Kikwete ndiye alisaini mkataba wa madini wa bulyanhulu?

Solomon David

JF-Expert Member
Mar 1, 2009
1,148
16
Kulikuwa na sababu kubwa kabisa kwa TBC kukatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chadema. Sababu hiyo ni kumlinda mgombea wa uraisi kwa tiketi ya ccm - Mheshimiwa Kikwete.

Kwa waliomsikiliza Tundu Lissu, Kikwete alisaini mkataba wa kifisadi wa madini wa bulyanhulu (sijui kama alipata 10 au 20 percent). Na kwa mujibu wa Tundu Lissu, Kikwete anahusika na yote yale yaliyotokea baada ya hilo kampuni la kigaidi la nje kuanza uchimbaji - kufukia wachimbaji wadogo wadogo kule bulyanhulu.

Nilipenda ile part ambayo Tundu Lissu alionesha mkataba ukiwa na sahihi ya Kikwete.

Swali kwa wasemaji wa Kikwete (nakuangalia wewe mheshimiwa Kinana), mtaendelea kukatisha vipindi wa TBC hadi lini?
 
Na Richmond ni yake pia ila wenzie wanamkingia kifua kutunza heshima ya nchi, "from internal sources"
 
Na Richmond ni yake pia ila wenzie wanamkingia kifua kutunza heshima ya nchi, "from internal sources"

Hii ya richmond atadai kuwa ni ya Lowassa ili yaishe. Lakini hayo mengine yana sahihi yake. Yaani anaendelea kula 10 percent hadi leo wakati huo nchi ikifilisika.
 
Hii ya richmond atadai kuwa ni ya Lowassa ili yaishe. Lakini hayo mengine yana sahihi yake. Yaani anaendelea kula 10 percent hadi leo wakati huo nchi ikifilisika.
tumeshaambiwa ufisadi ni dunia nzima, therefore we should expect this
 
Na Richmond ni yake pia ila wenzie wanamkingia kifua kutunza heshima ya nchi, "from internal sources"

Na Kagoda pia! Halafu wanamtumia Tido Mhando kuwasafisha kama alivyoandaa kipindi hovyo cha kumsafisha bwana wake Lowasa. Hivi kweli hapa Tido hakututukana kweli watanzania? @$#&***\@^&!@!
 
Hivi kwa data zote hizi kuna mtu anaweza kusimama for CCM? Labda kama ni kipofu au analipwa na hawa mafisadi!
 
tumeshaambiwa ufisadi ni dunia nzima, therefore we should expect this

Mkuu dunia nzima au Tanzania nzima?
Nenda kafisadi China kama hujaacha shingo kule kiwiliwili kikarudi makondoko kuzikwa..!
 
Back
Top Bottom