Kikwete na Magufuli wapishana

Kikwete na Magufuli wapishana

Hawa watu hawajawahi kuwa pamoja siku zote za umaarufu wao. Kumbuka wakati JK alipoingia madarakani alimfanya nini Magufuli. Pamoja na malalamiko kama si maombi anuai ya watu kwamba apewe wizara ya ujenzi ama uwaziri mkuu, ndivyo kasi,ari na nguvu zaidi ya kumdidimiza kwa lengo la kumpotezea kabisa ilivyoshika kasi ingawa jamaa alikomaa kila alikosukumiwa.

Kumrudisha wizara ya miundombinu ilikuwa ni aibu tu kutokana na fedheha zilizokuwa zikifanywa na wateule wa jk.

Kwenye uchaguzi wa mgombea wa CCM kila mtu anajua hata hawa wawili wanajua kwamba JPM hakuwahi kuwa chaguo la Jk hata katika tatu bora hakuwemo. Upepo wa anguko la kishindo la CCM ndio uliomsukumia embe JPM lakini hakuna asiyefahamu kwamba hakuwa mlengwa.

Tofauti zilionekana wazi hata wakati wa kampeni. Morogoro wakati JK akijisifia kwamba amelitoa taifa mbali na hadi kulifikisha hapa kafany akazi kubwa, mgombea uraisi alisimama na kucrush kwa nguvu kwamba tumefika hapa sababu ya ufisadi tu!.

Anachokifanya JK kwa sasa ni unafiki kama asili ilivyo ili kujaribu kujivalisha kinga ya kutumbuliwa kwake, familia yake na watu wake wa karibu kitu ambacho naona kama kinatoa harufu ya kufanikiwa. Lakini leo ikitokea Mkwere au mmoja wa watu wake akawa raisi, mtaona JPM atakavyofanywa!. Msisahau jamaa anaendeshwa na utashi wa visasi na vinyongo, vikipaliliwa na ubaguzi na upendeleo. Kama Saddam vile!.

Kusema wameanza leo kutofautiana ni kujaribu kufupisha historia kwa kuondoa mizizi.

Filamu ndiyo inaanza. Hapa niutangulizi. Kwa undani zaidi, stay connected!

Ciao!.
na wewe ndio???
 
Hii mada inashtua mioyo kwa vile kila mtu mwenye akili ya wastani anajua kuwa watu hawa wawili hawafanani kabisa kisiasa na kiutawala. Kuna siku watatofautiana hadharani kweupee na haitakuwa poa. Kwa hiyo suluhisho ni JK kuachia uenyekiti tu mapema akiwa bado anaheshimika kabla self-control ya JPM haijaisha.

[Mafahali wawili hawakai zizi moja]
Binafsi sioni km ni swala la mafahari wawili bali mkweli na mnafiki pia ni bora wabaki hivyo ili tuendelee kujua rangi halisi za watu wa juu ndani ya ccm
 
Hii habari imekuzwa tu lakini kwa anayefuatilia vikao vya CCM, Kikwete kuwa challenged kwenye vikao vya CCM wala sio jambo la kustaabisha na wengine ambao wamekuwa wakim-challenge ni watu wa kawaida tu! Na uzuri wake ni kwamba, mara zote anakuwa tayari kuwa challenged hata na wajinga wajinga let alone JPM ambae ni rais.

Huyo JPM mwenyewe kashika bendera ya CCM baada ya JK kuwa ameshakula vitasa vya kutosha kutoka ndani ya vikao vya CCM tena toka kwa wapuuzi puuzi tu kama akina Nchimbi!

Na naweza kusema uimara wa CCM ulitokana sana na hii tabia ya JK ya kuwaacha watu wa - blow out their anger kwa sababu, jinsi mwanadamu alivyo; hata kama alikuwa ameghadhibika namna gani; ukimwacha a-blow out his/her anger; anatulia! JPM nae anatakiwa kuchukuwa hii leadership style akidhakuwa Mwenyekiti kv kuongoza vikao vya CCM ni kazi ngumu mara tano ya kuongoza vikao vya Baraza la Mawaziri.
 
Mapovu yanakutoka kwa chuki binafsi ulizonazo kwa Kikwete huna lolote,kwa vyovyote iwavyo juwa kuwa alipofikia Magufuli Kikwete ana mchango kwani kama angehamua kumtema kwenye baraza la mawaziri isingeshindikana eti kwa kulikuwa na hizo kelele za watu kutaka apewe uwaziri

Juha wewe Kikwete ana mchango gani kwenye Nchi hii zaidi ya kutuibia watanzania? Katuibia na familia yake yote, mtoto, mjukuu, shangani, shemeji, hawara, binamu, mchepuko wote wametuibia kupitia serikali yetu.

Kwanza huwa tunafanya makosa sana watanzania kuwapa nchi Wazaramo au Wakwere kwasababu wanachokiweza wao ni kucheza ngoma tu na kusalandia wanawake basi.
 
Hawa watu hawajawahi kuwa pamoja siku zote za umaarufu wao. Kumbuka wakati JK alipoingia madarakani alimfanya nini Magufuli. Pamoja na malalamiko kama si maombi anuai ya watu kwamba apewe wizara ya ujenzi ama uwaziri mkuu, ndivyo kasi,ari na nguvu zaidi ya kumdidimiza kwa lengo la kumpotezea kabisa ilivyoshika kasi ingawa jamaa alikomaa kila alikosukumiwa.

Kumrudisha wizara ya miundombinu ilikuwa ni aibu tu kutokana na fedheha zilizokuwa zikifanywa na wateule wa jk.

Kwenye uchaguzi wa mgombea wa CCM kila mtu anajua hata hawa wawili wanajua kwamba JPM hakuwahi kuwa chaguo la Jk hata katika tatu bora hakuwemo. Upepo wa anguko la kishindo la CCM ndio uliomsukumia embe JPM lakini hakuna asiyefahamu kwamba hakuwa mlengwa.

Tofauti zilionekana wazi hata wakati wa kampeni. Morogoro wakati JK akijisifia kwamba amelitoa taifa mbali na hadi kulifikisha hapa kafany akazi kubwa, mgombea uraisi alisimama na kucrush kwa nguvu kwamba tumefika hapa sababu ya ufisadi tu!.

Anachokifanya JK kwa sasa ni unafiki kama asili ilivyo ili kujaribu kujivalisha kinga ya kutumbuliwa kwake, familia yake na watu wake wa karibu kitu ambacho naona kama kinatoa harufu ya kufanikiwa. Lakini leo ikitokea Mkwere au mmoja wa watu wake akawa raisi, mtaona JPM atakavyofanywa!. Msisahau jamaa anaendeshwa na utashi wa visasi na vinyongo, vikipaliliwa na ubaguzi na upendeleo. Kama Saddam vile!.

Kusema wameanza leo kutofautiana ni kujaribu kufupisha historia kwa kuondoa mizizi.

Filamu ndiyo inaanza. Hapa niutangulizi. Kwa undani zaidi, stay connected!

Ciao!.
Hujui chochote magufuli alikua ndio chaguo la jk na chenga aliyo wapiga hakika hamtaisahau
 
Jk Mnafiki Sana. Anawasukumizia Mizigo Watendaji Kwenye Vikao Vya Chama Kisha Akija Hadharani Anakenyua Tu
 
Mapovu yanakutoka kwa chuki binafsi ulizonazo kwa Kikwete huna lolote,kwa vyovyote iwavyo juwa kuwa alipofikia Magufuli Kikwete ana mchango kwani kama angehamua kumtema kwenye baraza la mawaziri isingeshindikana eti kwa kulikuwa na hizo kelele za watu kutaka apewe uwaziri
Nawewe utumiage akili hata kidogo basi
 
Hawa watu hawajawahi kuwa pamoja siku zote za umaarufu wao. Kumbuka wakati JK alipoingia madarakani alimfanya nini Magufuli. Pamoja na malalamiko kama si maombi anuai ya watu kwamba apewe wizara ya ujenzi ama uwaziri mkuu, ndivyo kasi,ari na nguvu zaidi ya kumdidimiza kwa lengo la kumpotezea kabisa ilivyoshika kasi ingawa jamaa alikomaa kila alikosukumiwa.

Kumrudisha wizara ya miundombinu ilikuwa ni aibu tu kutokana na fedheha zilizokuwa zikifanywa na wateule wa jk.

Kwenye uchaguzi wa mgombea wa CCM kila mtu anajua hata hawa wawili wanajua kwamba JPM hakuwahi kuwa chaguo la Jk hata katika tatu bora hakuwemo. Upepo wa anguko la kishindo la CCM ndio uliomsukumia embe JPM lakini hakuna asiyefahamu kwamba hakuwa mlengwa.

Tofauti zilionekana wazi hata wakati wa kampeni. Morogoro wakati JK akijisifia kwamba amelitoa taifa mbali na hadi kulifikisha hapa kafany akazi kubwa, mgombea uraisi alisimama na kucrush kwa nguvu kwamba tumefika hapa sababu ya ufisadi tu!.

Anachokifanya JK kwa sasa ni unafiki kama asili ilivyo ili kujaribu kujivalisha kinga ya kutumbuliwa kwake, familia yake na watu wake wa karibu kitu ambacho naona kama kinatoa harufu ya kufanikiwa. Lakini leo ikitokea Mkwere au mmoja wa watu wake akawa raisi, mtaona JPM atakavyofanywa!. Msisahau jamaa anaendeshwa na utashi wa visasi na vinyongo, vikipaliliwa na ubaguzi na upendeleo. Kama Saddam vile!.

Kusema wameanza leo kutofautiana ni kujaribu kufupisha historia kwa kuondoa mizizi.

Filamu ndiyo inaanza. Hapa niutangulizi. Kwa undani zaidi, stay connected!

Ciao!.
Aisee Rais kaongea jambo la busara sana hapo. Mungu zidi kumshushia hekima Rais wetu.
 
Hii mada inashtua mioyo kwa vile kila mtu mwenye akili ya wastani anajua kuwa watu hawa wawili hawafanani kabisa kisiasa na kiutawala. Kuna siku watatofautiana hadharani kweupee na haitakuwa poa. Kwa hiyo suluhisho ni JK kuachia uenyekiti tu mapema akiwa bado anaheshimika kabla self-control ya JPM haijaisha.

[Mafahali wawili hawakai zizi moja]
mapema gani mnataka nyie iwe wakati kashawaambia mwezi wa 7 anaachia ngazi??nyie labda mlitaka mapema iwe mwezi wangapi labda??
 
Nawewe utumiage akili hata kidogo basi

Usiongee na watu wasiojitambua ambao akili zao huchanua kwenye mzunguko wa taarabu tu. Mtu hata anachokiandika hakieleweki kama anakaanga dagaa na nyanya ntole, unaongea naye ili iwe nini? Watu kama hawa kuwajibu ni kujidhalilisha tu!.
 
Nawewe utumiage akili hata kidogo basi
Unataka kusema alipendelewa?
Hapana alitaka kumpoteza kwa style ya kumpa wizara ambazo hazisound ili baadae aachane nae, nini kilimfanya amrudishe miundombinu?
Wewe Ngosha aliibeba CCM kuliko unavyodhani, kwa maoni yako nani angeweza kusimama na kufanya kazi ya kuomba imani binafsi kama alivyofanya Magufuli? maana CCM ilikuwa haiuziki kabsaaaaa.....!!
 
Huwa nashindwa kabisa kumuelewa Kikwete.Jamani, kalishwa nini na Wazungu?Yaani yeye ni kutetea uovu tu.Nadhani kwa mtu aliye timamu Magufuli alipaswa kupongezwa kwa kazi nzuri anayofanya pamoja na vikwazo vyote anavyowekewa hasa na wana CCM.Ni Kikwete huyu huyu katika sherehe za miaka 39 aliyemsifu JPM na kusema yote anayofanya JPM ndiyo chama iliyoazimia kufanya na yako kwenye ilani ya chama.Nakumbuka siku ile alisoma ilani ya CCM.Lipi baya alilofanya Magufuli kwenye uchaguzi wa Meya Dar es Salaam.Alitaka CDM waporwe ushindi wao?Nini sasa maana ya democrasia?

Na lini CCM watajifunza kutokana na makosa yao?
Swali lako ktk aya ya mwisho ni swali ninalojiuliza mimi pia, sikutegemea kwa namna ambavyo Magufuli aliibeba CCM na kuwafanya warudi katika ramani, badala ya kujisafisha wasirudie makosa wanarudi kulekule. Cha kushangaza zaidi ni kama hawajui wanafanya kazi na mtu wa namna gani haswa, wanaendekeza unafiki kwa mtu ambaye si mnafiki, hawawezi kushtuka kuwa, anaweza asipendwe ndani ya Chama lakini kwa kutokuwa mnafiki kwa wananchi upinzani ukaunga mkono jitihada zake, na hivyo akaendelea kuongoza kwa heshima yake binafsi na si ya chama mwisho wa siku akimaliza muda wake wapinzani wataaminiwa kupitia kwake na kushika uongozi wa juu wa nchi, na huo ndio uwe mwisho wa zama za CCM.
Wapo wanaoweza kuchallenge logic hii kwa maelezo tofautitofauti km kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae, lkn pia si lazima iwe hivyo sio wabunge wote wa ccm ni wanafiki, ni watu wachache sana ambao hutaka kulobby utashi wa maamuz ya watu wengine na si lazima iwe hivyo pia, (kumbuka jinsi jitihada za kumwokoa Lowassa ktk kashfa ya Richmond zilivyogonga mwamba na kushangaza wengi mwisho akasurrender uPM, watu hawakutaka kuwa wanafiki ndani ya chama chake mwenyewe)
Ninachojua watakaojibainisha kuwa kinyume na Magufuli watajihalalalishia kuenguliwa na wananchi 2020, simple like that
 
RAIS Dk. John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, wameanza kutofautiana hadharani.

Kwa kasi, kutokupepesa macho ana kutokumung’unya maneno kwa Rais Dk. Magufuli, wengi walitarajia kwamba siku moja, isiyo na jina, angemwambia Mwenyekiti wake kwamba hapana. Raia Mwema limeambiwa kwamba siku hiyo ilikwishakutimia, bila shaka ikiwa ni mapema mno, pale kwa mara ya kwanza, hali hiyo ilipojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama chao kilichofanyika kabla ya Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mwezi uliopita.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika Dar es Salaam, Kikwete alieleza kutofurahishwa kwake na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa wakiunga mkono kufanyika kwa uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam uliomwibua Isaya Mwita, kutoka katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba Kikwete alikuwa amepewa taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM na wa jumuiya za chama hicho kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hawakisaidii chama jijini Dar es Salaam.

“ Hivi watu wa serikali au mawaziri ni watu wa namna gani hata wasitii maagizo ya chama chao? Hivi bila CCM nani angekuwa waziri au kiongozi wa serikali. Hii ni tabia ya ajabu sana,” chanzo chetu kilimnukuu Kikwete akisema maneno karibu na hayo.

Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu waliohudhuria mkutano huo, aliliambia gazeti hili kuwa Kikwete alionyesha kukerwa na jambo hilo na alizungumza kwa ukali. Gazeti hili limeambiwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliotoa lawama nyingi kwa mawaziri wa Magufuli na serikali kwa ujumla ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba.

Sofia mwenyewe anadaiwa kupokea taarifa nyingi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM waliokuwa mstari wa mbele kutaka uchaguzi huo wa Meya usifanyike.

Inaelezwa ya kuwa wakati wajumbe wakiwa kimya baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti Kikwete, Dk. Magufuli aliomba nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti alimruhusu. Katika maelezo yake, Magufuli ambaye anahudhuria vikao hivyo kwa sababu ya wadhifa wake wa urais, aliwatetea mawaziri wake kwa kufuata sheria na si kuyumbishwa na wanasiasa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia maelezo yako kwa makini. Naomba kusema kwamba haya matatizo yaliyopo sasa yalitengenezwa na sisi wenyewe na wengine waliosababisha haya matatizo wako humuhumu.

“Wakati wa Uchaguzi Mkuu, kuna wenzetu walitusaliti wakiwa ndani ya chama. Sasa baada ya chama kushindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya usaliti wao, leo wanataka mawaziri wavunje sheria kulinda usaliti wao.

“Hili kwa kweli Mwenyekiti hatuwezi kulitetea. Kama usaliti ulisababisha Ukawa wakashinda Dar es Salaam, basi tuache nasisi tuonje machungu ya usaliti. Kwa kufanya hivi tutajifunza kuwa usaliti si mzuri. “Kama mawaziri au watumishi wa serikali watakuwa wanafuata sheria kwenye shughuli zao, mimi nitawatetea. Lakini hatuwezi kuwasema kwa kufuata sheria na kuwaacha wasaliti ambao ndio wametufikisha hapa,” chanzo chetu kilimnukuu Magufuli.

Raia Mwema limeambiwa kuwa baada ya maneno hayo ya Magufuli, Kikwete aliahirisha mkutano huo ili wajumbe wakapate mapumziko ya chai. Kwa kawaida, kwenye vikao vigumu vya chama, Kikwete amekuwa na tabia ya kuahirisha vikao kwa muda wakati anapoona joto la mkutano limepanda na ni tabia hii ndiyo iliyofanya Uenyekiti wake uvuke baadhi ya vihunzi vigumu.

Wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais wa CCM mwaka jana, Kikwete alikuwa akitumia mbinu hiyo ya kuahirisha mkutano kwa muda mfupi na wakati mwingine kuchelewesha kuanza mikutano; akisubiri “joto la wajumbe lishuke”.

Sofia Simba na Madabida Katika duru za CCM, baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaamini kuwa Mwenyekiti huyu wa UWT bado yuko karibu na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema na Ukawa,Edward Lowassa. Kwamba wakati wa uchaguzi wa mwaka jana, hakupambana sana kuhakikisha Dk. Magufuli anashinda.

Mwaka 2009, wakati Lowassa akiwa anasakamwa na kashfa ya Richmond, Sofia Simba alijitokeza hadharani na kutamka kwamba katika CCM hakuna “mwanamume kama Lowassa”. Julai 11 mwaka jana, majira ya saa saba usiku, yeye, Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa, wote wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, walitamka kwa waandishi wa habari kutokukubaliana na maamuzi ya CC kukata jina la Lowassa.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Nchimbi alisema kwamba wao watatu hawakukubaliana na maamuzi ya hayo ya CC iliyoketi chini ya Kikwete na “kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu”.
“Katika kikao cha leo Kamati Kuu haikupokea majina yote yaliyojadiliwa na Kamati ya Maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni.

Pili, Katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika kwa manufaa ya wachache wasiokubalika,” alisema Nchimbi wakati huo kwa niaba ya wenzake hao wawili.

Kwa sababu hiyo, Nchimbi alitamka kwamba yeye na wenzake hao wawili wamewataarifu wenzao kwamba wamejitenga na uamuzi wa kikao hicho na kutangaza kutokuuunga mkono. Madabida naye amekuwa akifahamika kama mfuasi wa Lowassa kwa muda mrefu; akiwa mmoja wa viongozi waliohudhuria mkutano wa waziri mkuu wa zamani huyo wa kutangaza nia uliofanyika mjini Arusha.

Lakini, Madabida alionyesha sura yake halisi Juni 26, 2015 wakati alipotangaza kwamba Lowassa ndiye chaguo la Mungu wakati alipokuwa akizungumza kwenye mojawapo ya sherehe za kidini ambazo mgombea huyo wa Ukawa alihudhuria jijini Dar es Salaam.

Mjumbe huyo wa CC alilieleza Raia Mwema kwamba wapo wana CCM wanaoamini kwamba Madabida na Sofia ni mojawapo ya sababu za kushindwa kwa CCM jijini Dar es Salaam kwa sababu hawakupambana kama ambavyo wangepambana endapo Lowassa ndiye angekuwa mgombea.

Uchaguzi Mkuu 2015 Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, CCM kilifanya vibaya Dar es Salaam kuliko katika wakati mwingine wowote katika historia yake; kiasi kwamba sasa jiji hilo muhimu zaidi nchini, linaongozwa na Upinzani.

Katika Wilaya ya Ilala, CCM ilipata madiwani 22 kulinganisha na 30 wa vyama vilivyo kwenye Ukawa huku kikipata madiwani 15 katika Wilaya ya Kinondoni kulinganisha na 36 wa Ukawa. Ni Temeke pekee ambako CCM ilipata madiwani 29 kulinganisha na 17 wa Ukawa.

Kutokana na hali hiyo hiyo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, anatoka katika chama cha Chadema, pamoja na mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala. Ni Temeke pekee ambako CCM ina Meya.
Magufuli na wasaliti Wakati wa kampeni za kusaka urais, Dk. Magufuli alikuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu wasaliti walio ndani ya CCM; akisema kwamba mchana wanakuwa nao lakini usiku wanafanya kazi za Upinzani.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais, Dk. Magufuli akizungumza katika Ofisi Ndogo za CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam alitangaza hadharani kwamba yeye hatavumilia wasaliti kama alivyokuwa Kikwete.

Chanzo: Raia Mwema

Kikwete ndo "mastermind" so magufuli hana say kwa former.
 
Back
Top Bottom