uwezo wa uzalishaji wa umeme kuwa mdogo kuliko mahitaji. Hivyo basi, hitilafu katika mtambo mmoja au kituo kimoja cha kuzalisha umeme huzua tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme kwa nchi nzima.

  Ndugu Wananchi;

  Katika kukabiliana na tatizo hilo miaka mitano iliyopita, TANESCO kwa msaada wa Serikali, imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa MW 145 (MW 100 Ubungo na MW 45 Tegeta) kwa kutumia gesi asilia. Bahati mbaya mpango wa kuzalisha MW 300 kule Mtwara kwa kushirikiana na sekta binafsi, haukufanikiwa baada ya mwekezaji kushindwa kupata fedha kwa sababu ya mgogoro wa masoko ya fedha ya kimataifa. Kama tatizo hilo lisingekuwepo umeme huo ungekuwa unakamilika au kukaribia kutumika hivi sasa.

  Kwa sasa TANESCO ina mipango kadhaa inayoendelea nayo ya kuongeza uzalishaji wa umeme nchini. Kwa msaada wa Serikali ndani ya miezi 12 ijayo, TANESCO itaongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 160, (MW 100 Ubungo kwa kutumia gesi asilia na MW 60 Mwanza kwa kutumia dizeli nzito). Kwa kushirikiana na sekta binafsi pia, ndani ya miezi 36 ijayo TANESCO wanatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vya umeme huko Kinyerezi (MW 240) Somanga Fungu (MW 230) na Mtwara (MW 300). Inatarajiwa pia kwamba katika kipindi hicho mradi wa kuzalisha MW 200 pale Kiwira utakamilika.
   
Loading...