Kikwete na Magufuli wapishana

Kikwete na Magufuli wapishana

Angemtema angeanguka mapema, hakuwa na influence km aliyonayo Magu
Sema hapo magu amekuwa mkweli hakutaka kupepesa macho, wasaliti wanaosemwa ndani ya chama ni huyo madabida , Sophia simba etc, na alichosema magu ni cha maana na muhimu haiwezikani wasaliti waachiwe halafu wale wanaofuata sharia walaumiwe
 
Kulikuwa na mawaziri wachapakazi wazuri tu huko nyuma lakini baada ya kuachwa kwenye mabaraza ya mawaziri wamepotea kabisa,naamini kwa magufuli ingekuwa hivyohivyo
Influence gani ? mbona lowassa alikuwa na influence kubwa kuliko magu lakini aliondolewa uwaziri mkuu, watu(system) wakitaka kukupoteza wanakupoteza tu

Ni mkono wa Mungu,
Lakini nataka niwaambie pia kuwa aina ya siasa za Lowassa na Magu ni vitu viwili tofauti, Labda kwa vile Watanzania hawakuwahi kumfahamu na kushuhudia vizuri utendaji wa Magufuli, jaribu pia kufikiri iwapo CCM ikafika mahala wakamfanyia Magu km kile walimfanyia Thabo Mbeki S.A, kwa sasa nini kitatokea?
Hakuna chama kitathubutu kumkosa, kura atakazopata (ikiwamo ya kwako) za Shein cha mtoto, na CCM itabaki historia
 
Tunangoja Magu achukuwe uwenyekiti mbona tutasikia mengi kuhusu CCM na majipu ya wasaliti. Kwani JK ni mmoja wa wasaliti kwani hakusaidia kumnadi JPM badala yake alikuwa anasafiri kwenda kuaga na kushindwa kutoa ukweli kuhusu Richmond.
 
Sofia Simba si mmoja ya wasaliti mbona bado yupo tu. JK alisema atafukuza wasaliti mbona ameshindwa kuwafukuza. Sasa naamini kazi ya kutumbua majibu inawatu wake si kila mtu anaweza kwani jibu alitumbui jipu.
 
Hawa watu hawajawahi kuwa pamoja siku zote za umaarufu wao. Kumbuka wakati JK alipoingia madarakani alimfanya nini Magufuli. Pamoja na malalamiko kama si maombi anuai ya watu kwamba apewe wizara ya ujenzi ama uwaziri mkuu, ndivyo kasi,ari na nguvu zaidi ya kumdidimiza kwa lengo la kumpotezea kabisa ilivyoshika kasi ingawa jamaa alikomaa kila alikosukumiwa.

Kumrudisha wizara ya miundombinu ilikuwa ni aibu tu kutokana na fedheha zilizokuwa zikifanywa na wateule wa jk.

Kwenye uchaguzi wa mgombea wa ccm kila mtu anajua hata hawa wawili wanajua kwamba JPM hakuwahi kuwa chaguo la Jk hata katika tatu bora hakuwemo. Upepo wa anguko la kishindo la ccm ndio uliomsukumia embe JPM lakini hakuna asiyefahamu kwamba hakuwa mlengwa.

Tofauti zilionekana wazi hata wakati wa kampeni. Morogoro wakati JK akijisifia kwamba amelitoa taifa mbali na hadi kulifikisha hapa kafany akazi kubwa, mgombea uraisi alisimama na Ku crush kwa nguvu kwamba tumefika hapa sababu ya ufisadi tu!.

Anachokifanya JK kwa sasa ni unafiki kama asili ilivyo ili kujaribu kujivalisha kinga ya kutumbuliwa kwake, familia yake na watu wake wa karibu kitu ambacho naona kama kinatoa harufu ya kufanikiwa. Lakini leo ikitokea Mkwere au mmoja wa watu wake akawa raisi, mtaona JPM atakavyofanywa!. Msisahau jamaa anaendeshwa na utashi wa visasi na vinyongo, vikipaliliwa na ubaguzi na upendeleo. Kama Saddam vile!.

Kusema wameanza leo kutofautiana ni kujaribu kufupisha historia kwa kuondoa mizizi.

Filamu ndiyo inaanza. Hapa niutangulizi. Kwa undani zaidi, stay connected!

Ciao!.
Hivi ukiambiwa utoe ushahidi wa hizi porojo zako utaweza? kahawa bwana
 
Sofia simba ndie anaonekana msaliti kwa kuwa alikuwa team Lowasa, na atajuta magu akipewa uenyekiti huo ubunge wake wa kitu maalum ndio mwisho.
 
Sofia Simba si mmoja ya wasaliti mbona bado yupo tu. JK alisema HATAFUKUZA wasaliti mbona ameshindwa kuwafukuza. Sasa naamini kazi ya kutumbua majibu inawatu wake si kila mtu anaweza kwani jibu alitumbui jipu.
=atafukuza
 
Mkuu nakuhakikishia kwa utawala wa awamu ya 4 ulivyokuwa kamwe MKWERE hatakuwa raisi wa nchi hii.
 
Ukiwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa mwenye dola na unafikiri na kutenda sasa na dhamiri yako njema kwa watu wako basi huna la kuhofu hata kidogo.
Hongera rais hongera sana ni maneno ya hekima kwa watu muafaka na kwa wakati muafaka!
Diranqw.
 
Sjakupata mkuu
Ninamaanisha lile zengwe la uchaguzi wa meya dar ungefanyika kama vile Tanga na kuhatarisha amani magufuri ndiye angelaumiwa na si Kikwete pamoja ya kuwa Kikwete kama mwenyekiti wa CCM kwa maneno haya ndiye alikuwa anainjinia ubakaji ule wa demokrasia.
 
JK anachoongea mdomoni ni tofauti na kilichopo mdomoni. Magufuli anaongea yaliyomo moyoni kama alivyo Trump. Magufuli awategemee zaidi Watanzania kuliko CCM. Kwanza hata huo umwenyekiti wa CCM angewaachia tu. CCM imemharibia sana Magufuli kwenye suala la Zanzibar.

Kwa suala la Zanzibar, JK ndiye aliyecheza kwenye matope lakini tope likaja kumwangukia Magufuli.
 
Back
Top Bottom