Kikwete: MZEE NYERERE

kumbe mwalimu naye alikuwa hafai. Kwa nini kupipeleka barua yake kwa mkuu wa majeshi wakati inajulikana alikuwa ameandika juu ya ufisadi wa gen sayore. Kumbe naye mwalimu alikuwa analea mafisadi.
 
Jibu mbona rahisi kabisa. HAMKUBALI kwamba ni baba wa taifa hili kama wale mashehe wake. Maana huwezi kumuita baba yako MZEE SOMEBODY, ila kama ni mzee wa mtaani vile hutajiuliza mara mbili kumuita MZEE SOMEBODY.

mkuu, nauliza ya kwa kwamba ni kwanini Ndugu Mrisho Kikwete, huwa hayuko tayari kumuita Nyerere, "Baba wa Taifa".
Maana leo amezihirisha kabisa kwa kumuita MZEE NYERFRE
 
Ulidhani Kikwete ampende Nyerere wakati anajua fika angekuwa hai hata huu urais angeusikia maana alimjua alivyo wa hovyo kuliko mtu mwingine? Analipiza kisasi kichini chini. Mara hii mnasahau jinsi Kikwete alivyo bingwa wa kulipiza visasi!

Wakati Mwalimu akiugua pale St Thomas London, wakati huo JK ni Waziri wa Mambo ya Nje, alipita London juu kwa juu. Jamaa wa ubalozini wakamuuliza vp hupiti hospitali kumwona Mwalimu. Jibu lake lilikuwa rahisi,m huyu jamaa kaninyima urais kwa nini nikamwone? HUyo ndo JK kwa taarifa yenu. full visasi, both live and silently!
 
mkuu, kumbe tabia nyingine tuzionazo ni "inborn character" hata tumchukie vp na kuandamana, haitatusaidia wala kumuondolea kitu. Kweli kuna haja ya kuzidi kumuomba Mola atuvushe salama.
 
Ungezaliwa hospital na kupata malezi bora . Usingepoteza muda kutafuta unafiki
 
Bw. Kinana na Mangula wametukataza hayo.
Kuhusu u Dr, hata mi nilipohapa naweza kua Dk. Ila siwezi kuwa "Baba wa Taifa"

Kwani 'Ubaba wa Taifa' alipewa na nani? Na je kwenye Katiba kipo hiko cheo? Je kuna ulazima wowote wa kila mtu kumita Nyerere baba wa taifa? Na ni ipi hukumu ya mtu asiye mwita Nyerere baba wa Taifa?
 
Kwani jina la baba wa taifa kapewa na nani? Kwani watanzania walihusishwa kwenye kutoa jina hilo? na kama walihusishwa kivipi?
 
kwani ni lazima atamke baba wa taifa, kwani akisema Mzee si inajulikana anamlenga nani, hata akisema Rais wa awamu ya kwanza inajulikana ni Baba wa Taifa tu.

Mtu aliyekwishatangulia mbele ya haki na mtu mwenye hadhi huwezi kumwita mzee. Itakuwa kiroja leo uwasikie Wamarekani wanamwita George Washington, au Abraham Lincoln, mzee. Lakini kwa Kikwete naelewa kwa nini inamuwia taabu kumwita Mwalimu Nyerere baba wa taifa. Kumwita mzee ni kama vile anampunguzia hadhi yake katika fikra zake. Very sad. Kwani kuna shida gani kutaja marehemu Mwalimu Nyerere, au marehemu Nyerere peke yake?
 
Hamna kitu hapo mzee bado ni neno la heshima. kuweni wazi mueleweke mna maana gani mbona mnazunguka zunguka. Kila mtu anaweza kumuita baba wa taifa kadri aonavyo inafaa na hatujaambiwa sehemu yoyote ile kuwa lazima tuseme Baba wa taifa, ukisema Rais wa kwanza wa Tanzani inajulikana, ukisema waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika inafahamika. Acha utoto.
 
Mabadiliko yoyote katika tabia,mabadiliko katika sera, lazima yatazamwe kwa makini. Kumbuka sasa hivi tulikuwa tunaongea kuhusu replicas na robotoids. Huyu mtu alipokuwa inducted katika CCM alikuwa ultra revolutionary. What is his ideology today?
 
mkuu, nauliza ya kwa kwamba ni kwanini Ndugu Mrisho Kikwete, huwa hayuko tayari kumuita Nyerere, "Baba wa Taifa".
Maana leo amezihirisha kabisa kwa kumuita MZEE NYERFRE
Unakumbuka ile siredi iliyowekwa humu ya kumvua nyerere u baba wa taifa?
 
Kwani jina la baba wa taifa kapewa na nani? Kwani watanzania walihusishwa kwenye kutoa jina hilo? na kama walihusishwa kivipi?
Inaonyesha hata maana ya Baba wa Taifa hujui, inasikitisha na kushangaza,
Naomba nikuulize swali, Wewe ulihusishwa ktk kumuita Baba yako mzazi Mkuu wa familia.
 
Kwani 'Ubaba wa Taifa' alipewa na nani? Na je kwenye Katiba kipo hiko cheo? Je kuna ulazima wowote wa kila mtu kumita Nyerere baba wa taifa? Na ni ipi hukumu ya mtu asiye mwita Nyerere baba wa Taifa?
Kwani baba yako mzazi huo ubaba alipewa na nani, na je hicho cheo kwenye katiba kipo? Je kuna ulazima wa kila mtoto hapo kwenu kumuita baba yenu baba? Na ipi hukumu ya kutomuita baba yenu mzazi BABA?
 
Hiki kizazi cha leo kizazi kisicho na heshima, mungu atakilaani na kukifutilia mbali.
 
Unakumbuka ile siredi iliyowekwa humu ya kumvua nyerere u baba wa taifa?
hapana somo! Sikubahatika kukutana nayo. Kumbe ilifikia hadi hatua hiyo? Ilianzishwa na Mtanzania anayeijua Tanzania au?
 
Mabadiliko yoyote katika tabia,mabadiliko katika sera, lazima yatazamwe kwa makini. Kumbuka sasa hivi tulikuwa tunaongea kuhusu replicas na robotoids. Huyu mtu alipokuwa inducted katika CCM alikuwa ultra revolutionary. What is his ideology today?

mkuu binafsi sijakuelewa vizuri. Ila nikitafakuri kiundani nahisi unamaana kubwa na pana. Waweza inyambua hoja yako kiundani???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…