Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Tunasubiri miaka 2 Kigoma iwe kama Dubai

Hiyo sahau kwani kama ni utapeli tumeshatapeliwa mengi mkoani Kigoma. Hiyo Dar au Dodoma miji mikuu ya nchi haijawa kama Dubai itawezekanaje Kigoma?? Eh mtama, Leka Dutigite
 

Tunasubiri meli ya ziwa nyasa, TAnganyika na reli ya umeme kutoka dar hadi kigoma. maji kutoka ziwa victoria hadi tabora usijidai umesahau mkuu wa nchi
 
Hili niliwahi kulisema hata huko nyuma. Katika ujenzi wa barabara, JK amejitahidi. Nimepita mikoa karibu yote ya Tanzania, hakuna hata mkoa mmoja ambapo hakuna ujenzi wa barabara unaoendelea kwa kiwango cha lami. Kwa hilo whether ni hela ya mkopo au misaada, mimi kwa dhati ya moyo wangu nampongeza JK. Na mimi ni mwumini mzuri wa ukweli kuwa ni nadra binadamu kuwa mzuri katika kila jambo, JK ana mazuri yake. Wakati tunampinga maeneo ambayo hakufanya vizuri lakini tunawajibika kumfanya alipofanya vizuri.

Kama amejenga kwa mkopo laikini amekopa kwa jambo jema, basi watakaokuja watumie hiyo infrastructure kuzalisha na kulipa deni, sioni ubaya.

JK amejitahidi sana kujenga miundombinu japo hela zenyewe za madeni na sijui atakuja kulipa nani.
barabara ya kutoka singida hadi arusha ni moja ya sehemu zilikuwa zinaniudhi sana!!
HONGERA JK JAPO CCM mwisho wao ni 2015
 

badala ya kutekeleza ilani wamekuwa mabingwa wa kupambana na vyama vya upinzani maana sasa hawana tofauti na vyama vya upinzani
 
Bahati nzuri kauli yake hii anawalenga zaidi wapinzani wake kisiasa hasa ndani ya CCM!
 
mkuu, hawa hawajui hata maana ya ilani. hawajui pia kama serikali ya ccm inatekeleza ilani yake
mtaendelea kutumia neno '
ILANI' na SERA ktk dunia hii ya utandawazi mpaka lini? Maccm chorus zilezile
 
Aidha, Rais Kikwete amewashangaa baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na wananchama kushindwa kuzungumzia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya CCM na badala yake wamekuwa hodari wa kujadili wanapobezwa na wapinzani"

Source: Mwananchi

Maendeleo si mdudu mdogo hadi yaonekane kupitia darubini. Maendeleo kama yapo huonekana na kila mtu maana maendeleo ya kweli ni ya watu si vitu. Hata ukihubiri kuanzia asubuhi hadi jioni kuwa ccm imeleta maendeleo wakati hali ya maisha kwa watu walio wengi inazidi kuwa duni wewe muhubiri wa hayo "maendeleo" utakuwa unatwanga maji kwenye kinu ukitegemea kupata unga. Hivi mtu aliekuwa na njaa na akapewa chakula akala na kushiba anahitaji kuelezwa kuwa ameshiba??? Hivi ni kwani nini kikwete na ccm yake hiii hataki kuamini kuwa Watanzania tuna akili za kutambua zipi ni pumba na upi ni mchele?????
 

Sawa pamoja na hayo CCM lazima ife 2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…