Kikwete na Magufuli wapishana

Kikwete na Magufuli wapishana

L
Wakimtoa watanzania hawataelewa somo kabisa na hata kama atasimama kwa ticket ya chama chochote atashinda ila najua magu ni kipenzi cha Ben na Ben atamtetea kwa nguvu zote au labda mungu amchukue
Labda wamuue, kwa kweli hapatatosha
maana wakati wengine wanaona urais katika Tanzania ya leo ya kuipokea toka kwa JK ni kujitoa sadaka, wengine wanaona ni zawadi, na ndio maana walikuwa hawaishi kufanya sherehe na karamu za kila aina hata kama ni siku ya ukimwi
 
tulifanya makosa kumpa mkwere inchi,yeye ndio kasababisha ccm imeshindwa dar es salaam ,leo anamlaumu nani yeye alipomkata lowasa mwishoni alifikiri nini ?,magufuli ni jembe ,na atarudisha hadhi ya ccm kwa kufuata sheria na taratibu
RAIS Dk. John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, wameanza kutofautiana hadharani.

Kwa kasi, kutokupepesa macho na kutokumung’unya maneno kwa Rais Dk. Magufuli, wengi walitarajia kwamba siku moja, isiyo na jina, angemwambia Mwenyekiti wake kwamba hapana.

Raia Mwema limeambiwa kwamba siku hiyo ilikwishakutimia, bila shaka ikiwa ni mapema mno, pale kwa mara ya kwanza, hali hiyo ilipojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama chao kilichofanyika kabla ya Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mwezi uliopita.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika Dar es Salaam, Kikwete alieleza kutofurahishwa kwake na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa wakiunga mkono kufanyika kwa uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam uliomwibua Isaya Mwita, kutoka katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba Kikwete alikuwa amepewa taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM na wa jumuiya za chama hicho kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hawakisaidii chama jijini Dar es Salaam.

“ Hivi watu wa serikali au mawaziri ni watu wa namna gani hata wasitii maagizo ya chama chao? Hivi bila CCM nani angekuwa waziri au kiongozi wa serikali. Hii ni tabia ya ajabu sana,” chanzo chetu kilimnukuu Kikwete akisema maneno karibu na hayo.

Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu waliohudhuria mkutano huo, aliliambia gazeti hili kuwa Kikwete alionyesha kukerwa na jambo hilo na alizungumza kwa ukali.

Gazeti hili limeambiwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliotoa lawama nyingi kwa mawaziri wa Magufuli na serikali kwa ujumla ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba.

Sofia mwenyewe anadaiwa kupokea taarifa nyingi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM waliokuwa mstari wa mbele kutaka uchaguzi huo wa Meya usifanyike.

Inaelezwa ya kuwa wakati wajumbe wakiwa kimya baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti Kikwete, Dk. Magufuli aliomba nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti alimruhusu.

Katika maelezo yake, Magufuli ambaye anahudhuria vikao hivyo kwa sababu ya wadhifa wake wa urais, aliwatetea mawaziri wake kwa kufuata sheria na si kuyumbishwa na wanasiasa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesikia maelezo yako kwa makini. Naomba kusema kwamba haya matatizo yaliyopo sasa yalitengenezwa na sisi wenyewe na wengine waliosababisha haya matatizo wako humuhumu.

“Wakati wa Uchaguzi Mkuu, kuna wenzetu walitusaliti wakiwa ndani ya chama. Sasa baada ya chama kushindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya usaliti wao, leo wanataka mawaziri wavunje sheria kulinda usaliti wao.

“Hili kwa kweli Mwenyekiti hatuwezi kulitetea. Kama usaliti ulisababisha UKAWA wakashinda Dar es Salaam, basi tuache nasisi tuonje machungu ya usaliti. Kwa kufanya hivi tutajifunza kuwa usaliti si mzuri.

“Kama mawaziri au watumishi wa serikali watakuwa wanafuata sheria kwenye shughuli zao, mimi nitawatetea. Lakini hatuwezi kuwasema kwa kufuata sheria na kuwaacha wasaliti ambao ndio wametufikisha hapa,” chanzo chetu kilimnukuu Magufuli.

Chanzo: Raia mwema
 
Mbona Magu aliwahi mwenyewe kutaka kujiuzulu kwenye BARAZA LA JK kwa sababu za kutetea magari mazito, JK akamtuma Linda amsihi asiondoke. We viipi!!?
Yes I remember this!
Kuna mtu alinichallenge kuwa Jk angeweza kumwacha Magu ktk baraza, lkn ukweli ni kwamba wasingemwelewa na Magu alikuwaakitaka kujiuzuru nchi ilikuwa inazizima, ni vigumu kujua nini kingetokea lkn mtikisiko serikalini au chamani usingekwepeka
 
Hii habari inaonekana ya kawaida ila nyuma yake kuna image ya mtu inatengenezwa.
Habari huwa haina time limit ila hii tangu imetokea mpaka leo ni kitambo, kuna kitu kumeifanya iwe hivyo.
Lakini pili kwa maoni yangu, mlengwa hasa wa habari hii alikuwa ni Sophia Simba, kwa nini nasema hivyo? Anajulikana wazi alikuwa kambi ya Lowasa, na pamoja na kujifanya anakipenda chama, bado haaminiki kwamba alimtosa Lowasa, hivyo kujifanya ndie anapinga uchaguzi wa meya inaonekana ni unafiki. Pili baada ya Lowasa kutoswa kwa vyoyote hakuwa happy na mteule wa CCM hivyo hata mteule wa CCM hawezi kuwa happy na Simba ata angejikomba vipi. Kwa ufupi kama motion uchaguzi kutorudiwa ingeshikiwa bango kada mwingine ambaye si Simba kuna uwezekano kwamba hata mtazamo.wa Rais ungekuwa tofauti. Hii ni ishara kwamba safari ya Sofia Simba kutoweka kwenye ramani ya siasa za Tanzania imewadia, atakuwa anamalizia kufunga mabegi yake.
 
WANATAKA MAGUFURI AENDESHE NCHI KIJINGA JINGA KAMA WALIVYOFANYA WAO ??
 
RAIS Dk. John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, wameanza kutofautiana hadharani.

Kwa kasi, kutokupepesa macho na kutokumung’unya maneno kwa Rais Dk. Magufuli, wengi walitarajia kwamba siku moja, isiyo na jina, angemwambia Mwenyekiti wake kwamba hapana.

Raia Mwema limeambiwa kwamba siku hiyo ilikwishakutimia, bila shaka ikiwa ni mapema mno, pale kwa mara ya kwanza, hali hiyo ilipojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama chao kilichofanyika kabla ya Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mwezi uliopita.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika Dar es Salaam, Kikwete alieleza kutofurahishwa kwake na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa wakiunga mkono kufanyika kwa uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam uliomwibua Isaya Mwita, kutoka katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba Kikwete alikuwa amepewa taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM na wa jumuiya za chama hicho kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hawakisaidii chama jijini Dar es Salaam.

“ Hivi watu wa serikali au mawaziri ni watu wa namna gani hata wasitii maagizo ya chama chao? Hivi bila CCM nani angekuwa waziri au kiongozi wa serikali. Hii ni tabia ya ajabu sana,” chanzo chetu kilimnukuu Kikwete akisema maneno karibu na hayo.

Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu waliohudhuria mkutano huo, aliliambia gazeti hili kuwa Kikwete alionyesha kukerwa na jambo hilo na alizungumza kwa ukali.

Gazeti hili limeambiwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliotoa lawama nyingi kwa mawaziri wa Magufuli na serikali kwa ujumla ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba.

Sofia mwenyewe anadaiwa kupokea taarifa nyingi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM waliokuwa mstari wa mbele kutaka uchaguzi huo wa Meya usifanyike.

Inaelezwa ya kuwa wakati wajumbe wakiwa kimya baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti Kikwete, Dk. Magufuli aliomba nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti alimruhusu.

Katika maelezo yake, Magufuli ambaye anahudhuria vikao hivyo kwa sababu ya wadhifa wake wa urais, aliwatetea mawaziri wake kwa kufuata sheria na si kuyumbishwa na wanasiasa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesikia maelezo yako kwa makini. Naomba kusema kwamba haya matatizo yaliyopo sasa yalitengenezwa na sisi wenyewe na wengine waliosababisha haya matatizo wako humuhumu.

“Wakati wa Uchaguzi Mkuu, kuna wenzetu walitusaliti wakiwa ndani ya chama. Sasa baada ya chama kushindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya usaliti wao, leo wanataka mawaziri wavunje sheria kulinda usaliti wao.

“Hili kwa kweli Mwenyekiti hatuwezi kulitetea. Kama usaliti ulisababisha UKAWA wakashinda Dar es Salaam, basi tuache nasisi tuonje machungu ya usaliti. Kwa kufanya hivi tutajifunza kuwa usaliti si mzuri.

“Kama mawaziri au watumishi wa serikali watakuwa wanafuata sheria kwenye shughuli zao, mimi nitawatetea. Lakini hatuwezi kuwasema kwa kufuata sheria na kuwaacha wasaliti ambao ndio wametufikisha hapa,” chanzo chetu kilimnukuu Magufuli.

Chanzo: Raia mwema
Na hapo bado ile kofia ya uenyekiti haija fika kwa ngosha,wacha june ifike mkwere lazima atahama nchi
 
Kikwete naye sijui anakuwaje sometimes, badala ya kusimamia haki na sheria anataka kuzuia sauti za wananchi zisiamue? , kiongozi hapaswi kuwa hivyo!
 
More pop corn pleaseeeee............. Tamthiliya ya iris season one ndiyo inaanza
 
Hivi hili gazeti likipigwa ban kwa kuandika uzushi mtasema linaonewa?
 
Huwa nashindwa kabisa kumuelewa Kikwete.Jamani, kalishwa nini na Wazungu?Yaani yeye ni kutetea uovu tu.Nadhani kwa mtu aliye timamu Magufuli alipaswa kupongezwa kwa kazi nzuri anayofanya pamoja na vikwazo vyote anavyowekewa hasa na wana CCM.Ni Kikwete huyu huyu katika sherehe za miaka 39 aliyemsifu JPM na kusema yote anayofanya JPM ndiyo chama iliyoazimia kufanya na yako kwenye ilani ya chama.Nakumbuka siku ile alisoma ilani ya CCM.Lipi baya alilofanya Magufuli kwenye uchaguzi wa Meya Dar es Salaam.Alitaka CDM waporwe ushindi wao?Nini sasa maana ya democrasia?Na lini CCM watajifunza kutokana na makosa yao?

Back
Top Bottom