Kikwete na Magufuli wapishana

Kikwete na Magufuli wapishana

sioni ajabu hapo....kwani ukiona watu wanakubaliana kwa kila jambo basi hapo kuna walakini.

Kuhusu umeya JPM yupo sahihi na hakukuwa tena na choice...ni kama Pilot wa US Air ways alipoamua kuishusha Ndege Mto Hudson.....Air port zote alizokuwa anaongozwa aende zilikuwa mbali na Ndege ipo kwenye mwendo kwenda chini.....labda angekuwa Pilot wa Kibongo ndio angesubiri miujiza.
 
Wote ndio walwale tu maisha ndio yanazidi kua magumu vitu vinapanda bei kwa namna ya kutisha
 
RAIS Dk. John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, wameanza kutofautiana hadharani.

Kwa kasi, kutokupepesa macho na kutokumung’unya maneno kwa Rais Dk. Magufuli, wengi walitarajia kwamba siku moja, isiyo na jina, angemwambia Mwenyekiti wake kwamba hapana.

Raia Mwema limeambiwa kwamba siku hiyo ilikwishakutimia, bila shaka ikiwa ni mapema mno, pale kwa mara ya kwanza, hali hiyo ilipojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama chao kilichofanyika kabla ya Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mwezi uliopita.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika Dar es Salaam, Kikwete alieleza kutofurahishwa kwake na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa wakiunga mkono kufanyika kwa uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam uliomwibua Isaya Mwita, kutoka katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba Kikwete alikuwa amepewa taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM na wa jumuiya za chama hicho kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hawakisaidii chama jijini Dar es Salaam.

“ Hivi watu wa serikali au mawaziri ni watu wa namna gani hata wasitii maagizo ya chama chao? Hivi bila CCM nani angekuwa waziri au kiongozi wa serikali. Hii ni tabia ya ajabu sana,” chanzo chetu kilimnukuu Kikwete akisema maneno karibu na hayo.

Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu waliohudhuria mkutano huo, aliliambia gazeti hili kuwa Kikwete alionyesha kukerwa na jambo hilo na alizungumza kwa ukali.

Gazeti hili limeambiwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliotoa lawama nyingi kwa mawaziri wa Magufuli na serikali kwa ujumla ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba.

Sofia mwenyewe anadaiwa kupokea taarifa nyingi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM waliokuwa mstari wa mbele kutaka uchaguzi huo wa Meya usifanyike.

Inaelezwa ya kuwa wakati wajumbe wakiwa kimya baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti Kikwete, Dk. Magufuli aliomba nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti alimruhusu.

Katika maelezo yake, Magufuli ambaye anahudhuria vikao hivyo kwa sababu ya wadhifa wake wa urais, aliwatetea mawaziri wake kwa kufuata sheria na si kuyumbishwa na wanasiasa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesikia maelezo yako kwa makini. Naomba kusema kwamba haya matatizo yaliyopo sasa yalitengenezwa na sisi wenyewe na wengine waliosababisha haya matatizo wako humuhumu.

“Wakati wa Uchaguzi Mkuu, kuna wenzetu walitusaliti wakiwa ndani ya chama. Sasa baada ya chama kushindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya usaliti wao, leo wanataka mawaziri wavunje sheria kulinda usaliti wao.

“Hili kwa kweli Mwenyekiti hatuwezi kulitetea. Kama usaliti ulisababisha UKAWA wakashinda Dar es Salaam, basi tuache nasisi tuonje machungu ya usaliti. Kwa kufanya hivi tutajifunza kuwa usaliti si mzuri.

“Kama mawaziri au watumishi wa serikali watakuwa wanafuata sheria kwenye shughuli zao, mimi nitawatetea. Lakini hatuwezi kuwasema kwa kufuata sheria na kuwaacha wasaliti ambao ndio wametufikisha hapa,” chanzo chetu kilimnukuu Magufuli.

Chanzo: Raia mwema

Uzuri wa JPM katika mijadala kama hii ni urahisi wake wa kujenga hoja kwa sababu anasimamia UKWELI na ukweli huo unamuweka huru tofauti na kikwete ambaye anajikita zaidi kwenye usanii , ulaghai na mipasho, hawezi kuzishinda hoja za JPM na ndio maana uchaguzi umefanyika na UKAWA wameshinda kama ilivyotarajiwa na wengi.
 
Jk alitaka kutupeleka pabaya sana!Angeleta laana ya Taifa kutokana na tabia yake ya upendeleo,kutokujali na roho ya visasi!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
CCM Mpasuko.jpg
 
Nimejaribu kufuatilia Uzi huu ili nione Lumumba wataegemea kwa Magu au baba lao la usanii nimegundua wako njia panda.
Kama kweli Magi alimjibu hivyo tena kwa ujasiri JK nampongeza sana kwani ndio majibu sahihi alipaswa kumpa.
Ila Magu ashauriwe kuwa kwa vile vikao vya kamati kuu yeye anaenda kama mwalikwa kutokana na cheo chake aanze kuvikacha. Kila kikipangwa naye awe na ratiba nyingine, awaache wapige majungu yao yeye achape kazi na kwenye ujinga awashughulikie.
Tumegundua kuwa Uchaguzi wa mameya wowote ukiokuwa na matatizo chanzo ni uongozi wa juu wa ccm
 
ila ccm wasije wakamfanyia fitina Magu 2020 wamtoe mana sio mbali
 
Kilichobaki amtumbue Ridhiwani kwenye Lugumigate tu.
 
Huyu ndo magufuli baba semaaaaaaa babaaaaaaa wewe ndo rais huyo kikwete hajitambui kwanza in jipu huyo kikwete
 
Sisi tuna angalia maslahi ya Tanzania kwanza
Hayo mengine YA kwao
 
Pumbavu. Unafikiri watu wote ni vichwa butu kama wewe unayeishi kwa kukariri? Mbweha tafuta majuha wenzako.
BAVICHA All stars POVU kedekede! wahi ufipa kuna bakuli la kupaka rangi jengo linapitishwa! Dr CHINJA CHINJA hoi bin Taabani!
 
Mbona Magu aliwahi mwenyewe kutaka kujiuzulu kwenye BARAZA LA JK kwa sababu za kutetea magari mazito, JK akamtuma Linda amsihi asiondoke. We viipi!!?
 
Tatizo humu kila mtu anaweza kuandika chochote anachojisikia. chanzo hicho cha kuaminika kilikuwa wapi siku zote hizo. Story hiyo..
sio lazima chanzo kitoe mambo kesho yake, kuna kuangalia wapi mpenyo mzuri wa kutoa mambo. Hapa wiki zitapita
 
Ila CCM bwana of all the people uyu Sophia Simba nae bado mko nae na analalamikia wenzake wakati yeye wakati wa uchaguzi kundi lao linajulikana.
Simple mathematics uchaguzi mayor wa DSM ilikuwa lazima uende UKAWA unless kama mlitaka fanya kama ya Zenji.JPM aliliona ilo ndo maana akaona maji yafuate mkondo tuu ukiyazuia utasababisha mafuriko
 
Movie linaendelea Magufuli ndo stelingi kubwa la maadui hata ukipga mabomu halifi!Ukawa wako benchi wamebaki kuwa watazamaji tu !
 
ila ccm wasije wakamfanyia fitina Magu 2020 wamtoe mana sio mbali
Wakimtoa watanzania hawataelewa somo kabisa na hata kama atasimama kwa ticket ya chama chochote atashinda ila najua magu ni kipenzi cha Ben na Ben atamtetea kwa nguvu zote au labda mungu amchukue
 
RAIS Dk. John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, wameanza kutofautiana hadharani.

Kwa kasi, kutokupepesa macho na kutokumung’unya maneno kwa Rais Dk. Magufuli, wengi walitarajia kwamba siku moja, isiyo na jina, angemwambia Mwenyekiti wake kwamba hapana.

Raia Mwema limeambiwa kwamba siku hiyo ilikwishakutimia, bila shaka ikiwa ni mapema mno, pale kwa mara ya kwanza, hali hiyo ilipojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama chao kilichofanyika kabla ya Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mwezi uliopita.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika Dar es Salaam, Kikwete alieleza kutofurahishwa kwake na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa wakiunga mkono kufanyika kwa uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam uliomwibua Isaya Mwita, kutoka katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba Kikwete alikuwa amepewa taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM na wa jumuiya za chama hicho kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hawakisaidii chama jijini Dar es Salaam.

“ Hivi watu wa serikali au mawaziri ni watu wa namna gani hata wasitii maagizo ya chama chao? Hivi bila CCM nani angekuwa waziri au kiongozi wa serikali. Hii ni tabia ya ajabu sana,” chanzo chetu kilimnukuu Kikwete akisema maneno karibu na hayo.

Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu waliohudhuria mkutano huo, aliliambia gazeti hili kuwa Kikwete alionyesha kukerwa na jambo hilo na alizungumza kwa ukali.

Gazeti hili limeambiwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliotoa lawama nyingi kwa mawaziri wa Magufuli na serikali kwa ujumla ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba.

Sofia mwenyewe anadaiwa kupokea taarifa nyingi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM waliokuwa mstari wa mbele kutaka uchaguzi huo wa Meya usifanyike.

Inaelezwa ya kuwa wakati wajumbe wakiwa kimya baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti Kikwete, Dk. Magufuli aliomba nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti alimruhusu.

Katika maelezo yake, Magufuli ambaye anahudhuria vikao hivyo kwa sababu ya wadhifa wake wa urais, aliwatetea mawaziri wake kwa kufuata sheria na si kuyumbishwa na wanasiasa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesikia maelezo yako kwa makini. Naomba kusema kwamba haya matatizo yaliyopo sasa yalitengenezwa na sisi wenyewe na wengine waliosababisha haya matatizo wako humuhumu.

“Wakati wa Uchaguzi Mkuu, kuna wenzetu walitusaliti wakiwa ndani ya chama. Sasa baada ya chama kushindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya usaliti wao, leo wanataka mawaziri wavunje sheria kulinda usaliti wao.

“Hili kwa kweli Mwenyekiti hatuwezi kulitetea. Kama usaliti ulisababisha UKAWA wakashinda Dar es Salaam, basi tuache nasisi tuonje machungu ya usaliti. Kwa kufanya hivi tutajifunza kuwa usaliti si mzuri.

“Kama mawaziri au watumishi wa serikali watakuwa wanafuata sheria kwenye shughuli zao, mimi nitawatetea. Lakini hatuwezi kuwasema kwa kufuata sheria na kuwaacha wasaliti ambao ndio wametufikisha hapa,” chanzo chetu kilimnukuu Magufuli.

Chanzo: Raia mwema
majungu.
 
Nimejaribu kufuatilia Uzi huu ili nione Lumumba wataegemea kwa Magu au baba lao la usanii nimegundua wako njia panda.
Kama kweli Magi alimjibu hivyo tena kwa ujasiri JK nampongeza sana kwani ndio majibu sahihi alipaswa kumpa.
Ila Magu ashauriwe kuwa kwa vile vikao vya kamati kuu yeye anaenda kama mwalikwa kutokana na cheo chake aanze kuvikacha. Kila kikipangwa naye awe na ratiba nyingine, awaache wapige majungu yao yeye achape kazi na kwenye ujinga awashughulikie.
Tumegundua kuwa Uchaguzi wa mameya wowote ukiokuwa na matatizo chanzo ni uongozi wa juu wa ccm
Sioni sababu ya Magu kuwakacha, aendelee nao tu na penye ujinga awape live, hawawezi mfanya kitu.
Ukweli ni kuwa JK kwa muda wote wa utawala wake amesuka nyavu za kila aina ya utapeli katika siasa ambazo yeye mwenyewe pekee anaujua msingi wa kutufanyia hivi Watanzania. Sasa hapa anajaribu kufanya mambo ambayo yeye anayainjinia ili mwisho wa siku Magu aonekane mbaya, mnafiki sana. Alivyofaulu kupiga unafki kwa rafiki yake Lowassa amefanya km kamchezo kutaka kumnafikisha kila anayemwona anatakakumharibia kariba yake anayodhani bado anayo, hataki kuona mtu anakuja mbele yake anafanya vitu ambavyo vinawafanya Watanzania waone kuwa walikuwa wakichezewa akili pale wanapouakisi utawala wa JK.
Kwa bahati mbaya pia anajinafikisha ktk namna ambayo anataka aonekane mzuri ktk chama bila kujali tena Watanzania wanaathirikaje na maamuzi yake kutoka chamani, namshukuru rais kwa kuonesha msimamo mapema.
Inasikitisha sana kwa kiongozi kutanguliza maslahi ya chama badala ya Tanzania kwanza.
JK anajiona yeye na makanjanja wenzake ndio wenye chama na chama ndio kila kitu , wananchi baadae.

Hatari nyingine ni kasumba ya viongozi wa vyama kujenga dhana kuwa pale chama kinapofanikisha ushindi kwa mwanachama wake ktk ngazi yyte ya uongozi kinaona kwamba kimempa zawadi huyo mtu, hapo ndio mwanzo wa matatizo yetu makubwa unapoanzia.
Wakati wengine wanaona dhana ya uongozi ni uzalendo unaoongozwa na dhamira ya kutaka kuwasaidia watu kuondokana na matatizo yanayowakabili na kupiga hatua za kimaendeleo, wengine wanaona ni zawadi, hapo usishangae kiongozi wa chama akiwaambia viongozi wa serikali 'kisingekuwa chama wasingepata huo uwaziri na urais' si ajabu kuona watu wanatumia fedha na kila aina ya hila kutaka kupata uongozi, wakati USA wanatumia fedha na mitandao ya watu kupata uongozi kimsingi wanatafuta nafasi kwa dhati ya kuwatumikia watu wao ili kutokana na kazi hiyo wapate heshima yao, ni nafasi ya kutafta heshima na si mali km ilivyo kwa wengi wa viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom