Kikwete ndiye Rais wa maendeleo Tanzania

woyowoyo

Senior Member
Jul 24, 2011
173
12
Rais jakaya mrisho kikwete ndie Rais pekee anayeleta maendeleo yanayoonekana kwa macho katika zote za maendeleo 1. Elimu. ameasisi amejenga kila kata secondari na ameboresha kwa kiasi kikubwa majengo ya shule, leo tunapoöngea watoto wanaoingia secondari leo imeongezeka ukitofautisha na huko nyuma leo watoto wa masikini wanapata fursa yakuendelea mbele. Leo amejenga chuo kikubwa kuliko vyote Afrika mashariki kilicho na uwezo wa kuchukua wanafunzi 40000, leo kuna vyuo vyuo vikuu zaidi ya 40. 2.Afya. amejenga vituo vya afya vingi tembea uone, leo hospitali ya afya muhimbili vitengo vingi mf. kitengo cha upasuaji wa moyo, ameziboresha hospitali za zamani na kuonekana ni za kisasa, mf. maweni kigoma. 3. Barabara. amejenga ba rabara nyingi nyingi mf. mmtwara-Lindi, na leo anaiunganisha kigoma kupitia mmto malagarasi ambapo kutajengwa daraja kubwa na barabara kwa kila upande kilometa 60 Leo yupo anahangaika huku na huku na kule kuhakikisha analimaliza tatizo la umeme ambapo si muda mrefu litakuwa historia, jamani mbona mnajifanya mmetia pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao? mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!!
 
wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati nayo ni maendeleo??? wakinamama wanaofia njiani kutokana na umbali wa vituo vya afya nayo ni maendeleo????????????????
 
Unajua maana ya maendeleo kijana? Go back to your basic development studies course...au ndio kafesti year kanakosubiri kurudi darasani?

Maendeleo yakipimwa kwa vigezo hivyo tu ulivyotaja, basi dunia hii imeendelea kila nchi na hakuna nchi masikini
 
hivi shule za secondary bado hazijafunguliwa jamani. humu jamvini kuna posts za kivulana sana toka kuvuana magamba na kuanzia likizo ya mwezi wa sita kwa wanafunzi...............
 
Usifanye mchezo na hii mboga

12790.jpg
 
Unajua maana ya maendeleo kijana? Go back to your basic development studies course...au ndio kafesti year kanakosubiri kurudi darasani?

Maendeleo yakipimwa kwa vigezo hivyo tu ulivyotaja, basi dunia hii imeendelea kila nchi na hakuna nchi masikini
kajiunga tu tarehe 24/07/2011 so keep an eye on him.
 
Elimu, hivi kumbe yale 'magofu' yasiyo na madirisha wala madawati achilia mbali maabara na wanafunzi wanaolundikwa darasani bila ya kuzingatia pass mark eti tunaangalia quantity sio quality na walimu wa 'vodafasta'..mshajiuliza mnatengeneza Taifa la namna gani kwa jinsi hii..??
 
Rais jakaya mrisho kikwete ndie Rais pekee anayeleta maendeleo yanayoonekana kwa macho katika zote za maendeleo 1. Elimu. ameasisi amejenga kila kata secondari na ameboresha kwa kiasi kikubwa majengo ya shule, leo tunapoöngea watoto wanaoingia secondari leo imeongezeka ukitofautisha na huko nyuma leo watoto wa masikini wanapata fursa yakuendelea mbele. Leo amejenga chuo kikubwa kuliko vyote Afrika mashariki kilicho na uwezo wa kuchukua wanafunzi 40000, leo kuna vyuo vyuo vikuu zaidi ya 40. 2.Afya. amejenga vituo vya afya vingi tembea uone, leo hospitali ya afya muhimbili vitengo vingi mf. kitengo cha upasuaji wa moyo, ameziboresha hospitali za zamani na kuonekana ni za kisasa, mf. maweni kigoma. 3. Barabara. amejenga ba rabara nyingi nyingi mf. mmtwara-Lindi, na leo anaiunganisha kigoma kupitia mmto malagarasi ambapo kutajengwa daraja kubwa na barabara kwa kila upande kilometa 60 Leo yupo anahangaika huku na huku na kule kuhakikisha analimaliza tatizo la umeme ambapo si muda mrefu litakuwa historia, jamani mbona mnajifanya mmetia pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao? mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!!

Duh! Mawingu analeta maendeleo nchini!!! Na wakati huo huo nchi iko gizani Watanzania chungu nzima wanapoteza kazi zao kwa kuwa viwanda vinashindwa kuzalisha chochote kile kutokana na ukosefu wa umeme. Hivi ana haki yoyote huyu zaidi ya kuachia ngazi kwa kushindwa kuiongoza nchi!?
 
Utakuta hata huyu wowo ametokea uswekeni hata maji hamna, barabara anazisikia bombani, umeme wa kibatali, shuleni anakaa chini lakini cha ajabu leo anamsifia kikwete.kweli wtz sijui tumelogwa na nani huruma kweli!
 
Hivi wewe wowowo una maanisha kweli au unamkejeli huyu mcheza kiduku? Kama una maanisha basi wewe lazima utakuwa Ephraim Kibonde tuuuuuu.
 
Kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kinapanda au kinashuka?! Elimu wanayopata ni ya kiwango kinachohitajika au?! Barabara/Madaraja yanayo/zinazo-jengwa ni za kiwango kinachohitajika au?! Fedha zinazotumika kwenye miradi ni sahihi au zimefisadiwa?! Majengo ya vyuo, shule na hizo hospitali ni ya kiwango kinachotakiwa au?! Miradi ya umeme inayowekezwa au iliyopangwa kuwekeza inapelekana na mahitaji ?!

Kama ndugu yangu unaweza kutujibu labda mimi naweza kubadili mtazamo nilionao sasa.
Kumbuka wenzetu mf. congo wapo kwenye mradi wa mw 10,000, ethipia wapo kwenye mradi wa mw 1,975 sisi tupo kwenye "miradi" ya mw 100! Umewahi kujiuliza kwanini tuna miradi mingi sana ya umeme ya umeme wakati tuna vyanzo vya kutufanya tuwe na miradi michache tu mf. stiglers gorge? Tafuta majibu rejea tena na hoja labda tunaweza kuwa wafuasi wa hii serikali na madudu yake.
 
Sijui safari hii atasafiri kwenda nchi gani ila
tunataka atuletee WAWEKEZAJI KWENYE UONGOZI AKIANZIA NA YEYE MWENYE ANATAKIWA ATAWALIWE SASA atuletee WAJERUMANI AU WAINGEREZA angalau tutamwona wa maana mana hao watatudisha enzi za mwalimu nyerere
 
Back
Top Bottom