PreGE2025 Kikwete: Nchi ni tulivu, mambo safi chini ya Rais Samia

PreGE2025 Kikwete: Nchi ni tulivu, mambo safi chini ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
"Nakupongeza sana kwa kazi kubwa unayoendelea kufanya nchini katika maeneo mbalimbali, katika nyanja mbalimbali. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia na kwa hii ambayo tumeona leo, kwanza kuhusu uwanja wa ndege, uwanja wa ndege wa Msalato umekuwa ni dhima ya viongozi wote waliokutangulia tangu baba wa Taifa, akaja Rais wetu wa pili Mzee Mwinyi, akaja Rais wetu wa tatu Mzee Mkapa, nikaja mie, akaja Ndugu yetu Magufuli.

Jambo hili tumekuwa wote tukilitamani lionekane, lipatikane lakini safari hatua, imekamilika kwenye kipindi chako, tunakupongeza sana. Ndoto ya Viongozi wote waliokutangulia imetimia, hongera sana Mhe. Rais. Kwakweli nami nimepita pale, nimeshangaa shangaa lakini nimefarijika sana kuona mnajenga kiwanja cha kisasa kabisa, kiwanja ambacho kitakuwa na uwezo wa kupokea na kuhudumia ndege ya abiria iliyokuwa kubwa kabisa kuliko zote duniani. Hata uwanja wa ndege wa Dar Es salaam bado haijajengwa uwezo huo kwahiyo hongera sana Mhe. Rais kwa jambo hilo kubwa kwa manufaa ya nchi yetu.

La pili ni barabara hizi za mzunguko. Kwanza inajibu jawabu la tatizo maana siku hizi hata Dodoma kuna msongamano na jawabu la msongamano ni barabara zile za juu kwa juu (interchange) lakini kujenga hizi Ring road, barabara hizi za mzunguko na unaweza ukajenga tu lakini zile zilizojengwa nzuri sana na kama alivyosema waziri wa Ujenzi zinaupendezesha Mji wa Dodoma.

Ile interchange pale Ihumwa, Mtumba, namuomba Mwenyenzi Mungu anijalie kuniweka nami nije kuiona. Kwahiyo Mhe. Rais nikupongeze tena kwa kazi kubwa nzuri unayoendelea kuifanya, nikupongeze unao vijana wazuri, wachapakazi, vijana hodari - wanaiheshimisha serikali unayoiongoza, wanatoa matumaini kwa watanzania. Sisi wazee tuliokwisha staafu utake nini tena, nchi tulivu, mambo yanakwenda vizuri na Rais hayo tunayaona chini ya Uongozi wako, Mungu akujalie."- Rais mstaafu Jakaya Kikwete leo Juni 14, 2025 Jijini Dodoma kwenye Mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Ukisikia rimoti iko msoga ndio ujue ni kweli! Yaani mpaka aibu, jaji mkuu mpya alikuwa mshauri wa JK mambo ya sheria Ikulu.

Jaji mkuu wa mwisho ambaye alianzia utumishi wake mahakamani ni nani? In short mihimili yote inaongozwa na 'waserikali', watu wa usalama wa CCM.
 
1749915627959.png
 
Ukisikia rimoti iko msoga ndio ujue ni kweli! Yaani mpaka aibu, jaji mkuu mpya alikuwa mshauri wa JK mambo ya sheria Ikulu.

Jaji mkuu wa mwisho ambaye alianzia utumishi wake mahakamani ni nani? In short mihimili yote inaongozwa na 'waserikali', watu wa usalama wa CCM.
Huyu Masaju alikua AG pale serikalini ilikua na mabishano ya Kisheria Bungeni na Lisu nilibaki nacheka
 
Back
Top Bottom