Elections 2010 Kikwete naye awatukana CHADEMA?

Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
793
101
Baada ya Mkutano wa Dr.Slaa wa Mwembe yanga ambao umepelekea mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kupitia Chadema kufikishwa kituo cha polisi kwa madai kwamba alitoa lugha ya Matusi,Mgombea Urais huyo wa ccm amejibu mapigo kwakuuita ule Mkutano ulikuwa ni Mkusanyiko wa Majuha.
 
Baada ya Mkutano wa Dr.Slaa wa Mwembe yanga ambao umepelekea mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kupitia Chadema kufikishwa kituo cha polisi kwa madai kwamba alitoa lugha ya Matusi,Mgombea Urais huyo wa ccm amejibu mapigo kwakuuita ule Mkutano ulikuwa ni Mkusanyiko wa Majuha.

It takes one to know one
 
Juha wewe na uk...wako acha kuwaita watu na heshima zao ni majuha. Wewe unaishi mbingu ipi? Usitukanie wazazi wetu,watoto wetu, vijana wetu,wajomba zetu,wakwe zetu etc.. juha wewe na mafisadi waliokulipa pesa uje hapa uwatukane watanzania wanaotetea haki yao. Unajisikia vipi wewe ukiitwa 'juha'
 
mnaona polisi mlivyojiingiza ktk biashara ya ajabu ya ku control speech. mnamweka ndani mgombea wa chadema eti katukana, haya sasa JK naye ametukana kwa kuwaita watu wote walioudhulia mkutano kuwa majuha sasa inabidi mumchukulie kwa sababu watu wote sawa mbele ya sheria na hamutakiwi kutumia kipimo tofauti bali kutumia sheria ileile kumchukulia hatua za kisheria JK. tulishawaonya polisi kuhusu mambo ya ku control kauli zinazotolewa kwenye majukwaa ya siasa, kwanini musiwaache wananchi wenyewe waamue kuwa fulani hafai kwa sababu anatukana na siyo nyie kujiingiza ktk biashara ya ku control speech. kwa maana hamtaiweza kwa maana hawa ni wana siasa.
 
hivi kikwete anajua tafsiri sahihi ya neno juha?nani kati ya hawa ktk chadema yeye anapata uthubutu wa kumwita juha kujilinganisha nanyeye?
je,ni:
  • prof baregu?
  • prof kahigi?
  • dr slaa?
  • dr mkumbo?
  • zitto?
  • mnyika?
  • mrema?
  • mbowe?
  • ndesapesa(ndesamburo)?
  • wanachama wa chadema ambao ni watanzania wenye uthubutu wa kuhoji madudu yake?
nataka kikwete aeleze kwa umma wa watanzania kuwa matusi anayozungumzia yeye toka kkwa chadema ni:
  • kuhoji wizi wa epa?
  • kuitaja kagoda ya rostam?
  • kuhoji mikataba mibovu yya madini?
  • kusema watanzania vijijini wanalala kwenye nyumba za tembe?
  • kuwaeleza watanzania kuwa ikulu ilichota mabilioni yao kutengeneza mabango yake yaliyotawanywa nchi nzima huku yeye akisema afya na elimu bure haviwezekani?
 
101025015201_kikwete_slaa.jpg
 
Juha huona wengine nao kama majuha.....kwa hiyo Kikwete yuko sawa kuwaona Chadema ni genge la majuha, kwani yeye ni juha in the first place!
 
Kama mnavyojua, jana 'muungwana' naye kaamua kuonesha uhodari wake wa kujibu mapigo, baada ya kutukanwa (kwa tafsiri yake na CCM, maana matusi inategemewa na tafsiri ya mtu), yaani mtu unasema umetukanwa nawe unaamua kutukana...hii ni ishara ya uwezo mdogo... maana ujuha kwa tafisri ya mtu mwingine linaweza kuwa 'tusi' pia.

Lakini mbaya zaidi ni kuwa aliyetoa maneno yale ya ajabu ya kumtukana 'muungwana' JK, alikuwa ni mgombea ubunge, kwanini JK aamue kujishusha hadhi na kujibizana na mwanasiasa wa level ya Dickson G'hily (former CCJ assistant secretary)...au lengo lake ni kuendesha propaganda za kuwa CHADEMA ndicho kinachohusika zaidi na si yule mgombea mmoja...kma walivyoandika HABARI LEO; Mkutano wa Slaa watumika kumtukana Kikwete...

Nway tuyaache hayo, jambo moja la ajabu ambalo mpaka ni moja ya strong eviedence kuwa CCM na JK wamejiandaa kuvuruga amani ya nchi kisha watimize malengo ya propaganda zao...KWA NINI JK NA CCM WANAWEZA KU-RESPOND KATIKA ISSUES ZOTE LAKINI HAWATAKI KUZUNGUMZIA HAKI AMBAYE NDIYE MZAZI WA AMANI...KWA NINI HAWATAKI KUZUNGUMZIA GREEN GUARDS NA VITA WANAYOENDESHA?
 
Hahaha,
kikwete katukana, angemwita mkulo amsaidie maana yule babu kwa matusi si mnamjua???
alimtukana mtangazaji wa praise power radio ahsubuhi wakati wa msimu wa bunge....
 
Sasa mbona MAJUHA ni tusi pia...
kama ndivyo ngoma droo, hakuna kushitakiana!
 
Tuiweke ishu ya green guards kwenye headlines za kesho kwenye media ili watanzania wajue kwamba tunapoitaja hiyo platoon ndo inakuja tafsiri kwamba kikwete anatukanwa
 
Ayaseme haya yote Lakini hiyo tarehe 31 tutaonekana hivi hapa chini ili kumchagua tumtakaye
 

Attachments

  • Ny.jpg
    Ny.jpg
    37.3 KB · Views: 72
UJUHA mkubwa zaidi ni kutoweza kuona kwamba Watanzania wamechoshwa sana na utawala uliopo. Kushindwa kusoma alama za nyakati ni ujuha.

Mtu yeyote ambaye ana moja au zaidi ya vilema vifuatavyo ni JUHA:

(1) Kushindwa kuona kwamba baada ya mika 50 ya utawala usioleta maendeleo inabidi kubadilisha chama tawala.

(2) Kushindwa kuona kwamba inawezekana kabisa kubadilisha chama tawala kama Kenya ilivyofanya na kupata faida kubwa.

(3) Kushindwa kuona kwamba mtu anayesema anapigana na mafisadi na huku anapita akiwaambia watuhumiwa wana kesi ndogo tu ambazo watashinda ni laghai.

(4) Kushindwa kuona kwamba Tanzania bila CCM inawezekana, tena itanufaika sana. Ndivyo ilivyokuwa kwa Zambia, Kenya, Ghana etc.

UJUHA mkubwa zaidi ni kudhani wewe ni kipenzi cha watu wakati umeshawachosa ile mbaya.
 
Back
Top Bottom