RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,041
- 510
RAIS Dk. John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, wameanza kutofautiana hadharani.
Kwa kasi, kutokupepesa macho na kutokumung’unya maneno kwa Rais Dk. Magufuli, wengi walitarajia kwamba siku moja, isiyo na jina, angemwambia Mwenyekiti wake kwamba hapana.
Raia Mwema limeambiwa kwamba siku hiyo ilikwishakutimia, bila shaka ikiwa ni mapema mno, pale kwa mara ya kwanza, hali hiyo ilipojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama chao kilichofanyika kabla ya Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mwezi uliopita.
Katika kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika Dar es Salaam, Kikwete alieleza kutofurahishwa kwake na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa wakiunga mkono kufanyika kwa uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam uliomwibua Isaya Mwita, kutoka katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba Kikwete alikuwa amepewa taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM na wa jumuiya za chama hicho kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hawakisaidii chama jijini Dar es Salaam.
“ Hivi watu wa serikali au mawaziri ni watu wa namna gani hata wasitii maagizo ya chama chao? Hivi bila CCM nani angekuwa waziri au kiongozi wa serikali. Hii ni tabia ya ajabu sana,” chanzo chetu kilimnukuu Kikwete akisema maneno karibu na hayo.
Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu waliohudhuria mkutano huo, aliliambia gazeti hili kuwa Kikwete alionyesha kukerwa na jambo hilo na alizungumza kwa ukali.
Gazeti hili limeambiwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliotoa lawama nyingi kwa mawaziri wa Magufuli na serikali kwa ujumla ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba.
Sofia mwenyewe anadaiwa kupokea taarifa nyingi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM waliokuwa mstari wa mbele kutaka uchaguzi huo wa Meya usifanyike.
Inaelezwa ya kuwa wakati wajumbe wakiwa kimya baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti Kikwete, Dk. Magufuli aliomba nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti alimruhusu.
Katika maelezo yake, Magufuli ambaye anahudhuria vikao hivyo kwa sababu ya wadhifa wake wa urais, aliwatetea mawaziri wake kwa kufuata sheria na si kuyumbishwa na wanasiasa.
“Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesikia maelezo yako kwa makini. Naomba kusema kwamba haya matatizo yaliyopo sasa yalitengenezwa na sisi wenyewe na wengine waliosababisha haya matatizo wako humuhumu.
“Wakati wa Uchaguzi Mkuu, kuna wenzetu walitusaliti wakiwa ndani ya chama. Sasa baada ya chama kushindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya usaliti wao, leo wanataka mawaziri wavunje sheria kulinda usaliti wao.
“Hili kwa kweli Mwenyekiti hatuwezi kulitetea. Kama usaliti ulisababisha UKAWA wakashinda Dar es Salaam, basi tuache nasisi tuonje machungu ya usaliti. Kwa kufanya hivi tutajifunza kuwa usaliti si mzuri.
“Kama mawaziri au watumishi wa serikali watakuwa wanafuata sheria kwenye shughuli zao, mimi nitawatetea. Lakini hatuwezi kuwasema kwa kufuata sheria na kuwaacha wasaliti ambao ndio wametufikisha hapa,” chanzo chetu kilimnukuu Magufuli.
Chanzo: Raia mwema